Samweli Eto’o Aendelea Kumchimba Mourinho

SAMUEL Eto’o aliwaduwaza Ujerumani kwa bao lake juzi Jumapili wakati Cameroon ilipotoka sare ya 2-2 na Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia.

Eto’o alimzidi ujanja beki, Mats Hummels, kisha akamchambua kipa Roman Weidenfeller, lakini kubwa lililovutia kwenye mchezo huo ni ushangiliaji wake baada ya kufunga bao hilo.

Eto’o aliendeleza vita yake na kocha Jose Mourinho, aliyehoji kuhusu umri wake kwa kudai kwamba straika huyo amezeeka na hivyo staa huyo kumjibu baada kukimbia hadi kwenye kibendera za kona na kisha kushika mti wa kibendera hicho na kuigiza mzee anayetembea na mkongojo. Eto’o aliwahi kushangilia kwa staili hiyo pia kwenye mchezo wa Chelsea.

Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Thomas na Andre Schurrle kwa upande wa Ujerumani na Eric Choupo-Moting kwa upande wa Cameroon.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duh hahahaaaa umeuaaaa mkubwa we ni vitendo tu. Bora umemkomesha mourinho anachonga sana

    ReplyDelete
  2. Thank you for this fascinating post, I am happy I observed this website on Google. Not just content, in fact, the whole site is fantastic. Top Vn Bet

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad