Tabia Kumi Mbaya Ambazo Zinazokufanya Ushindwe Kutunza Hela na Kubaki Kulalamika Maisha Magumu

1.Unanunua nguo bila mpangilio..
Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na
nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea
chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae
kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale
kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo
sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya
sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au
wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5.Unakopa hela banki na kununua vitu kama
simu ya milioni na gari ambazo sio productive.
Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini
kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi
Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako
au hamuendani kivipato hivyo unajikuta
unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili
uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa
sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe
meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye
salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako,
unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa
kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.
Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie
kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa
kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu
huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani
kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji
hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu.
Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila
anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au
mshahara wote kwenye wallet au handbag au
nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash
nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia
hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na
hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.
Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi
tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa
kufanya vitu vikubwa endelevu

Yako Namba Ngapi Hapo?

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ebu huko maisha yenyewe haya mafupi tunakufa ghafla hapo umejinyima weee hadi unapewa majina ya ajabu na pesa zako zote unaziacha aaah acha tule ujanaaa!!!

    ReplyDelete
  2. Thank you so much kaka, umetuzalau Sana Ss walimu

    ReplyDelete
  3. he he he usiwe mkristo kuliko yes.

    ReplyDelete
  4. hiyo ya roho ya huruma ndiyo tatizo langu kubwa!!

    ReplyDelete
  5. duh yangu namba moja aisee kweli nipadilike

    ReplyDelete
  6. Yah!Ni kweli kabisa ht mm zamani nilikua na baadhi ya tabia mentioned lkn tangu nimebadilika maendeleo nayaona

    ReplyDelete
  7. umesahau kuhongahonga ovyo maana unaweza ukawa na mwanamke 1 lkn huyo huyo akawa bonge la kirusi hasa kwa sisi tusio oa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad