Tundu Lissu Ailipua Tena Serikali Kwa Kutoa Taarifa za Ungo

Serikali imeumbuliwa bungeni ikidaiwa kuwasilisha taarifa za uongo kupitia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ugawaji wa madawati yaliyonunuliwa kwa ‘chenji ya rada’.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alitoa tuhuma hizo jana, wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema Serikali imewadanganya wabunge kwa kuwa hakuna kitu kilichofanyika.

Alisema katika majibu ya Serikali kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa kuwa imetangaza kununua madawati 93,740 na kuyagawa katika halmashauri mbalimbali nchini wakati siyo kweli.

Alisema kwa mtindo huo, Serikali imelidanganya Bunge pamoja na Watanzania kwa kuwa imetangaza madawati hewa ambayo hayapo.

“Wabunge kama kweli mnatimiza majukumu yenu na hampo hapa kwa masilahi yenu tu, hebu hojini halmashauri zetu zimepelekewa haya madawati 93,000 yanayozungumzwa humu au mnapiga makofi tu? Serikali inadanganya tunatakiwa tuihoji tuiwajibishe,” alisema.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa mfano wa mgawo huo kwenye Halmashauri ya Ikungi, Singida kwamba ilitangazwa kupelekewa madawati 508 lakini amekwenda jimboni na hakukuta dawati hata moja.

Alisema uchunguzi wake umebaini kuwa hata katika wilaya mbalimbali ikiwamo ya Iringa, hakuna kitu kama hicho.

“Jana sikuwa hapa bungeni nilikwenda kwenye halmashauri yangu, hakuna dawati hata moja. Hata Halmashauri ya Iringa kwa Mchungaji Msigwa (Peter) hapa ananiambia hakuna dawati hata moja, mnatudanganya ili iweje?” Aliwashauri wabunge wengine kufanya utafiti katika maeneo yao iwapo kuna madawati ambayo yamepelekwa kutokana na fedha zilizorejeshwa na Serikali kama chenji ya rada.

Lissu alisema ni maneno matupu ambayo yamekuwa yakiwahadaa wabunge na kuwafanya wasahau wajibu wao wa kuisimamia Serikali na kujikuta ni washangiliaji wakati wote. Lissu alisema kinyume na taarifa hizo za Waziri Mkuu, Bunge jana lilikuwa limeelezwa na Naibu Waziri (hakumtaja) kuwa madawati hayo hayajagawanywa.

Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa akijibu swali la nyongeza la Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe - CUF), kuhusu madawati hayo, alisema kwa kuwa madawati hayo bado yanagawanywa, watakaa na kuangalia utaratibu mzuri wa kuyafikisha Zanzibar.

Lissu pia alisema fedha ambazo zilitajwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo kuwa ni pato la Watanzania ni uongo kwa kuwa ni mali ya wamiliki wa migodi.

Alisema takwimu za waziri zimesababisha Watanzania kuamini kuwa wameingiza fedha nyingi ilihali kiasi kilichoingia hakifikii hata asilimia 10 ya pato la wawekezaji.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuwa shabiki au mwanachama wa ccm kunahitaji kuachana na akili zako timamu. Serikali ya ccm inaishi kwa ghilba au uongo! Na wabunge wa ccm nao ni kama mazezeta!

    ReplyDelete
  2. safy lissu!!! hawa ccm n wahuni ukiwaacha 2!!! tutabaki 2nalia miaka hamsin...wanasema hatuna ttxo la walimu wkt kuna shule zn wlm 4-3 wnf 360:

    ReplyDelete
  3. Nina uhakika kabisa viongozi na wabunge wa ccm hawana uzalendo hiyo mtu abishe akatae!hata ukieaona bungeni wako kwaajiri ya kuteteana wao kwa wao hata kama jambo hilo ni lakumkandamiza mwanaichi wa hali ya chini!chakushangaza kuna watu anakwambia yeye ni ccm damu na ukimuona ni choka mbaya sasa sijui siasa anaona kama ni simba na yanga au?kwakifupi viongozi wa ccm wanatunyonya sana jamani!wako kwa ajiri ya familia zao na vimada wao tu kuma nina zao!

    ReplyDelete
  4. Ccm ni mbwa tu wamekaa kutuibia washenzi wakubwa

    ReplyDelete
  5. mmeonaeeeeeeeee......kwni simnajua maana ya CCM...........Chukua Chako Mapema.......kwa hiyo wanatimiza wajibu na kanuni ya chama chao hao ...........tumewachojka jamani tumesema kwa midomo mpaka tunachoka mnataka tuserme na nini?...............bha.........

    ReplyDelete
  6. Tundu Lisu ni nyoka, jimbon kwake hakuna anachofanya shule zipo tuuuu majengo hayatoshi wala nyumba za walimu hakuna.....kazuia wananchi kutoa michango ya maendeleo mashuleni wamekaa kulima viazi watoto wanaacha shule....mi ananikwaza sana hd nimehama huko kwake.mayatima aloahidi atawasaidia mashuleni kawatelekeza ....si kiongoz mzur mana yupo kama picha jimbon mwake

    ReplyDelete
    Replies
    1. We kweli umesoma wewe mbona unaongea vitu vya kipuuzi kabisa embu fikiria kabla hujaongea bhana acha ujinga

      Delete
  7. We anonymous 8.01 hapo juu ni fala tena usiyejitambua.kwani Tundu Lisu ndio tunampa kodi yetu kujenga madarasa na kuajiri walimu.rudi shuleni kasome uraia namna ya kuendesha serikali m..mbwa wewe.

    ReplyDelete
  8. Tehetehe! Eti mazezeta.

    ReplyDelete
  9. Tehetehe! Eti mazezeta.

    ReplyDelete
  10. Watanzania amkeni jamani CCM na watu wake wanatuua kijinsia na ndo maana wanarithishana tu madaraka hebu stukeni tuwatoe kuanzia serikali za mitaa hadi uraisi jamani IMETOSHA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad