TFDA Yatoa Ushahidi wa ARVs ‘Feki’ Mahakamani

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imedai ilikagua na kugundua dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) zilizotengenezwa na Kiwanda cha Tanzania Pharmacentical Ltd (TPL) kinachomilikiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida ni bandia.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Osward Tibabyekoma alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa usikilizwaji wa awali wa kesi inayomkabili Madabida na wenzake ya usambazaji wa dawa hizo bandia na kusababisha hasara ya Sh milioni 148.

Licha ya Madabida ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, washitakiwa wengine ni Mkurugenzi Uendeshaji, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msoffe na Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango.

Wengine ni wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao ni Meneja Udhibiti Ubora, Sadick Materu na Ofisa Udhibiti Ubora, Evans Mwemezi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba, Tibabyekoma alidai , kiwanda cha TPL kiliingia mkataba na MSD kutengeneza dawa hizo na mwaka 2011 waliagizwa watengeneze dawa hizo.

Alidai kati ya Aprili 5 na Aprili 11 walipeleka makopo 12,252 ya dawa bandia na kulipwa Sh milioni 148.3 kupitia hundi mbili. Alidai Aprili na Mei mwaka 2012, MSD ilisambaza dawa hizo katika vituo vyake vya kanda.

Inadaiwa Agosti mwaka huo, TFDA ilipata taarifa kuwa kuna dawa hizo ambazo ni bandia, wakaagiza kila kanda ifanye ukaguzi.

Aliendelea kudai kuwa baada ya ukaguzi waligundua dawa zilizotengenezwa na kiwanda hicho ni bandia, zina mwonekano tofauti na dawa zilizotakiwa kutengenezwa hivyo waliamuru dawa hizo zirudishwe na zote zilibainika kuwa bandia.

Baada ya kusomewa maelezo ya awali, pamoja na wafanyakazi wa TPL kukiri kiwanda hicho kutengeneza dawa za ARV na kukubali kwamba waliingia mkataba na MSD, lakini walikataa kuwa dawa hizo zilikuwa bandia.

Hakimu Mwaseba aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 30 mwaka huu itakapotajwa tena na Julai 28 mwaka huu watakapoanza kusikiliza mashahidi kwa upande wa Jamhuri.

Inadaiwa Aprili 5 mwaka 2011, Madabida, Shamte, Msoffe na Fatma waliisambazia MSD makopo 12,252 ya dawa bandia, ikionesha zimetengenezwa Machi 2011 na mwisho wa matumizi Februari mwaka jana.

Wanadaiwa pia walijipatia Sh milioni 148.35 kwa madai kuwa ni malipo halali ya dawa hizo.

Materu na Mwemezi wanadaiwa, kati ya Aprili 5 na 13, 2011, Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa MSD, walishindwa kutumia uwezo wao wote kuzuia kutendeka kwa kosa hilo. Pia washitakiwa wote walisababisha hasara ya Sh milioni 148.3 kwa kusambaza dawa bandia.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hawa hawawezi kusamehewa kamwe, hivi mtu anaumwa ukimwi halafu umpe dawa feki, hili taifa jamani hapa tunakokwenda kwa ajili ya kujali maslahi yetu taifa litateketea wahlah

    ReplyDelete
  2. natamani wangekua na kesi hii china,tena naushahidi upo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sana bora ingekuwa china nina imani hatua kali zingechukuliwa lkn tz yetu hii hamna kesi na wala hawaona madhara ambayo wamewasababishia wagonjwa hao

      Delete
  3. Aisee watu wangapi wamekufa?mbona watu hawana huruma!! Wanyongwe tu hao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad