TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA.
A. UTANGULIZI
Ndugu wanahabari.
Mbele yenu ni viongozi halali wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutoka mikoa yote ya Tanzania kwa uchache tumekutana jumla ya wajumbe 78 kuwakilisha wenzetu walioshindwa kufika kwa sababu mbali
Sisi ni wajumbe wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa Chama ambapo pamoja nasi tumejumuika na wenyeviti wa mabaraza ya WANAWAKE WA MIKOA YA TABORA NA SINGIDA, MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA TABORA pamoja na MUASISI WA CHADEMA kutokea mkoa wa SINGIDA na mwenyekiti wa M4C wilaya ya SINGIDA hivyo tunafanya jumla ya tuliokutana kwa jambo hili kuwa ni wanachadema 82.
Tumewaita kuwaeleza namna ambavyo tumekuwa tukisononeshwa na mwenendo wa chama chetu kwa kipindi kirefu sasa, hivyo tunaomba mtusaidie kuufikishia umma mawazo ya wanachadema tunaowawakilisha huko mikoani tutokapo.
B. KUSHINDWA KWA UONGOZI WA KITAIFA.
Tunasikitika kuona kwamba kadri siku zinavyoenda Uongozi wa juu wa chama unazidi kushindwa kufanya kazi ya kukiimarisha chama.
Baada ya jitihada tulizozifanya kwenye uchaguzi wa 2010 sehemu mbali mbali, ni dhahiri ushindani kwa sasa ungekuwa mkubwa sana kiasi cha chama kushika dola uchaguzi ujao iwapo chama kingejikita kwenye jitihada za ujenzi wa chama.
Badala yake uongozi wetu umewasaliti Watanzania waliokuwa na tumaini kubwa sana na chadema na kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye Kuimarisha migogoro baina ya viongozi wakuu wenyewe kwa wenyewe, wanaimarisha ubinafsi miongoni mwa wanachama, wanaimarisha Udini na Ukabila pamoja na ubadhilifu wa mali za chama.
Matendo haya ya viongozi wetu ni UNAFIKI wa kisiasa, kiasi cha kutumia mabilioni ya shilingi kwenda kumshambulia ama kummaliza kisiasa kiongozi mwenzao (Zitto Kabwe) na kuacha ujenzi wa chama ukiendelea kuporomoka.
Kwenye ujinga huu, hakuna wa kumlaumu zaidi ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe na na Katibu Mkuu Dkt.Wilbrod Slaa. Hawa wanafaa sasa kuhukumiwa na watanzania wanaopenda mabadiliko ya kweli kwa kurudisha nyuma jitihada za kuwakomboa na kukiimarisha chama na badala yake wamekuwa wakitumia nguvu kubwa na rasilimali nyingi za chama kujiimarisha wao wenyewe.
C. UBADHILIFU WA FEDHA NA MALI ZA CHAMA.
Ndugu WanaHabari.
Mtakumbuka kwamba baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2010 ruzuku ya chama iliongezeka kutoka million 56 mpaka milioni 239 kwa mwezi.
Tunasikitika kuona kwamba mpaka sasa chama kimeshindwa kufanya uwekezaji wenye tija ili kukisaidia chama kiweze kujiendesha bila kutegemea Ruzuku ama kukopa kutoka kwa Mbowe kama mwenyewe anavyopenda tuwe tunafanya.
Mpaka sasa chama kimepokea jumla ya shilingi BILIONI 10.038 kama ruzuku kutoka serikalini ili chama kijiendeshe. Ni narudia, mpaka sasa chama kimepokea kutoka serikalini jumla ya SHILINGI BILLION KUMI, NA MILIONI THELASINI NA NANE.
Cha kusikitisha kwa kipindi chote hicho na kiasi chote hicho cha pesa zitokanazo na kodi za waTatanzania pesa ambazo zinasababishwa na kazi kubwa tuliyoifanya ya kukipigania chama kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, leo chama hakina hata jengo moja la OFISI MIKOANI KOTE na OFISI zote za mikoa tunapanga kwenye FREMU za maduka na hata Pango la fremu hizo tunajilipia wenyewe kwa kuchangishana, Mbowe na Slaa wanatumia MABILIONI HAYA KURUKA NA CHOPA sisi huku chini tunaendelea kumenyeka kwa kigezo cha UKAMANDA ,huu ni utumiaji mbaya wa mali za chama.
Tunasikitishwa sana na kitendo cham mwenyekiti MBOWE kusema anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila siku, kiasi cha zaidi ya MILLIONI 700 Mbowe anajilipa kama madeni aliyokikopesha chama. Sasa tunashindwa kuelewa deni hili ni deni gani lisiloisha?, na je deni hili alikikopesha chama kwa mkataba gani?, na aliusaini mbele ya nani huo mkataba wa mkopo?, Taratibu za chama kukopa zipo wazi je zilifuatwa?. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Tunasikitishwa na kitendo cha mwenyekiti mbowe kukiuzia chama MAGARI CHAKAVU kwa zaidi ya million 600, Huku akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia chama alikuwa anakikodisha magari hayo
Masikitiko yetu ni kitendo cha MBOWE kununua LANDCRUISER V8 VX 2 kwa pesa za chama na kasha kuja kukiuzia chama, lakini kama haitoshi mpaka leo hii Gari hizo zimesajiriwa kwa majina ya MBOWE HOTELS. Haya ni matumizi mabovu mno ya mali za umma na kwamba yampasa sasa ajitathmini kama anapaswa kuendelea kuwa kiongozi mtetezi wa wanyonge ama mnyonyaji wa wanyonge.
Tunahudhunishwa na kitendo cha Dkt. SLAA kutufanyia huduma ya kutuuzia ukombozi, haiwezekani kwa akili ya kawaida, ukawa katibu mkuu unayelipwa zaidi ya million 130 kwa mwaka na chama halafu makatibu na viongozi wako wa mikoani wanalipwa 0 kwa mwaka. Huu ni udalali na unafiki wa kisiasa.
D. UVUNJIFU WA KATIBA NA KANUNI ZA CHAMA.
Mpaka sasa viongozi wakuu hawa, wamevunja katiba ya chama kwa mambo makuu matatu yafuatayo.
1. Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge la katiba bila kuruhusiwa na vikao halali vya chama.
Bunge la katiba lilikuwa ni mazao ya Juhudi zetu sisi wanaCHADEMA tuliopambana nchi nzima kuidai katiba.
Chama chetu kilikuwa na fursa kubwa ya kutuwakilisha kwenye kuandika katiba hiyo na kufanya marekebisho makubwa kwa kadri tulivyoazimia.
Lakini kususa Bunge la katiba lililotokana na Sheria mliyoishiriki kuitunga, ni kutufanya sisi sote tunaowakilishwa na viongozi hawa tuonekane ni majuha.
Kwa kuwa CHADEMA ni miongoni mwa waasisi wa mchakato huu wa Katiba. Ni kuwasaliti Watanzania na kuikosesha nchi fursa ya kuandika katiba kususa.
2. Kitendo cha Kuunda Baraza Kivuli la mseto na vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushirika na CCM.
Kwenye hili, chama kinapaswa kuelezwa kama mazingira yaliyowafanya wenzetu hawa kuungana na CCM yamebadilika ama bado yapo?, Chama kinapaswa kuelezwa na mbowe na Slaa kuwa Uteuzi wa Mbatia kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa CCM umebatilishwa ama la?.
Lakini chama pia kitueleze kama Nafasi ya juu ya viongozi wa CUF kwenye serikali ya mseto na CCM kule Zanzibar haipo tena. Vinginevyo viongozi wetu wote walioshiriki hili wanatakiwa wawajibike haraka iwezekanavyo.
3. Kutokuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu. Katiba yetu inatuagiza Kuwa Baraza kuu la chama litaitishwa kila baada ya miezi kumi na mbili. Kwa kuwa baraza kuu la mwisho liliitishwa February 2013, kulipaswa kuitishwa tena baraza kuu lingine kabla ya mwezi February 2014 kuisha.
E. AGIZO
· Tunawaagiza viongozi wetu waitishe haraka MKUTANO WA BARAZA KUU ili pamoja na mambo mengine viongozi wetu wajieleze mbele ya Wajumbe ni kwanini Tusiwachukulie hatua za kinidhamu kwa makosa ya UBADHILIFU, KUSALITI NDOTO ZA WATANZANIA, na KUHAMASISHA MGAWANYIKO NA UBAGUZI NDANI YA CHAMA.
· MBOWE na Dkt. SLAA wanatakiwa wajipime wenyewe kama ni sahihi chama kukodi HELKOPTA (CHOPA) 3 na kutumia zaidi ya BILIONI 1.4 za ruzuku ambazo ni kodi za Watanzania halafu eti tunashinda KATA TATU kati ya zaidi ya KATA 27, Yaani kila HELKOPTA MOJA imeleta KATA MOJA ama kila SHILINGI MILLIONI 466.6 kwa KATA MOJA, halafu chama hakionyeshi kushtuka wala Kujali
· MBOWE na Dkt. SLAA wajipime zaidi kama wanafaa kuendelea kuwa viongozi wa chama huku chama kikizidi kudidimia kila uchao kiasi cha KUDHARIRISHWA KWA kupata KURA 2000 CHALINZE na KURA 5000 KALENGA huku chama kikitumia zaidi ya MILLIONI 600 kushiriki CHAGUZI HIZO.
…………………………..
0756767672
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TABORA
MJUMBE BARAZA LA MASHAURIANO KANDA YA MAGHARIBI
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA.
mcaga wa hai anapiga hela huyo ni mfanyabiashara huyo walasii kiongoz mi nasema ila sio sheria CHADEMA mwaka ujao mtadondokea pua mtashia kama NCCR mageuz yan mmetusaliti wananchi na kwa taarifa tenu amtafikisha ata viti ishirin bunge lijalo mmepoteza mvuto kwa wananchi na tayar amna mtu Ambae ataweza msimamisha kugombe uraisi na magwiji wa CCM ata mkijipanga tayar imechelewa Mtani wangu kavuruga chama
ReplyDeleteKazi imeanza,Chezea CCM wewe!!!
ReplyDeleteSafi kama mmeyaona hayo zitto aligusa mahesabu ya vyama akaundiwa zengwe viongozi wetu hawa wanafiki sana.
ReplyDeleteChadema mmechemsha vitivinaenda kwa vyamavingine hatakama ccm lakini nyie sijui mjipangeje mpite sahiz mmechelewa
DeleteEbwana tunawakaribisha ccm......milango iko wazi.....zimwi likujualo halikuli likakwishaa....ccm oyyyeeee
ReplyDeleteKama mchezo wa kuigiza vileeeeee,,
ReplyDeleteNa ww mwenyewe tabora umefanya nn taarifa unaandikiwa na zitto ujifanye unajua, kwenda zako huko!
ReplyDeleteYaani kuna mijitu inatia hasira sana kama hii mijitu iliyotumwa na ccm!sasa muda woote yalikuwa wapi eti leo hii yameona karibia na uchaguzi ndio mapumbu mbele mbele eti viongozi hawafai!nyinyi mngekuwa kweli mnadhamila nzuri na chadema mngesubiri mpaka chaguzi zipite then ndio mngeongelea mambo yenu sasa tutajuaje labda mmepewa hela na mafisadi ili kuja kukidhoofisha chama?na nyinyi kweli hamuoni hapo mnatugawa sisi wanachama!tuwaeleweje maana chaguzi ndio hizo zinakuja sasa baada ya kunadi sera za chama watu waanze kusuruhisha migogoro hamuoni kwanza mnawafaidisha mafisadi kwa hatuwa yenu hiyo?kwa kifupi kama habari hii ni ya kweli basi nyinyi asilimia 90 mmetumwa na mafisadi kuma nyoko zenu nyinyi!kwataarifa yenu hamtuyumbishi na bado tunaimani na viongozi wetu!mshindwe na mkafirwe mbele!
ReplyDeleteImetumwa na CCM kivipi??? Wewe anonymous hapo juu ungejaribu kuchukua muda nakuichanganua hiyo taarifa ili kuona kama inaukweli ndani yake na kama inakidhi matakwa ya watoa taarifa. Na sio kukurupuka bila mpango. Kitu kingine unacholaumu kuhusu ucheleweshaji wa kutoa hiyo taarifa, kwani umesahau ukiritimba wa viongozi wa juu wa chama????...Nadhani ungejitahidi kuwasiliana na Mbowe na Slaa kwa maelezo zaidi.
ReplyDeletehebu achen chuki binafsi na muongee ya kweli, watumwe na ccm ili iweje, kwani kilichongelewa hapo ni uongo, au hamumjui mboye nyie, msikieni hivyo hivyo, lkn ni ukweli usiopingika ndivyo anavyofanya kujitia anajilipa madeni na hela tumboni kwake, eti kiongozi anayeaminika mwe hivi bado tu mnamatongotongo na mmefumba macho, fungueni hata kama hamtapigia ccm sawa ila chadema imeoza hakuna kiongozi mwadilifu na elimu pia o
ReplyDeleteKwahiyo ndio mmeshakubali kutawaliwa na mafisadi maisha yenu yote sio?kweli eatanzania sio watu wakuonewa huruma kabisa kwa miaka 52 mpaka leo hali ni ngumu kila siku mnasikia ufisadi wa mabilioni ya shilingi viongozi ndio wanaofaidika sio mwananchi wa hali ya chini,lakini bado tu mmengangania kuwasaport hao mafisadi kweli akili za watanzania ziko kwenye maajabu kumi ya dunia,na viongozi wa ccm wameshawajua akili yenu ya kufikiri ni ndogo sana ndio maana kila chaguzi wanakuja na danganya toto nyingi then wanawapa tshirt na pilau basi mnawapa kula duh ndio maana nchi kama kenya wanatudharau sana,hebu fikiria mali asiri zipo za kumwaga lakini mpaka leo tunaomba omba na madeni kibao sasa hapo hamuwezi kujiuliza hiki chama tawala hakiwezi kuongoza nchi?tafakari mtanzania nchi inawenyewe hii na wenyewe ni mafisadi!
DeleteNdio uanze wewe kuwa mzalendo hapo ulipo hapo ofisin kwako umeiba mshahara laki 5 nyumba ya mil 150 hujiulizi hayo ni zaidi ya maajabu 7 kazini miaka 5tu hujakopa..bora chizi unaemjua kuliko usiemjua...
Deletemambo mengine yamalizen ndan ya chama chenu kwa7bu mnazid kuharibu chama hcho....
ReplyDeleteMTI KUPUKUTISHA MAJANI HAIMANISH MAJAN NDO YAMEKUFA ILA YANAPISHA NA MENGNE YACHIPUE@ pipoz
ReplyDeleteIli chadema wanishawishi kuwa viongozi wao wa juu ni waadilifu watoe sababu za kumfukuza zito uanachama tuu.....pia elimu inasaidia sana jamani....
ReplyDeleteTuliwapenda ila mmeharibu wenyewe kwa ubabe wenu ngazi za juu chuki unafiki uongo ubaguzi choyo na kuwatimua wasomi wenye maono ya mbali na uwezo wakuhoji why this msibani big noo but hao hao kwa wakwenu kula ubwabwa mliibuka na sut hizoo ndio tuwape nchi kweli kidogo mlichonacho mnakifisadi balaaa mkipewa nchi tutalia poo jipangeni upya pokeen maoni ya wasomi mtafika mbali ila ubabe hausaidii na kujilimbilikizia mali eti mnajilipa nyie si wazalendo jioleeni kwa chama na nchi yenu tz mchaga na hela mmmh kazi ipo
ReplyDeleteacha ujinga miaka 52 hali ni ngumu ni sawa na kupanga foleni kwa kuchukua sukari, au bado leo ukitaka kuwasiliana na bibi kijijini mpaka uende sio sasa ukimtaka kuongea na mtu uk na unaongea, acheni ujinga kwanza ulikuepo wakati nchi ndo imepata uhuru ulikuwa hata hujazaliwa so hujui hizo shida zilizokuwepo sasa, ukitaka kwenda moro kutoka dar siku mibili shwain wewe anoy hapo juu unakurupuka tu, hatuwezi kuwapa nchi watu wasioweza hata tu kuishi vizuri na familia zao ukiwapa nchi itakuaje, ni ukweli usiopingika chadema zee zizi la ng'ombe
ReplyDeleteNdio endeleeni kuwapa hao mafisadi waendelee kuwaibia vizuri sasa na sio mnakuja kulalama hali ngumu ya maisha hapa!yaani we ndio shwaini kabisa unatoa mifano ya kiseenge eti kutoka hapa na moro unafika siku hiyo hiyo hivi wewe huo nao ni mfano kweli?umeshatembelea mahospitalini ukaona watu wanavyoteseka wewe?inawezekana naongea na mtu kula kulala hata bei ya sukari hujui maaana unaongea na kutolea mifano kirahi rahisi tuu!mijitu mingine mifala kweli nenda kamuulize anaye kuweka mjini akwambie ugumu wa maisha na vitu vilivyo panda bei msenge maziwa wewe!
DeleteMi huwa sipendi watu wanaolalama kila siku na kusifia kenya kma vipi kaombeni uraia wa hizo nchi mnazozipenda na kuzisifia tuachieni tz yetu miaka 52 bado hujaona mabadiliko yoyote hata wachukue chadema hutaona pia coz huna macho na hutaki kuona...Africa bana mi namkumbuka gadafi hadi leo hafai hafai sasa wanamtamani arud ukifika wakati hao wachaga tutawapa tu nchi muone utamu wa ngoma serikali inawapa mabilion hawazitaji wanagawana haya kujenga ofis kunawashinda mi napenda upinzani ila si wakishamba tunawajua wote na tunajua tutachagua nani kma wazee wa kususa hata nchi wataisusa sawa kma mafisadi papa sawa
ReplyDeleteUshauri wako tuendelee kuwapa hawa mafisadi au?
DeleteNoo ila wanafanana tofauti huyu yupo jikoni kwa sasa anakula zaidi napenda wa tz tubadilike tuwe wazalendo maneno yetu yaendane na vitendo mungu tupe viongozi wazalendo wanao faaaa sio hawa hawana jipya
DeleteMe napita tu na tanzania yetu
ReplyDeleteunasema serikali inanunua magari ya gharama wakati na chama chako kinanunua ma v8 sasa tofauti na ccm iko wapi?tuna taka chama cha upinzania chenye vionjo tofauti na ccm
ReplyDeleteCHADEMA SAFI, HALALI NA SAHIHI NIILE YA BOB MAKANI NA DR.AMAN KABUROU, WALIONGOZA CHAMA KWA MATAKWA YA WANACHAMA, WALIOPO SASA NI WATAFUTAJI NA WALAJI NDIO MAANA HAWAMTAKI ZITTI TUNDA LA KABUROU NA MAKANI.
ReplyDeleteMPAKA HAPO TUTAKAPOCHAPANA NDIPO TUTAHESHIMIANA NA KUHESHMU RASILIMALI ZETU.
ReplyDeleteUmenena mdau... nakupa kadi ya auanachama Al Shabaab...
DeleteKula 5
USA4lfe
Mi naona kinuke tu nshachoka sasa mxxxxxzzxxxssss nna hasira. Hv kuna tawi la alshabab tanzania ...
ReplyDelete..
comments?
ReplyDeleteNa Nyie bwana mnatoka povu bure!!' Kwani mmesahau hao viongozi Wanapenda dogodogo, mfano ulio hai huo mwenyekiti Ana wanawake Kila mkoa!!! Ataacha
ReplyDeleteDuuuuuu!!! Mil 700 jamani!!' ccm nafuuu!!!' Uwiiiiiiiiii!!!!
ReplyDeletemashoga ya ccm haya hamtafika mbali, yashamkuta Mbowe sana haya, Mbowe mafia bwana!
ReplyDeleteCHEZEA CCM WEE HIZO NI MBINU ZA CCM PENDA USIPENDE JAMANI UCHAGUZI UMEFIKA NI LAZINA CCM IZOOFISHE VYAMA VINGINE NA HAO WALIOANDIKA HIYO HABARI MJUE WALIINGIA CHADEMA KUFANYA KAZI YAO SASA WAMEMALIZA LAZIMA WATOE RIPORT NA RIPORT NDIO HIYO NASSI WANANCHI KWA KUWA AKILI ZETU NI ZA KUPEWA NDIO HIVYO TUMEPOKEA KWAHIYO TAYARI TUMEONA NIKWELI CHADEMA NIWABAYA TENA TUNAIFAGILIA CCM WAKATI NIMAFISADI JAMANI KUWENI WAANGALIFU KAMA TUNATAKA MBADILIKO ILI WANANCHI TUPATE AHUENI
ReplyDeleteafrika amna sias aukiongea sana unaonekan muhaini ivyo vyama vina wenyewe alikuepo KAFULILA akaondolewa kimizengwe na wanamtak ZITTO bt bora unafki wa CCM kuliko huu wa CHADEMA chama kinamwenyewe na anatmko.Naisi kam tunaish nchi ya KIFALME
ReplyDeleteWa Tz ni kichwa cha mwenda wazimu, kumshangilia Lowassa kwa kukuibia au kumtukana Slaa kwa kumwita Lowassa fisadi. Kupata mawazo ya kuindeleza Nchi yet, si kizazi hiki kinacho penda wezi na unafiki. Tz inahitaji kuzazi kipya na chenye fikira pevu hasa, acha kizazi hiuki kilicho chaa UDAKU
ReplyDelete