Tabia za Mama Mkwe Ndio Tabia za Mkeo..Chukua hiyo Kubali Au Kataaa

Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.
kwanini mama mkwe?
1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake
2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye
3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acha uongo kila mtu anatabia zake mara chache sana zikafanana,
    mfano mie mama yangu ana tabia za kunywa pombe mpaka anauzi lakini mimi pombe sinywi, baba nae hivyo lakini kaka zangu hawanywi, ukorofi wa wazazi lakini watoto wapole balaa, wazazi sio watu wa imani lakini watoto wanasali sana,
    tabia inatokana na mtu mwenyewe aamue kuiga, mara nyingi watoto wanaiga sio kwamba anazaliwa nazo

    ReplyDelete
  2. kula tano mtoa mada, yaani ni mara chache sana kutofautiana kwani watoto wanajifunza tabia kwa malezi, ushauri,kuishi, mazoea, desturi, mila,kabila,mazingira, kufundishwa na kuiga.

    ReplyDelete
  3. Mmh mkikosa cha kuandika muwe mnapasua hâta kuni. Huu utafiti sijui umefanyia wapi,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umewapa wazo zuri. Au wachimbe mitaro iliyoziba

      Delete
  4. its true in other word mzazi au mlezi na mazingira alokulia determine her behaviour

    ReplyDelete
  5. Wakati mwingini tabia au mazingira ya mtoto aliko kulia,yanatokana ,na jamii husika,japo sio kwa asilimia 100,watoto wengi huwa hawapendi kuiga tabia za wazazi kama mimi,baba alikuwa na wake wengi,na kunywa,pombe,ila mimi sinywi,watoto au vijana ,wengi wanapenda kukwepa matatizo au tabia za wazazi wao,pia hata kazi,kwa kutokufanana,na wengine wanataka kufanya kazi wazazi wao walizo somea.

    ReplyDelete
  6. hii ni kweli kabisa mkuu hata mimi nina experience hiyo maishani mwangu. ukitaka kuoa angalia maisha wanayoishi wazazi wa huyo bint au kijana. je ni wacha Mungu/ wanaishi kwenye ndoa kwa muda wote au walishatengana/ mama au baba anatabia gani mbaya/. ni nadra sana watoto kutokuiga tabia za wazazi wao.

    ReplyDelete
  7. Thubutuuuuu kuoa ni sala na maombi tu,ukiangalia familia ya mpenz wako waweza ingia chaka baya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad