Wabunge acheni siasa na Misamaha ya Kodi, Haikwepeki ni lazima iwepo!

 Ninashangazwa sana na Baadhi ya Wabunge wanapochangia hoja zao toka majuzi kuhusu Bajeti ya Wizara ya Fedha, wakilalamika sana kuhusu Misamaha ya Kodi kwa wawekezaji bila ya kutoa Alternative, I mean wawekezaji wanasamehewa kodi Dunia nzima sio Tanzania tu. Kama Serikali haiwezi kuweka mikakati ya kodi ambayo ni rafiki kwa wawekezaji wala sio siri kwamba wawekezaji watakwenda nchi nyingine ambayo ina mazingira rafiki na biashara zao. Ningetegemea Mbunge mmoja asimame na kutoa solutions za namna ya kusamehe kodi na kuhakikisha Taifa linanufaika kwa sababu ndivyo inavyofanyika Dunia nzima na ndipo tatizo letu lilipo aidha hatujui nini cha kufanya ili misamaha ya kodi kwa wawekezaji itusaidie kama nchi zingine, au tunajua ila tunafanya makusudi kwa masilahi ya binafsi.

- Muwekezaji anatakiwa kubanwa mbavu kwamba kweli atasamehewa kodi, lakini analazimishwa kujenga Shule katika eneo lake la biashara au kuajiri vijana wengi kwenye biashara yake ndivyo Dunia nzima wanavyofanya. Na kwenye hili ni muhimu sana Manispaa kupewa madaraka zaidi ya waliyonayo sasa kwa sababu ndivyo inavyofanyika kwenye Mataifa yaliyoendelea, Manispaa wanakuwa na mamlaka ya Kodi ndani ya Manispaa, matokeo ni kwamba kama mazingira ya kodi Ilala hayapo sawa Muwekezaji anahamia Temeke maana kule anakuta mazingira rafiki ya kodi, na infact Manispaa zinakuwa kwenye competition ya wawezekaji.

- Ukienda Swaziland ni kwamba Muwekezaji anapewa msamaha wa kodi kwenye madini, lakini analazimishwa kutoa mchango katika kuendeleza mifugo yao, Marekani Muwekezaji anasamehewa kodi lakini analazimishwa kutoaa ajira kubwa kwa vijana. Tatizo tulilonalo sio misamaha ya kodi, isipokuwa ni mikataba ya misamaha ya kodi Bunge likae chini na kutengeneza Sheria itakayotoa madaraka zaidi kwa Manispaa ili ziweze kuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu misamaha ya kodi kwa wawekezaji ndani ya Manispaa zao.

- WABUNGE WETU WAACHE KULALALAMIKA KUHUSU MISAMAHA YA KODI, HAIKWEPEKI WATOE MUONGOZO NAMNA YA KUISIMAMIA MISAMAHA YA KODI!!

LE MUTUZ SYSTEM
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ww n mwehu kwl!! umejitahidi kuongea pumba 2!!!Ni gan dunian inayowalipisha wake maskini km hawa halaf unamwacha mchimbaj wa mkubwa wa madini anachota mali nying na hatimaye anaacha mazingira yale yakiwa shagala baghala.... c waondoke 2.. hayo kaongee na dada ako ...nyooooooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad