Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam imesema majambazi waliohusika na mauaji ya Sista wa Kanisa Katoliki, Clencensia Kapuli wamepora kiasi cha Sh20 milioni na nyaraka mbalimbali.
Tukio la kupigwa risasi sista huyo lilitokea juzi saa 8 mchana eneo la Riverside Ubungo, Dar es Salaam na dereva , Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.
Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence Makoka jijini hapa alikuwa Mhasibu wa Parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.
Kamanda wa Kanda hiyo alisema Kamishna Suleiman Kova alisema jeshi hilo limetangaza msako wa kuwatafuta na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.
Kova alisema marehemu akiwa ameongozana na wenzake ambaye ni Sista Brigita Mbaga na dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha.
Alisema walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la Thomas Francis ndipo walitokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki ambayo haikusomeka namba.
Alisema kati ya majambazi hao mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gari hilo kisha sista huyo alipigwa risasi ya kifua na kuporwa fedha hizo Sh20 milioni.
Kova alisema jeshi hilo limebaini kuwa matukio ya ujambazi hasa unaohusiana na wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha fedha unaanzia benki na huwafuatilia wanapoingia na kutoka.
“Ni muhimu kwa benki kuwahimiza wateja wao kutochukua kiasi kikubwa cha pesa kiholela kwani ni rahisi kuporwa na watu wasio na nia njema,” alisema Kova.
Alisema benki ziwahimize wateja wao kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi kama vile kwa hundi, kufanya miamala bila kadi na matumizi ya kadi za ATM.
Kova alizishauri benki nchini zianzishe vitengo vya ushauri kwa wateja ili wanapokuwa na fedha nyingi wasindikizwe na polisi.
Sasa mtu ataenda kutoa milioni 20 kwenye muamala. Je ikatokea umeweka milion 20 kwenye simu alaf simu yenyewe ukaporwa utakua umeepusha nini
ReplyDeleteAcha umbulula wakipora cm namba za siri si unazo wewe jiongeze bas.. Kova yupo right...
ReplyDeleteLoooh mdau 2:45 kula tano, umesahau kumwelimisha kwamba pesa hazikai kwenye simu
ReplyDeleteHa aha aha aha. Jamaa wa kwanza ametoa kali.
ReplyDeletePolice wanawajua sana hawa waharifu, unadhan angeuawa police mwenzao au Inspekta wa police wasingewashika hao watu? Hapo ndio tunaanza kuona uzuri na ubaya wa bodaboda, ni rahisi kutuwaisha tunakoenda na ni rahisi kumkimbiza kaka jambazi, R.I.P Sister
ReplyDeletePole sana ushauri wa kova upo ok! wewe kama unakwenda kudroo pesa nyingi we nenda na mdai mlipe humo2. bank kama ataondoka nazo juu yake kama ataingiza benk nae yote sawa.
ReplyDeleteWabunge waotetea bodaboda kwenda mjini wapate somo , mji umetulia
ReplyDeletehuyo wa kwanza kweli mbulula.........
ReplyDeleteHuyo wa kwanza kachemka balaa
ReplyDelete