Sakata la Mumewe kusota Rumande Kwa Ubakaji….Flora Mbasha Ajikuta Akiambulia AIBU ya Mwaka.

Wakati jana mumewe Emmanuel Mbasha (32) akipandishwa kizimbani kwa mara ya pili kwa soo la ubakaji wa shemejiye, mwimba Injili kinara Bongo, Flora Mbasha (31) amepitia katika hatua tatu za aibu.
 
Mbasha ambaye naye ni mwimba Injili na mfanyabiashara alitarajiwa kupandishwa kizimbani jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilala, Dar akitokea mahabusu Keko akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Flora ambaye alihama nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza, Dar, kitendo hicho kilimuingiza staa huyo kwenye hatua ya tatu ya aibu na kujikuta akiwa katika masikitiko makubwa.

AIBU YA KWANZA
Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, aibu ya kwanza inayomuuma Flora ni ile ya ndoa yake kuingia kwenye gogoro kisha kudaiwa kutengana na mumewe kinyume na kile anachokihubiri kupitia nyimbo zake zinazopendwa na wengi ndani na nje ya Bongo.
 
“Unajua lile neno la ‘mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ (Mithali 14:1) linamfanya awe na aibu mbele za watu.

“Unaambiwa kanisani (anasali Kanisa la Ufufuo na Uzima la Mchungaji Josephat Gwajima kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar) anaona aibu hasa kwa waumini wenzake.

“Flora amedumu na Ima (Mbasha) kwenye ndoa kwa miaka 12 hivyo kutokea kwa kilichotokea ni aibu kwani tayari walikuwa wamekomaa tofauti na walipoona wakiwa na umri mdogo.

“Hebu fikiria, mtoto amekuwa mkubwa, anaposikia mama ana matatizo na baba si ni aibu jamani? Cha msingi tuwaombee wamalize matatizo yao, inaweza kusaidia kuifuta aibu hiyo kwani imeandikwa ‘Ndoa na iheshimiwe na watu wote…’ ( Waebrania 13 : 4 -),” alisema mnyetishaji wetu akisisitiza kuwa akitajwa  ataonekana mvujishaji wa mambo ya siri ya wanandoa hao.
AIBU YA PILI

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa aibu ya pili inayomkabili Flora ni skendo ya yeye kudaiwa kuhamishia makazi kwa mchungaji wake, Gwajima.
 
Katika aibu hiyo, mumewe alinukuliwa na gazeti la Uwazi akimlalamikia mchungaji huyo amwachie mkewe kwani yeye ndiye alisababisha sakarakasi zote hizo za ndoa yake.

Ilidaiwa kuwa kwa mke wa mtu achilia mbali mhubiri kwa njia ya nyimbo, kitendo cha kukumbwa na skendo nayo ni aibu pia.
 
“Kwa mtumishi kutajwa kwenye jambo kama hilo lisilo na mrengo wa kupendeza masikioni mwa watu, ni aibu kuu,” kilidai chanzo hicho.

AIBU KUU YA TATU

Ilisemekana kuwa achilia mbali ndoa, mambo ya mchepuko lakini aibu kuu ya tatu kwa Flora, ni kashfa ya ubakaji wa shemejiye inayomkabili mumewe Mbasha.

“Unajua usifikirie kwamba mume akipata aibu mke anaweza kuikwepa. Hawezi kwa sababu ‘wanazungumza lugha moja’ (yaani ni mwili mmoja). Ona sasa mume anapandishwa kizimbani kwa ubakaji.
 
“Pia usifikiri watu watasema kashfa ni ya Ima peke yake. Kwanza hata kutamka watu wanasema mume wa Flora. Ikumbukwe aibu ya mume ni ya mke pia. Ni vigumu mno kwa Flora kusema aibu ni ya mumewe pekee,” alitiririka mto habari huyo.
FAMILIA ZATOFAUTIANA

Wakati hayo yakiendelea, habari zinadai kuwa familia za pande zote zinatofautiana huku kila moja ikilaumu nyingine.
Ilidaiwa kuwa upande wa Mbasha unamlalamikia mama wa Flora kuwa anamuunga mkono mwanaye badala ya kusaidia kutuliza hali ya hewa.
Ilielezwa kuwa upande wa Flora wao wanamlaumu Mbasha kwa madai kuwa chanzo cha yote ni mgawanyo wa mali hasa baada ya kuona kuwa hakuna tena ndoa.

FLORA ANASEMAJE?

Akizungumza na Ijumaa juzi kwa njia ya simu, Flora alitoa la moyoni: “Kweli naumia sana tena sana. Kwa sasa kesi ipo mahakamani, siwezi kuizungumzia lakini ndiyo hivyo. Siyo siri nateseka sana.”

Mbasha anadaiwa kumbaka ndugu wa Flora ambaye ni yatima kati ya  Mei 23 na 25, mwaka huu ambapo kesi yake inaendelea kuunguruma baada ya kukaa mahabusu ya Keko kwa siku kadhaa ambapo sheria ndiyo itakayoanika siri zote juu ya sakata hilo.

Crediti: GPL

Post a Comment

25 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. flora muongo mkubwa tena mkubwa hana haya hana anachoumia si ndio njama ya kummaliza mwenzie ili yake ya muendee sasa aibu gani aliyonayo. hana jipya

    ReplyDelete
  2. Ya ngoswe tumwachi ngoswe mwenyewe,na usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.Tambaeni huko

    ReplyDelete
  3. tuombe tuu sisi Mungu wa haki ajionyeshe

    ReplyDelete
  4. Flora sio muongo bali amechoshwa na aibu za mumewe..wanawake wengi wanavumilia aibu za waume zao mwishowe wanaletewa UKIMWI nyumbani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Makanisa mengi n'a dhambi kibao.kwa mchungaji kafuatanini kama si kuvliwa naye

      Delete
    2. Ndoa zina siri kubwa wajuao ni wana ndoa pekee

      Delete
  5. mimi jibu ambalo sijalipata bado nikwamba kwanini alivyobakwa ijumaa hakuenda kuripoti polisi mpaka alivyobakwa juma pili ndio akaenda kuripoti au cha ijumaa kilikua kitamu mpaka ukarizika na matokeo yake?

    ReplyDelete
  6. Flora ni zaidi ya jambaz huwez kumfanyia hivo mumeo!mungu atamlaani

    ReplyDelete
  7. Flora ni zaidi ya jambaz huwez kumfanyia hivo mumeo!mungu atamlaani

    ReplyDelete
  8. wasichana wanaosali na mbasha na flora wanajua aibu aliyokuwa anaipata flora.eti mume anatongoza mpaka waumini wanaokuita dada bado kavumilia kisa mume handsome,au kuogopa aibu,aaaaaah bora nikae bila kuolewa mie.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani akuoe nungayembe wewe.

      Delete
    2. Flora anajikomentia mwenyewe shetwain weee

      Delete
  9. Hivi wandugu Watanzania, kosa la ubakaji siku hizi si kosa kwa sababu limetendwa na mtu fulani au kwa sababu ni ndugu yako? Kwa nini kosa linaitwa kosa, AU dhambi inaitwa dhambi?
    Watanzania tumeingia kwenye ushabiri usiyo na maana, tumeacha ya muhimu na kujikuta tukizolewa na 'mkumbo' na makandokando yake. Hebu tutulie na kulitafakari hili, hebu tukae chini na kujiuliza uadilifu ni kitu gani?

    ReplyDelete
  10. Jamani wengine tuko kwenye ndoa miaka mingi na huwa tunagombana, vikizidi ni kuhama chumba na sio nyumba,nadhani mwanamke mwenzetu yalimzidi ndio maana kaamua kuishi hoteli,kwangu mie tutabanana hapahapa,labda atahama yeye, hatoki mtu hapa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na akikuletea ukimwi?ndo maana wanandoa wengiiiii wameathirika.

      Delete
  11. Hv jamani wadau mbona mm binafsi manyimbo ya Huyu YUDA flora mbona hayana Upako??? Eeh kweli MIMI Nina cd Kama 1000 nyumbani kwangu ZA Gosple cna ya flora hata 1.Ana makelele na maccm ndani!!! tupa kuleeee

    ReplyDelete
  12. Ndoa ni kitu kingine mwacheni flora apumzike. Mwanamke mpaka aseme bassssss kavumilia mengi wanaume hawana adabu na hawajali maumivu ya wenza wao. Nje hajarizika mpaka aje kwa ndugu yake. Yupo sawa flora kama hujaolewa ucmcheke flora

    ReplyDelete
  13. Flora naye ndio wale wale! Kwani huko hotelin nani anajua alikua analala na nani? Mbona asiende kwa ndugu zake au ndugu wa mume au hata wazamini wa ndoa? Au kwavile yy hajafumaniwa ndio hajafanya? Mtu akizini ikigundulika ndio zambi ila isipogundulika swari.

    ReplyDelete
  14. Wanaomchukia flora hawajapata masahibu yandoa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siri ya flora tunaijua Mbasha Hana Hela ndo maana kakimbia kwa Mchungaji

      Delete
  15. MAGAZETI M MEHONGWA NA MBASHA MU MPAKE MATOPE FLORA, WANGAPI WANA BAKA WANASOTEA JELA KWANI MBASHA NI NANI HASA KTK ULIMWENGU HUU KAMA KATENDA KOSA A PATE ADHABU YAKE NA KAMA HAJATENDA KOSA ATAKUA HURU.

    ReplyDelete
  16. Jamani kiuhalisia hata kama mume kakukosea nini as long as ni mumeo ni mwili mmoja huwezi kufikia hatua ya kinyama kama ya frola ulokole gani huu ucojua msamaha?hawezi kufikiria impacy ya mtoto wake wanapoanika nyumba yao magazetini frola namjua jamani sana tu yote yaliyoongelewa na mbasha juu yake ni ya kweli na mbasha c kama amembaka yule binti ni watu waliokuwa na mahucan•o na yote haya yametokea ili frola afiche aibu yake baada ya issu ya gwa••kujulikana !jamani pesa shetani frola zimemchanganya ukweli utajulikana tu ila ameyukatisha tamaa wakristo tunaimba kila cku samehe samehe yeye?namuhurumia cjui km kuna mtu atashawishika kununua kazi zake tena

    ReplyDelete
  17. Wanaume wote ni baba mmoja mama mmoja frola ackudanganye mtu wanawake wote tunalia na ndoa zetu lkn mungu ametujalia wanawake kuwa na huruma na moyo wa msamaha wanja wako pekee unaonyesha frola c mtu wa msamaha upo kikazi zaidi amka frola kaeni chini mmalize tofauti zenu kwa faida ya binti yako ataathirika kisaikolojia sana na mtt wakike kipenzi chake ni baba atakuchukia bure malizeni tofauti mfungue ukurasa mpya jifanyeni km mlikuwa mnatoa movie mpya

    ReplyDelete
  18. Flora dadangu umejivua nguo. Umejidhalilishs. Ucdhani unsmkomoa mumeo aibu yake ni yakwako kwasababu ww ndio mlezi wa ndoa yako. Mume akitoka nje jiulize vzr ww mama kwann atoke. Pole kwakuwa unyumba wako umeuanika Tz nzima tumejua. Zaid mwombee mumeo coz kipsycholojia kasha athirika

    ReplyDelete
  19. Acheni ushabiki wa kijinga mambo ya ndoa ni magumu sana. Wanaume hawaridhikagi siku zote. Mbasha hakua na sababu ya kuwa na mahusiano na shemejie eti kisa mkewe kahamia hotelini, hapa busara ilitakiwa kutumika zaidi na si kulipia . lakini pia Mbasha hana adabu inavyoonekana alikua na mahusiano na huyo shemejie what a shame! !! Flora kachoka na umalaya wa mumewe so mwacheni amfundishe , mzinzi mkubwa Mbasha nyambafffff

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad