Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa muda mrefu bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi 10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda Kiondo.
Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
GPL
sawa.
ReplyDeleteacheni kutunga maneno wake wa vigogo hawaendi kwa waganga njaa kama hao
ReplyDeleteTANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ANDIKWIBWA DRIVING SCHOOL
ReplyDeleteShule ya Udereva Andikwibwa Iliyoko Mwananyamala B inatangaza nafasi za kazi ya ualimu kwa walimu wenyenye cheti, uwezo na uzoefu wa kufundisha udereva.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na uwezo wa kuendesha na kulimudu gari.
Awe uwezo wa kufundisha na kuelekeza wanafunzi jinsi ya kuendesha gari.
Awe na cheti cha ualimu wa udereva kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali
MSHAHARA
Mshahara mnono kutolewa kwa kuzingatia viwango vya serikali.
MAWASILIANO
ANYOSISYE RICHARD MWAKIKUTI (Chief Instructor)
SIMU: O784300824, 0715300824, 0767300824
BARUA: Kwamanjunju,
Mwananyamala B
P.O BOX 61613
Dar es salaam
kisa umesijika ajira kwa vijana ni janga, basi ungetanza kiheshima labda watu wangeshtuka, sasa hapo ume comment au umetangaza? Tumia akili kuwavuta watu, wewe na hao waganga hamna mwenye tofauti, kasoro wao wameongeza na ku-do ila wote matapeli tu.
Deletesasa kuliko kuComment matusi si bora kupost hiyo vijana wapate kazi? Haikuhusu unakaa kimya au unaendelea kupost matusi kama ulivyozoea.
ReplyDeleteAcheni kudhalilisha wanawake mbona humusemi mkewako mbwa wee
ReplyDeleteAseme mke wake achekwe
ReplyDeleteKwa mtu mshirikina kama mwigulu mke wake amepona kweli?
ReplyDeleteIt might be true
ReplyDelete