Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa Malawi.
Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.
Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpya wa kutaka kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.
Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na Tanzania ni kupoteza muda.
“Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa la Malawi daima,” alisema Mutharika ambaye pia amewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alimshutumu Banda na kudai alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursa kwa Tanzania kutumia udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.
“Ziwa hili letu ila Tanzania inatumia tu udhaifu wa Serikali iliyopo kwani wenyewe wanajua ndani ya mioyo yao kuwa hawana chochote katika ziwa hilo. Tutakaporejea serikalini mwakani haya mambo yote yasiyo na kichwa tutayamaliza. Nataka niwahakikishie kwamba tutapeleka meli zaidi kwenye ziwa hili ili kuinua shughuli zetu za kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu.”
Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali ya Tanzania ilitoa msimamo wake kuhusu mzozo huo wa mpaka na kudaia kuwa itaendelea kujadiliana na Malawi.
Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya kazi na serikali yoyote itakayoingia madarakani.
Waachieni tu tatizo ni nini?
ReplyDeleteWeee hebuangalia mfano mdogo tu,unaweza kuniambia bahari ya feri je ni yaupande wa posta au kigamboni au yao wote?
ReplyDeletemtapigwa magharibi kusini kaskazin na north est by kenya so mko wapi wenzangu
ReplyDeleteKama vp tuwaachie tu ili amani iendelee ndani ya nchi yetu
ReplyDeleteRais mwenyewe wa malawi ndo kabomoka hivi duh, iyo sura kama kalamba ndimu vile itakua roho yake na sura vinaendana
ReplyDeletemdau 1:15 una maana kenya itatupiga!! au? kwani wamemalizana na alshabab? yaani jamaa wametulia siku mbili hizi wanavuta kasi mnaanza kuropoka ni wa ajabu nyie.
ReplyDeletewee mdau 1.15 wewe ni wa wapi,boko haram au?BRING OUR GIRLS BACK.
ReplyDeleteuyo nae ndo walewale ana kauli ya dada ake ya kugombea ziwa nyassa, waachien bac watajirike
ReplyDeleteHuyu anataka bwana huyu... sio bure... na atapata tu.
ReplyDelete