Mshambuliaji wa klabu ya Man utd pamoja na timu ya taifa ya Uholanzi Robin Van Parsie amesema yupo fit kwa ajili ya kulitetea taifa lake kwenye fainali za kombe la dunia ambazo zitaanza kuunguruma siku tatu zijazo huko nchini Brazil.
Robin Van Parsie ametangaza kuwa tayari kwa ajili ya fainali hizo, akiwa mbele ya waandishi wa habari nchini Brazil ambao walitaka kufahamu maendeleo ya afya yake ambayo kila mara imekua ikikumbwa na mushkel.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema hakuwahi kuwa fit kama ilivyo sasa, hasa ikizingatiwa alikuwa akitumikia mchezo wa soka kwa kipindi cha miaka sita iliyopita kwa uchungu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili.
Amesema baada ya kutaabika kwa muda mrefu hana budi kulishukuru jopo la madaktari lililomtibu na kufikia alipo sasa na pia anaamini jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Uholanzi wanajua namna ya kukabiliana na hali yake pale itakapokwenda tofauti.