Jk Atumia Dakika 15 Kumfagilia Diamond

Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”

“Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua wazi Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni tuzo kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa kwake kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo wake ni njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena kuchukua tuzo hizo,”

“Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond  na wasanii wengine wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye ulimwengu wa muziki”,

“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.

Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana rais wetu .....kwa upande wangu nakupenda sana jinsi unavyojali watu wako unaowaongoza.....mungu akulinde na madhila ya dunia pamoja na mahasidi....Na akujaaliye mwisho mwema.....inshaallah.....

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. Uku kwenye Udaku bila storY ya Wema Sepetu sioni raha.tuwekeeni stori za Wema Sepetu .

      Delete
  3. Yaani we mzee huna future hata kidogo unaacha kuwaza vitu vya msingi unaongea pumba zako, unamatatizo ya kufikir we mzee na domo wako poleni sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndie usie na future unaecoment pumba,nyooo

      Delete
  4. Pumbavu zako ww una future gan hpo ulipo?km amna cha kucomment funga bakuli lako cyo yote anayofanya kikwete ni mabaya mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ingawa ckukubali president ila sometimes unafanya vitu vya maana

    ReplyDelete
  5. Kweli waTz hatuna uzarendo ns nchi yetu tunaichafua nchi yetu kisa kwa chuki binafsi sio vzr.Baadhi ya wasanii hawajfny kitu kizuri kumponda mwenzao wazi wazi

    ReplyDelete
  6. well done mr president

    ReplyDelete
  7. Kampeni ya CCM next year mpe Nasibu

    ReplyDelete
  8. Lovenes aka divathepumbu umemsikia kikwete

    ReplyDelete
  9. Nasikia loveless diva Wa clous alikuwa anammwndea diamond ili amchune.anadai Hana mapenzi Ni pesa tuuuuuuu anachotaka kwa wanaume

    ReplyDelete
  10. Thats nice of u baba Liz...............Diamond sky is a limit all the best kaka, hata mbuyu ulianza km mchicha.........never loose hope

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad