Punguzo la P.A.Y.E Kwa Asilimia 1 ni Dhihaka kwa Wafanyakazi!

Punguzo la 1% (kutoka 15% hadi 14%) kwenye kodi ya mishahara (PAYE) ni dhihaka kwa wafanyakazi wa Tanzania kwani gharama za maisha ziko juu sana kufuatia mfumuko mkubwa wa bei. Ifike wakati sasa serikali iwaonee huruma wafanyakazi kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi badala ya kufawafanyia mzaha kama huu. Wafanyabiashara wakubwa na mafisadi kibao wanasamehewa kodi lakini mfanyakazi masikini anazidi kukandamizwa tu kila kukicha. Hii haikubaliki hata kidogo.

Kwa jinsi serikali ilipokuwa inatamba kwa mbwembwe kwamba itapunguza kodi ya mishahra, sikutegemea kwamba mwisho wa siku wangekuja kupunguza kiasi kidogo kama hiki cha kodi. Ni aibu kwa kweli. Wafanayakazi mnanapaswa kutambua kwamba seriklali ya CCM haina nia njema katika kuwapunguzia ukali wa maisha, hivyo basi fanyeni uamuzi sahihi hapo mwaka 2015 ili kurejesha nidhamu kwa serikali hii isiyokuwa na mwelekeo. 

Kana kwamba hili halitoshi, bado wafanyakazi hao hao watakamuliwa Tsh 2500 kama kodi ya kumiliki simu kwa kila mwezi! Wananchi mmnatakiwa kuacha uzezeta—amkeni tukawafundishe adabu hawa mafisadi mwaka 2015. Saa ya ukombozi ni sasa. Bila kufanya hivyo, tutaendelea kukandamizwa hadi mwisho wa dahari. 

Tafakari, chukua hatua!
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ngoja tutaifundisha kazi CCM 2015 maana wamejisahau sana,tutarudia tulichofanya 2010 hadi J.K akaambulia aibu na kushuka kura za rais baada ya kututukana wafanyakazi pale Diamond Jubilee alipokua anaongea na ma CCM aliowavalisha koti la Wazee wa DSM. Hii serikali ya mafisadi mwisho wenu umekaribia

    ReplyDelete
  2. Wamejisahau madarakani sana hawa shibe mwanamalevya.baba pumzisha wasanii kufa hamia bungeni kila fisadi papa unaemuona kwajicho lako asife ILA mtaabishe mpaka akutafute ulipo.namaanisha kama nifisadi papa mpe misukosuko kwendambele.maramiradi iyumbe,Mara auguliwe auguze mpaka akome,yemwenyewe Aumwe ajitibie tu,kufa asife ilachamoto kimhudumie.uwataabishe mpaka wakutafute mungu wajekutubu.tumewachoka sana.kila aliesoma hapa naaseme amen.mungu shuhulikanao wanatesa watuwahali yachini.wapige majibu kama ulivyompiga ayoub mwanzo mwishoo.

    ReplyDelete
  3. yaan mfanyakazi wa kitanzania ananyonywa mpk mwisho tunakatwa bima ya afya ila nenda na mkadi wako hospitali haki kama huna cash unakufa hivi hivi kwann msitugaie mshahara wetu km tulivyosign tu hayo makato yatasaidia lini

    ReplyDelete
  4. Haki ya MUNGU aliyekojuu hamuoni aliyechini! hv mbwembwe zote za punguzo la makato kwnye mshahara ni 1%!! amakweli hatupo kwa ajili ya wengine.

    ReplyDelete
  5. Bila ya Aibu mtaona hawa hawa wafanyakazi wanaonywa wanairudisha ccm madarakani 2015

    ReplyDelete
  6. Maaninestic ccm to hell chama cha mafisadi,chukua chako mapema.alale Pema peponi kamanda alale pema peponi kamanda.nani aonywe waloge kwavishindo vyote ilawengine hatuwataki nahatutawachagua.

    ReplyDelete
  7. soma hapa jinsi ya kutengeneza pesa kupitia kwa computer yako

    ReplyDelete
  8. Imefika sehem hii nchi wanaiona km yao na Familia zao,wana hatimiliki ya nchi ya nchi hii,Time for changes....Tuwang'oe wajifunze...

    ReplyDelete
  9. hawa magamba wanatutesana, manina zao! mwisho wa mateso yote haya ni 2015. tuache kulalamika sana, tutakutana nao kwenye sanduku la kura.

    ReplyDelete
  10. We umeongea ILA niwezisana hao chama tawala.wataibakura ilalazima tuwanyooshe madarakani vyama vyaupinzani viwevingi bungeni tuongeze idadi mamayo zao wamejisahausana.tuwanyime Kura.natusiwe waoga amani haiji kwa upole mtu anakudidimiza bado unamchekea kwakumuogopa.toa makucha mteme ajue kabisa humtaki tuwakomeshe washenz sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad