Video: Flora Mbasha Aelezea Kisa cha Mume wake Mbasha Kumtishia Kumuua, na Tuhuma za Kumbaka Shemeji Yake

Muimbaji wa Injili Flora Mbasha amefunguka kuhusu kisa cha mume wake, Emmanuel Mbasha kumtishia kumuua, pamoja na tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17, katika Exclusive Interview aliyofanyiwa na Global Publishers.

“Yani alikuwa mpaka ananitukana matusi ya nguoni kama mtu ambaye hajaokoka”, amesema Flora. “Nikahisi labda kuna kitu amabcho kimemuingia, nikamwambia Mbasha au umerogwa ndugu yangu we unaongea vitu gani hivyo, akawa analalamika tu basi we ndio umerogwa sio mimi.”

Flora ameendelea kusema,
“Na kabla sijatoka ndani alisema we lazima leo nikufundishe adabu alinishika tu akaniniga yani mpaka akaniachia maalama kwenye shingo yani hivi ninavyozungumza mpaka saizi bado shingo yangu inauma yale maumivu niliyoyapata hiyo siku. Nikamwambia Mbasha Mbasha Mbasha unaniuwa hata kuongea siwezi”.

“Huo usiku sikurudi nyumbani na asubuhi Jumatatu yule binti akapiga simu hakunipigia mimi alimpigia mdogo wangu mwingine akamwambia tu mimi naondoka ilikuwa mida kama saa 12 kasoro akasema mi naondoka mi shemeji ameninyanyasa amenidhalilisha kanifanyia kitendo kibaya sana, sasa akamuuliza amekufanyia nini akawa hawezi kuongea kwenye simu akamshauri tu kwamba usiondoke subiri dada yako atakapokuja kwanza anarudi muda si mrefu…kwasababu Yule binti tulikuwa tunakaa nae nyumbani sasa ni miaka kama mitatu au mine naishi nae pale nyumbani namtunza mimi ni mdogo wangu kwahiyo nilikuwa naishi nae hapo ndani kwahiyo alikuwa kama ni mtoto wa kwangu mimi tulikuwa tunamlea pamoja na mme wangu.” Amesema Florah Mbasha.

Tazama Video
Bongo5/GPL

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa nini ulivyoondoka usiondoke nae kama ulimwona mzee kabadilika usituzuge bwana we endelea na mambo yako, sasa mmeanza kua kama dai na wema

    ReplyDelete
    Replies
    1. Flora Ni muongooooooooo Eti kaokoka,sasa anatunga uongo mwingine baada ya kasi ya kubaka kugonga mwamba,nasikia kasema atahakikisha mumewe anaozea jela,wanawake wakipata wakuwawezesha wanakuwa na jeuriiiiii

      Delete
  2. Polee dada Flora inasikitisha sana mungu akupe nguvu uyashinde haya majaribu

    ReplyDelete
  3. Wapuuzi nyie mmekosa hekima ya Mungu na ulokole wenu mnatangza upuuzi wenu wa ndan kama majinga pumbavu.

    ReplyDelete
  4. yarabi! hata hawa watumishi! shetani kajitahidi kwa kweli!

    ReplyDelete
  5. Mr Mbasha ni Chui aliyejivika ngozi ya Kondoo hana ulokole wala si mtumishi wa Mungu, nyie hamu mjui vema uliza watu tunao kaa nao karibu, Mungu hachezewi kaamua kumu umbua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenda zako wewe Ni flora pumbaffff,unatembea na gwaj prado,Uingereza ukapelekwa mke Wa mtu,hizi ndoa za siku hizi.

      Delete
  6. Meokoka nn?mnatudanganya tu.watumishi wa mungu nao wana nyumba ndogo.Flora umegawa tunda nje na mwenzio kagawa, ngoma droo usikasirike,ila mkumbuke kwamba mungu hadhihakiwi.

    ReplyDelete
  7. Hivi flora huna wazazi ugomvi ukitokea kitu cha kwanza utaenda kuwaeleza wazazi ,ndugu wa karibu au dada yako hapo sijaelewa mimi????

    ReplyDelete
  8. Flora umejiabisha dada!kunyamaza kimya kingepunguka nini kwako?naamini mlikuwa na uwezo wa kujadili hilo suala kifamilia pasi kupekeleka police.Hadhi yako kwa jamii imeshuka masikini.Pole sana ila wengine tujifunze kupitia hili.

    ReplyDelete
  9. Huna Haya mlokole gani Wewe muongo hivyo humuogopi hata mungu Mambo yako unayapeleka kwenye udaku badala umkabidhi mungu we ndo umerogwa huyo gwaji mwenyewe umetembea nae,unampakazia tu mbasha makesi yako ya ajabu mungu akushushie adhabu hapa hapa DUNIANI mfyuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  10. mmetuchosha na wewe frola na huyo mmeo, watu hatufanyi mengine kukaa tunawasoma nyie tu, wewe mwenyewe frora umejiweka kimalayamalaya tu mawanja kama lishetani na huyo mbasha kajikirim na kujibabua ngozi kama lipopo mtu. Tupa kureeeeeee! Tumewachoka.

    ReplyDelete
  11. Mungu ndio anajua nini kimewakumba, na awasaidie kubeba hiyo aibu hiyo, yote alimaliza pale calivary

    ReplyDelete
  12. Flora hata mimi saa nyingine huwa napigwa mpk natamani nimuundie skendo km hiyo Mume wangu, lakini sijawahi kufikia hatua hiyo, we umezidisha

    ReplyDelete
  13. Yaani kwa maelezo yako tu unaonekana mnafiki we flora,unamsaliti mmeo sababu ya gwajima?duh kweli wanawake ni mashetani hata biblia imeandika!!Usoni tu unavyopepesa macho unatafuta maneno ya kuongea unaonekana unadanganya,umemsaliti mmeo kuwa mkweli nawe ni icon ya walokole walio wengi acha uongo basi!!Na kama issue ni kugombana na mmeo kwann ukamwambie gwajima na co ndugu zako ambao kwa mtazamo wangu nadhani ndo wapo karibu na ww kuliko hy gwajima?mhhh hii dili inaonekana kabisa ila mungu yupo na huwa analipa hapahapa duniani ngoja tusubiri tuone matokeo!!I will never trust a woman again hata kama ni mke wangu

    ReplyDelete
  14. Hahaha anony 1.02 upo sahihi kabisa huyu flora ana lake jambo kuna kitu kadanganywa na huyo gwajima!!!Mme wako hata kama kabaka huwezi ukamtoa kafara kirahisi namna hiii flora utubu ati

    ReplyDelete
  15. Anonymous 9.23 ww unaonekana ni mke bora kuliko hata hy flora mbasha anatupakia wanja ka bar maid afu anajifanya mlokole hakuna kitu hapo maana kuna watu wanamjua toka mdogo alikuwa kicheche blaa

    ReplyDelete
  16. 40 ndio imefika mbasha nenda kanyee debe miaka 30 kule utakutana na watalaamu wengine waliokubuhu mambo hayo na huduma hiyo utaikosa kutoka kwa flora na huyo binti 30 years hujatuambia wakati polisi wanakusaka ulikuwa wapi mkeo unasema alikuwa kwa gwajima wewe ulikuwa wapi ? Mnaomsakama flora unajua uchungu wa mmeo sio kutembea na mdogo wako ila kumbaka bila ridhaa yake ,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad