Spain Yachezea Kichapo Cha Mbwa Koko Kutoka Kwa Holand

Michuano ya kombe la dunia imezidi kushika kasi kwa michezo miwili iliyopigwa leo.
Mchezo wa kwanza leo hii ulikuwa kati ya wawakilishi wa Afrika Cameroon dhidi ya Mexico, na wamexico wakaondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.
Mechi ya pili iliyomalizika hivi punde ilishuhudia mabingwa watetezi Spain wakidhalilishwa kwa kipigo kizito kutoka kwa Uholanzi.
Spain walianza kuliona lango la Uholanzi kwa mkwaju wa penati wa Xabi Alonso, lakini Robin van Persie akaisawazishia Uholanzi kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Uholanzi walirudi kwa kasi na kufanikiwa kuongeza magoli mengine manne kupitia Van Persie, Robben aliyefunga mawili na beki Stephan de Virj akaongeza la tano. Mpira ukamalizika kwa Spain kufungwa 5-1.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad