Ukatili Mwingine Tena..Mfanyakazi wa Ndani Mwingine Ajeruhiwa Vibaya na Bosi Wake

HAUSIGELI aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15, ameumizwa vibaya sehemu za kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na bosi wake aitwaye Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.

Akiongea na mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina amesema amekuwa akipigwa na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia waya, brenda na vifaa vingine japo alikuwa akiogopa kusema.

Vitendo hivi vya ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku chache baada ya hausigeli aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi wake aitwaye Amina Maige aliyepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Binti huyo aliyeletwa Mwananyamala leo alfajiri akiwa na hali mbaya amefanya kazi kwa miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani Kagera.

Melina alikuwa akiongea na mwanahanbari wetu akiwa na mpira wa kuongezewa damu mwilini na amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea tukio hilo.

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna mwanamke mwenye roho mbaya huku boko kama mama rwechungura ila tulikuwa hatujui kama amefikia hatua ya kumfanya mtoto wa mwanamke mwenzie hivi,

    ReplyDelete
  2. Jamano Ina maana wanawake tayari tumesahau uchungu WA kuzaa au Ni kea watoto wetu tuu? Hapana hii Ni zaidi ya ukatili naapaa duu😰😰

    ReplyDelete
  3. jamani mimi nataka kuona serikali inafanyaje, nitafatilia kesi ya yusta, nasra na huyu tuone hii serikali inafunga macho kwa nini kwa nini jamani ninahasira sana nasubiri nione unless otherwise isipochukua hatua stahiki na tutaandamana wajuiuzuru, enough

    ReplyDelete
  4. Mmm!! hawa wanawake wa bala makatili sana pamoja na wanaume wao, ila huyo mama atukuwa muhaya makatili sana yana mioyo migumu huruma hayana, mungu hawamjui pumbavu kwenda jela

    ReplyDelete
  5. Msenge we we wanawake wa bara makatili nyokooo nyie wa pwani si ndo mnaongoza kwa roho mbaya zenu na hiyo mijanamume yenu.

    ReplyDelete
  6. Aaahh ukweli unaumaa eehh. Pwani twacfika kwa ukarimu bibiee. Ushaidi c ndio huu wote wa balaa pwani noo

    ReplyDelete
  7. Morogoro ni bara

    ReplyDelete
  8. Ndio mana mnachomewa watoto wenu.lngekua ni mimi ningemuwekea sumu ya kuua taratibutaratibu ili asijue kua ni mimi niliyemuua

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushindwe pepo wewe

      Delete
    2. Si bure unahitaji maombi maraika wa mungu kakukosea nn adi umuue si bora utoroke uache kazi, maana damu yake huyo mtoto itakuandama siku zote za maisha yako

      Delete
  9. Duuu binaadamu tumekua kama wanyama kwa ukatili.

    ReplyDelete
  10. Huyu mama rwechungura anaroho mbaya kupita maelezo namsubiri aingie katika angazangu basi atajuta kwa nini alihamia boko.

    ReplyDelete
  11. Hawa watu bora tuanze kuwachoma moto,maana serikali hii haitabiriki waweza kuwaachia hawa wauaji!

    ReplyDelete
  12. Anonymous 11.25 hata mimi namsubiri sana kwenye anga zangu.unakumbuka issue ya mbwa kuingia kwake?

    ReplyDelete
  13. Hapa Hakuna wa bara wala wa pwani wanawake roho mbaya mmezidisha jamani muogopeni mungu tena naweza kusema wanawake wa pwani nyie ndo mmezidi kujidai wamjini

    ReplyDelete
  14. Anonymous 11.12 inaonyesha wewe ni mzoefu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad