Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
Faili la tuhuma dhidi ya
Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
“Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.
“Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
“Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana… ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.”
Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.
Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.
Hata hivyo, Mbasha alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”
“Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”
Mgogoro wa familia
Mbasha alidai kwamba chanzo cha kusingiziwa kwake ni mgogoro baina yake na mkewe Flora, ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa ambao umefanya achukiwe na familia nzima ya mkewe.
“Yako mambo mengi tu ambayo yanahusu familia, kwa hiyo ilifika mahali mimi na Flora tukawa hatuishi kwa amani na hata hili jambo limetokea wakati tukiwa na mgogoro huo. Hivyo Flora na ndugu zake waliamua kumlisha binti huyo maneno ili mimi nifungwe,” alisema Mbasha.
Hata hivyo, Flora hakutaka kuingia kwa undani katika suala hilo, akisisitiza kuwa Mbasha bado ni mumewe na kwamba yaliyotokea awali alishamsamehe, lakini akamtaka ajitokeze kutoa maelezo polisi.
“Mimi nilishamwambia kwamba hata kama alifanya au hakufanya, nilishamsamehe kutoka ndani ya moyo wangu maana yeye ni mume wangu wa ndoa na Mungu wangu ni shahidi, lakini kuna suala la kisheria polisi ambalo mimi siwezi kuliingilia,” alisema Flora ambaye alitamba na wimbo wa injili wa “Tanzania” ambao ulimfanya aalikwe katika shughuli mbalimba za kitaifa.
“Tatizo linakuwa kubwa kwa sababu yeye mwenyewe haonekani na taarifa ni kwamba amekimbia,” alidai Flora. “Sasa kama kweli hajafanya kitendo hicho, kwa nini anajificha? Ajitokeze… aende polisi na huko ndiko akatoe maelezo yake. Kuzungumza na vyombo vya habari haisaidii kabisa.”
Mwimbaji huyo, ambaye ni mjukuuu wa muhibiri maarufu wa Injili, Askofu Moses Kulola alisema yeye hana uwezo wa kuingilia kesi hiyo kwani hakuhusika kwa namna yoyote ile kupeleka suala hilo polisi kwa sababu hakuwapo wakati likitokea na kwamba linasimamiwa na familia.
“Inawezekana anatamani nikafute kesi polisi, mimi sina uwezo huo kwa sababu ni suala la kisheria na tuhuma zenyewe ni za kijinai. Pili familia yenye mtoto ndiyo inafuatilia kesi hiyo, lakini hilo halifuti msamaha wangu kwake,” alisisitiza.
Kauli ya Flora kwamba ameshamsamehe mumewe inafanana na ya Mbasha ambaye pia alisema kwamba kama kuna jambo ambalo mkewe alimkosea, hana tatizo na kwamba alishamsamehe.
“Flora ni mke wangu, mke wa ujana wangu, ninampenda asilimia 100 na yeye analifahamu hilo, lakini sijui ni kitu gani kimemkuta? Sijui ni nini kimeingilia ndoa yetu?” alisema Mbasha.
Alisema ameshampigia simu mkewe mara nne akitaka waonane ili wazungumze, lakini hakuonyesha utayari, kauli ambayo Flora aliikanusha akisema: “Hajanitafuta maana tangu Jumatatu hapatikani kwenye simu.”
Mwenendo wa upelelezi
Wakati hayo yakiendelea, maendeleon ya kesi hiyo yanasuasua baada ya faili kutokupelekwa Kituo cha Polisi Buguruni kutoka Tabata kwa ajili ya hatua zaidi.
Baadhi ya wanafamilia wa mtoto anayedaiwa kubakwa walisema jalada hilo lingefikishwa Buguruni Jumatano jioni, lakini kutokana na ofisa anayeshughulikia kesi hiyo kuwa na udhuru, ilishindikana.
Mjomba wa Flora ambaye amepewa jukumu la kusimamia kesi hiyo, alisema wamekuwa wakifuatilia Kituo cha Polisi cha Tabata tangu tukio hilo liliporipotiwa, lakini wakaelezwa kuwa kesi hiyo itahamishiwa Buguruni.
“Tuliambiwa lile faili lazima lihamie kituo cha Buguruni. Nilifika hapa nikaonana na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ametupokea vizuri na kuonyesha moyo wa kutusaidia,” alisema.
Kamanda wa polisi wa Ilala, Marietha Minangi alisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo na kwamba hafahamu taarifa kuwa faili hilo linacheleweshwa kuhamishiwa Buguruni. “Tunaendelea kuchunguza, ila siyajui hayo masuala ya faili yanayotoka kinywani mwako. Lakini nimepata taarifa kuwa bado wanachunguza,” alisema Minangi.
Mwanzoni mwa wiki jana, Kamanda Minangi alisema kuwa maofisa wake walikuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa na kwamba walienda mpaka nyumbani kwake, lakini hawakumkuta.
“Nimefuatilia ni kweli hiyo kesi imefunguliwa na maofisa wangu wameniambia walienda nyumbani kwake na hawakumkuta mtu. Waliniambia walikaa pale kwa takribani dakika 20 na ile nyumba ina fence (uzio) na geti waligonga kengele, lakini hakuna mtu aliyekuja kufungua.
“Na baadaye waliwauliza majirani, nao wakasema hawafahamu mtu huyo alipo. Inaonekana ametoweka, lakini sisi kama wasimamizi wa sheria tunaendelea kumtafuta mpaka tutakapomkamata,” alisema Minangi.
Ustawi wa Jamii
Kesi hiyo pia inafuatiliwa kwa karibu na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Manispaa ya Ilala kujua usalama na matibabu ya binti huyo. Ofisa ustawi wa jamii anayeshughulikia ulinzi na usalama kwa mtoto wa manispaa hiyo, Fransica Makoye alisema kuwa wanalishughulikia suala hilo kama mengine katika kutafuta haki na usalama wa mtoto na wala hawahusishi na umaarufu wa wahusika.
“Sisi tunafuatilia kama alipata tiba sahihi mara baada ya tukio la kubakwa na kufahamu mahali ambako anakaa kwa ajili ya usalama wa huyo mtoto. Tumeiona PF3 haionyeshi kama alipata matibabu, lakini tutawajulisha zaidi kinachojiri kwa kuwa tutaenda Hospitali ya Amana kwa maelezo zaidi,” alisema Makoye.
duu frola kama ni kweli hii kesi ni ya kutengeneza hakika litajakukukuta balaa kubwa sana wewe!!! hivi ni kweli hata kama mna mgogoro ndo mfanye jambo kubwa hivi wewe na ndugu zako hee unaimba nyimbo za bureee!!
ReplyDeleteTru stor
DeleteSi wote waliitalo bwana bwana watauona uzima Wa milele' Flora kwanza umekonda"pili Mwaka jana ulitoa mwenyewe kwa kinywa chako kuwa Ndoa yenu ina miaka 10 BILA KIKOHOZI" kumbuka wana Wa Mungu hawaongei hovyo hovyo! Ingetakiwa kutoa sadaka ya Kums hukuru Mungu sio kusema kwenye MEDIA Ebu Soma John 6:63 ,,, Unavuna ulichopanda!!!!
ReplyDeleteTusubirr ukweli utajulikana
ReplyDeleteMbona matatizo jamani kwa ndugu yetu.....ahmed
ReplyDeletekama ni uongo FLORA utakua unajitafutia balaan n inaonekana ni njama tu
ReplyDeleteKama wanakusingizia mwenyezi mungu atakulinda ndugu yetu....
ReplyDeleteKumpa mtu kesi kama hiyo ni sawa na uuaji shame on u flora mnamuaibisha sana bbu yenu kulola huko alipo shenz zenu
ReplyDeleteHuyu flora nafamilia yake wanaujua ukweli ulivyo hebu ngoja tuone mwishowake
ReplyDeleteDada yangu Frola, wewe ni kioo cha walio wengi kama kweli hili umelitengeneza na wewe ni muhubiri wa injili utakua umetenda dhambi kubwa sana ambayo hisameheki mbele za mwenyeenzi mungu. Frola jamii itakuchukuliaje mumeo akienda jela kwa kumuundia kosa.
ReplyDeleteHuku ya flora na mumewe yakijiri, hebu na tuone warembo wakenya wanaosemekana kuchukiwa na waTanzania
ReplyDeletewe nae na warembo wako idiot!!!wenzio tunamsikitikia mwenzetu unatuletea upumbavu hapa kwani tz hakuna warembo!!umenkera pumbavu sana wee!
ReplyDeleteHuyo jamaa kamtomba kweli kwa nini akimbie acheni kutetea ujinga.tunataka akanyie debe miaka (30) hili iwe fundisho kwa wengine wenye tamaa za kisenge.
ReplyDeleteKuna mazito sana juu ya hili Flora kama kweli unamsingizia il Iafungwe ili ww uendelee kutanua na huyo kigogo aliyekununulia Prado na kuishi hotelini kumbuka machozi ya mumeo hayamwagiki bure
ReplyDeleteYeeeesu Iruva! Kigogo?? Na Ana Ndoa YESU usinyamaze Kama Ni kweli hii taarifa! Hilo prado Liwake MOTO!!'
DeleteInasikitisha sana Flora kwa kitendo hicho, Kama umemsingizia mume wako kuwa amebaka wakati si kweli hakika kisasi cha Mungu kiko juu yako.
DeleteHivi mbasha unaapa hujawahi kucheat kweli?kweli?kweli?kweli?kweli?kweli?kweli?kweli?
ReplyDeletehaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,swala na kubaka kilichokufanya ujifiche nini?sijawahi kufanya dhambi,wewe?wewe?wewe?wewe?
mm napta 2 ila ukwel upo njian waja,yaitaj uvumilvu kwetu kwa xaxa,hakka km flora na familia yake wameltengeneza bac kaa mkjua flora n zaid ya satan dunian...
ReplyDeleteHILO NIPEPO LA KURITHI HUYO BINTI AMERITHI KUTOKA KWA MZAZI KWANI HATA MZAZI WAKE ALIMTENDA MWENZI WAKE
ReplyDeleteAJUE CHA KUJIBU KWA MUNGU LA SIVYO ATUBU KWANI ANAJUA KINACHOENDELEA
Mbasha ndio ana tengeneza story, kabaka kweli na ushaidi upo acheni sheria ichukue mkondo wake, mbona liko wazi na video kachukuliwa.kama alikua hajabaka kwanini alikimbia? Ushahidi upo na wala sio huyo shemeji yake tu Huku Tabata katembea na Ma binti Kibao kazoea huyo Mkewe mvumilivu sana.
ReplyDeleteMch gwajima ananukia sakata hili
ReplyDeleteWalikubaliana hao kubaka ni mara moja hiyo mara tatu walikubaliana na binti kamchezo alikapenda ndiyo maana waliamua kurudia mechi huyo bint ni malaya mbwa apigiwi anacheza.
ReplyDeleteKesi hii ni frola na mch wake gwajima wanamtoa kafara mbasha ili wao wabaki uraiani wajitanue kisawa sawa, kwasababu mgogoro wa ndoa ulianza pale tu frola aliposhawishiwa na gwajima ahamie kanisa lake hivi kwanini siku zote huo mgogoro haukuwepo leo uje utokee muda mfupi tu baada ya kuwa karibu na MCH. GWAJIMA JAMANI? frola kaenda kuishi hotelini pesa za hoteli et analipa gwajima hivi hamuoni hapo mambo yapo wazi tu? hata msichana anaedai kubakwa na mbasha kachukuliwa na Gwajima ili afundishwe namna ya kujieleza mahakamani na frola amemweleza yule msichana hata umbile la ndani la mume wake ili msichana huyo akifika mahakamani aweze kumwelezea mbasha jinsi alivyo uchi wa mbasha, frola huyo huyo akatoka akaenda kwa dr kuhonga pesa ili vipimo vionekane kuwa msichana ameingiliwa? Hivyo basi, kesi hii mbasha msitegemee kwamba atashinda hata kidogo kwani ni mkakati ambao Frola anaucheza akishirikiana na huyo hawara yake kuhakikisha mbasha hachomoki, ushauri kwa mbasha, mosi, hoja si mtoto kuonekana kaingiliwa, hoja hapa shahawa hizo ni za mbasha? mbasha anatakiwa ayakatae hayo majibu ya kupikwa na badala yake msichana huyo apimwe na jopo la madaktari huru ili kujua shahawa hizo ni za mbasha? kwasababu ukisema et msichana kaingiliwa ukaishia hapo na kumtia hatiani mbasha kuwa ni kweli kambaka je kama alitembea na boy friend wake huko?
ReplyDeleteKanisa la ufufuo et wamejitokeza kujibu shutuma za kuhusika kwa gwajima kutembea na frola, kwanza anaepaswa kuzungumza ni gwajima mwenyewe na siyo kutumia kivuli cha kanisa, kwani kanisa ndilo lilimtuma gwajima atembee na frola?ampeleke uk? aambatane nae kwenye ziara?amlipie frola hotelini? pia hata kanisa lenyewe limebaki likijichanganya tu, kwasababu halisemi wazi kuwa linatuhumiwa nini? na limejibu nini? msemaji wa kanisa anaishia kusema et kama kuna maswali yatumwe nao watayajibu!! hivi kwanini kanisa kama limeamua kumsemea gwajima lisingeanza kujibu tuhuma nyingi na maswali mengi ambayo yameulizwa huko jamii forum? wanaotuhumiwa kuzini ni wawili tu, na tena walienda katika mazingira ya kujificha,hapo waumini hawakuwepo, sasa kujibu tuhuma hizo hapo kanisa linahusikaje? Gwajima ajitokeze aseme kuwa hakuwa anamlipia frola kulala hotelini,hakumpeleka frola uk kusoma,hakumnunulia gari ili hali mumewe hakumnunulia hata pikipiki huku wote ni waimbaji,aliambatana na frola kwenye ziara na kumuacha mumewe frola huku wote wakiwa ni waimbaji na wote ni wanena kwa lugha? ajibu hayo maswali na siyo kuleta porojo hapa
ReplyDeleteSo sad
DeleteMMMMMH !TUTASIKIA MENGI,ALIJISEMEA MDAU MMOJA WACHA MOVIE IENDELEEE.
ReplyDeleteLakini mbona mwenyewe anajiuma uma kwenye ile audio asimuulize yule binti straight aseme ukweli kabaki kuzunguka tuu. Mliokuwa hamjasikia audio ingieni kwenye blog ya jipange101.com
ReplyDeletejambo isilo lijua. sawa na usk wa giza ukwel upo moyon mwa watuhumiwa
ReplyDeletejamaa kabaka ukweli ndio huo na asijifanye msafi ni malaya mbwa. file lake ninalo, tena msipayuke hovyo kumtetea, ana jifanyaga tyson kwa mkewe na anapigana hovyo mpaka na mashemeji zake. zarau zake ndio zimefika mwisho, audio yake kaongea kwa majitapo anajiuma uma ka mwehu.
ReplyDeleteTumuachie Mungu atahukumu isije ikawa hukumu kama ya babu seya sasa
ReplyDeleteMambo ya ndoa kamwe hayasuluhishwi kwa njia hiyo mliyoichagua sana sana mnajidhalilisha na kujichoresha tu. Kwani kuimba mziki wa injili au kuimba kwaya ndo umaarufu? sansana ni ulimbukeni tu.
ReplyDeleteTumechoshwa na ujinga ujinga wenu wa dada wa kisukuma, juzi alikuwa vicky kamata, leo Flora Mbasha. Jifunzeni hekima na busara, kabla ya hii mitandao mambo ya ndoa yalikuwa yanamalizwaje,mpka kila mtu ajue unamchepuko,tena wa mchungaji wenu huyo feki! Sasa kama wewe unamchepuko wa mchungaji, mmeo akiwa na mchepuko wa shemeji kipi cha ajabu. Yaani mavichwa yenu makubwa yamejaa ujinga tu, hata sioni mwenye afadhali,si mke,si mme,hao ndugu,shemeji mtu, mchungaji, wote pumbavu tu.
daaaa dada yangu frola kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu.
ReplyDeletekuna tatizo lipo hapo. Kwa nini Flora hawaonani na Mbasha uso kwa uso?. kila mmoja anajibu kivyake. kama mke amemsamehe mme basi waonyeshe watu kuwa wapo pamoja watoke hadharani na kutoa kauli moja kuwa wapo bega kwa bega wakumbuke kiapo mbele ya madhabahu. pia nashangaa huyo aliyechukua video ya kubaka alikuwa anajua kuwa kuna tukio hilo litakalotokea?
ReplyDeleteNdg. zangu wapendwa tumuogope Mungu. Naamini kuna kamchezo kachafu hapo. Mbasha ana haki ya kujificha kwanza ili ajipange maana anahofia hatima yake. Narudia ubakaji umerekodiwa siamini ninachokisoma.
unaona eeh! Inawezekana ametengenezewa zengwe huyo ili afunguliwe mashitaka kama akina babu seya
Deletekaah! Haya jamani, tunataka kuona haki inatendeka! Inavyooenekana huyo jamaa aliyemhonga prado mbaya sana si ndio huyo mchungaji maarufu! Haya jamani hakuna cha dini wala nini ni wizi mtupu
ReplyDelete