Ukiwa na Mpenzi Mwenye Haiba hii, Kujenga Uhusiano Imara ni Mashaka

Wataalamu wa tabia na mienendo ya binadamu wanasema, kuna Makundi kadhaa ya haiba. Wana maana kwamba, binadamu wamegawanyika katika Makundi kitabia.

Je, wewe uko kwenye kundi lipi?

Hiki ndicho ninachotaka kuwasaidia siku ya leo.

Lakini leo ningependa kuwazungumzia watu wenye haiba ya ukamilifu. Hawa ni wale watu ambao wanaamini kwamba, hawapaswi kukosea. Kwao, wanaamini kuwa, mtu anatakiwa afanye kwa usahihi na ukamilifu na kukosea kuna maaana ya udhaifu mkubwa na unyonge.

Nguvu kubwa ya watu hawa iko kwenye usahihi, ukamilifu na kurekebisha makosa. Iko kwenye kufanya ambavyo mtu angetakiwa kufanya, na kufanya mambo kwa usahihi.

Watu hawa wenye haiba ya usahihi huko ndani mwao kuna sauti (little voices) ambazo zina nguvu sana kwao, zenye kuwaamuru wafanye mambo bila kukosea. Lakini, sauti hizi zinakosoa na kuwadhibiti wahusika kwa njia yenye kuwaumiza. Huwa ni sauti zenye kuzalisha mashaka. Kushtakiwa na dhamira na hofu.

Kwa sababu ni watu wanaoamini katika “nzuri na sahihi,” inakuwa ni vigumu sana kwao kuishi na watu wengine kwa amani. Mbaya zaidi ni kwamba, wapenzi wao hupata shida sana kuendana nao. Hii ni kwa sababu, wanataka mambo yaende kwa njia yao, yawe sahihi. Kuna, “ingetakiwa iwe hivi,” nyingi sana.

Watu hawa huwafanya wengine wanaohusiana nao kuhisi kama vile wanatembea juu ya maganda ya mayai.

Kwa nini?

Ni kwa sababu hawa watu wenye haiba hii, hujiona wanaweza kuliko wengine na wanastahili kuliko wengine. Watu hawa wana tabia ya kusema au kumwambia mtu ukweli moja kwa moja kwa njia yenye kukera sana. Hali hii huwasononesha watu wanaoambiwa ukweli.

Watu ambao wameoa au kuolewa na wenye haiba hii, huwa wanatamani kuona mambo yakiwa tofauti kidogo. Wanajihisi kufungwa pumzi, kukaliwa kooni, kufungiwa kwenye dema na kushindwa kuona nafasi yao kama watu huru. Huhisi kuwa wao ni watoto, wanaokosea kila kitu, kwani ndivyo sauti za wapenzi wao zinavyowaambia kila wakati.

Inabidi mtu wa haiba hii ajifunze kukubali makosa, kwamba, kukosea siyo udhaifu, bali kujifunza. Ajue kwamba, kuna njia nyingi za kujifunza mambo, siyo njia moja tu ya “usahihi.” Kuna ya kukosea na kujifunza makosa, halafu ndiyo usahihi ufuate.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. watu wenye haiba hiyo hata akikosea hapendi kuambiwa, ukimuambia utapigiwa kelele mpaka utajuta kwa nini umeuliza,wengi wanaishia kulalamika mimi sipendwi sasa kwa tabia kama hizo atakupenda nani.

    ReplyDelete
  2. Nadhani mie ni mmoja wao. Nitajifunza kuwavumilia wengine kama wanavyonivumilia mimi. Lakini nyie tuache mzaha kuna watu wazito, yaani kila kitu kufanya kwa makosa tu.

    ReplyDelete
  3. duu ni kweli!!.. nina rafiki yangu wa hivyo yaan ananikeragaaa!!! anajifanyaga mjuajii!!! lkn mi namchukulia hivyohivyo.

    ReplyDelete
  4. Duu! Mm mpenzi wngu anatabia iyo xo ananichosha xna kitu c kitu kwake bonge ra neno. Ananionea xna naishia kulia nakuwa mnyonge kira wakati .

    ReplyDelete
  5. Wapo wengi mno wanakera mno

    ReplyDelete
  6. Ebwana hii topic imenigusa me ni mtanzania ila naishi nje ya nyumbani ebwana me mpenz wangu hayo uloandika hapo yoote yanamuhusu hapendi kukubali kosa ata siku moja na kila utakalolifanya wewe basi ni unakosea na umuombe samahani yeye. Wakati mwengine unahisi ni bora ata uwe single ili usonge na maisha yako mengine na uwe huru. Yaani ni adhabu kuliko mfungwa we acha tu

    ReplyDelete
  7. Mmmh hyo mada ina ukwel kabisa tena imenigusa, hadi mpenz wangu huwa ananiambia laiti angekuwa hanipendi 2ngekuwa tushaachana.Ila tunajifunza kupitia makosa asante wadau kwa kutukumbusha vitu kama hiv

    ReplyDelete
  8. Mmmh hyo mada ina ukwel kabisa tena imenigusa, hadi mpenz wangu huwa ananiambia laiti angekuwa hanipendi 2ngekuwa tushaachana.Ila tunajifunza kupitia makosa asante wadau kwa kutukumbusha vitu kama hiv

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad