Waganga wa Kutibu Kwa Kutumia Ngono na Nguo za Ndani Wakamatwa Temeke

POLISI Mkoa wa Temeke, imewakamata vijana wawili wanaodaiwa kujifanya waganga wanaotoa tiba kwa wanawake, ambayo masharti yake ni kushiriki nao ngono bila kinga na kuacha nguo za ndani, ili zifanyiwe dawa zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alidai vijana hao Juma Hemedi (32) na Abrahman Mulsin, wote wakazi wa Tandika, baada ya kushiriki ngono na wagonjwa wao huwaambia waache nguo za ndani.

Kamanda Kiondo alidai baada ya kupata malalamiko, Jeshi la Polisi lianzisha msako na kuwapekua waganga hao, ambapo walikutwa na nguo za ndani za kike 22, ambazo alisema zitakuwa ushahidi wa kuingiliwa kimwili kwa wanawake hao. Vitu vingine wanavyodaiwa kukutwa navyo ni pembe, tunguli, makopo ya dawa na vibuyu.

“Sheria iko wazi, inasema mganga anapofanya ngono kama uganga anakuwa amebaka, na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu 130 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” alisema Kamanda Kiondo.

Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kiondo, vijana hao wamekuwa wakijifanya waganga wa tiba asili, husambaza vipeperushi sehemu mbalimbali za jiji kutafuta wateja.

Mbali na tiba hiyo ya kupata watoto, inayotolewa kwa kushiriki ngono na mganga, Kamanda Kiondo alidai watuhumiwa hao wamekuwa wakidai kutibu magonjwa mengine kama kisukari, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume, kukuza maumbile, kupata kazi, kufaulu mtihani, mvuto wa biashara, kumilikishwa jini na kupewa pete ya bahati.

 Katika tukio lingine, Polisi inamshikilia kijana mwingine mkazi wa Tandika Devis Corner, Maalim Kimti Rita au kwa jina lingine, Joseph Rita anayedaiwa kutapeli Sh milioni 11 akijidai kumfanyia dua mfanyabiashara aweze kukuza biashara yake.

Alidai kuna mfanyabiashara mwanamke ambaye alitoa Sh milioni 11 kwa Maalim Rita, akidanganywa kuwa atafanyiwa uganga ili afanikiwe katika biashara yake, lakini alipoona hakuna alichopata, akaamua kutoa taarifa Polisi.

Kamanda Kiondo alisema jamii inapaswa kuelimishwa kuachana na mambo hayo, kwa sababu tiba yake haipo kwa waganga wa jadi na kwamba hakuna uhusiano kati ya kufaulu na kwenda kwa waganga isipokuwa bidii ya kazi.

“Watu wengi wamelalamikia matukio ya namna hiyo, sasa tumeamua kuweka wazi kwa umma kwa kuwa watu wanateketea kwa kukosa elimu… watu wanauza nyumba magari na mali zao, kwa ajili ya kupata fedha za kupeleka kwa waganga wakiamini kuna tiba, huu ni utapeli vijana kama hawa hawawezi kukupa utajiri wala mtoto,” alisema Kamanda Kiondo.

Alisema waganga hao wamepata vyeti vya kufanyia kazi hiyo ya uganga wa jadi, lakini wanachofanya ni kinyume na kazi hiyo ambapo aliahidi vyeti vyao kuchunguzwa, kuona wamevipataje na kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii, ili watambue pembe wanazotumia ni za mnyama gani.

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wajinga ndio waliwao

    ReplyDelete
  2. Watu wanaotaka chochote waende kwa Mungu watapata hicho wanachotafuta la sivyo watajikuta wakiambukizwa ukimwa na magonjwa mengine ya ajabu. Uganga ni uongo mtupu.

    ReplyDelete
  3. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa..
    Tumepewa macho hatuoni,masikio hatusikii na akili hatutumii..
    Tuamke jamani

    ReplyDelete
  4. Makubwa kiazi unatoa milion 11 na moja biashara yako iende vizuri, kwa mfano ungesaidia watoto yatima, wajane, na wazee ungepata sana thawabu na biashara yako ingeenda bila kujua, ni lini watz tutaelimika, wazungu wanaendelea wanasaidia sana sana watoto yatima, wajane na vikongwe, mtasema mungu kawapendelea hapana ni utamaduni waliojiwekea na wanaendelea milele sisi tutakufa na umasiki kwa kuwamini wanganga badala ya mungu, ni shiriki kubwa ambayo mungu hawezi isamehe

    ReplyDelete
  5. JAMANI HUO NI UTAPELI NI WIZI WA KUAMINIWA CONMEN WAFIKISHWE KORTINI .

    ReplyDelete
  6. kekundu kekundu, x 2 wajinga ndiyo waliyao mama poyee

    ReplyDelete
  7. hao waliotapeli naomba waachiwe huru tu kwani ni wabunifu wazuri ila huyo aliyetapeliwa achukuliwe hatua kwa kosa la uzembe na kujisababishia hasara. Hivi kweli mfanyabiashara unatoa 11m unampa mganga wa kienyeji ili biashara ikue hiyo 11m kwanini usingeiongeza kwenye mtaji ili biashara ikue???

    Na hao wakinamama waliokuwa wanaingiliwa kimwili na waganga feki hivi kweli katika ulimwengu huu unakutana kimwili na mtu usiyemjua tena bila kinga hivi zinakuwa ni akili zao au ndo imani iliyopitiliza???

    ReplyDelete
  8. Ujinga wao tu. kwa nini uendekeze imani za uganga badala ya kumlilia Mungu aliyewaumba.

    ReplyDelete
  9. Anonymous 2.01.
    hiyo picha tu inaonyesha huyo mama hakuingiliwa kwa ridhaa yake,wanaleweshwa,hawa watu ogopa sana sio wa kuwa nao karibu.mganga,mtabiri huwa wanaoa kwa nguvu za giza,ni wa kuogopwa.

    ReplyDelete
  10. wakamatwe kabisa coz wanasababisha michepuko!

    ReplyDelete
  11. HIVI KUNA NCHI INAYOONGOZA KWA MAZUZU KULIKO TANZANIA AIBU KUBWA

    ReplyDelete
  12. kuna mwengine anakula kabang kabisa..subiri nimtaje hapa ndo akome!

    ReplyDelete
  13. Moja ya sharti baada ya kupewa dawa ilikuwa ni kuacha pichu, sasa jamaa wamekutwa na pichu 22, inamaana hao wote walikuwa wakigugumia kutapeliwa kimya kimya wala hawakuwa na ujasiri wa kupiga kelele hadharani kwamba wametapeliwa

    ReplyDelete
  14. ha ha ha haa jamaa atakuwa alikuwa na ham

    ReplyDelete
  15. wanawake amkeni

    ReplyDelete
  16. mtu na akili zako una dangaywa upewe dawa unakubali kama ndio hivyo si umweambie bwana wako akupe hiyo dawa ?

    ReplyDelete
  17. jinsi ya kutengeneza pesa kupitia computer yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad