Waliofanyishwa Ngono na Mganga wa Kienyeji Wengi ni Wake wa Vigogo

Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito  baada ya kukaa  muda  mrefu  bila watoto,  wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake  hao umebaini kuwa,  waume wao wanafanya kazi  katika nyadhifa za  juu serikalini, wengine ni wastaafu  na kwamba waume hao  hawajui kinachoendelea.

Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.

Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.

‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani  ‘kufuli’ za  wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa  na polisi  kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.

KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa  baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.

Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao  yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema  ni  kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi  10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.

Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.

KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.

Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya  waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo  hivyo  vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi  mbalimbali ikiwemo  Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema  Kamanda Kiondo.

Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
GPL

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acheni kutunga maneno wake wa vigogo hawaendi kwa waganga njaa kama hao

    ReplyDelete
  2. TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ANDIKWIBWA DRIVING SCHOOL
    Shule ya Udereva Andikwibwa Iliyoko Mwananyamala B inatangaza nafasi za kazi ya ualimu kwa walimu wenyenye cheti, uwezo na uzoefu wa kufundisha udereva.
    SIFA ZA MWOMBAJI
    Awe na uwezo wa kuendesha na kulimudu gari.
    Awe uwezo wa kufundisha na kuelekeza wanafunzi jinsi ya kuendesha gari.
    Awe na cheti cha ualimu wa udereva kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali
    MSHAHARA
    Mshahara mnono kutolewa kwa kuzingatia viwango vya serikali.
    MAWASILIANO
    ANYOSISYE RICHARD MWAKIKUTI (Chief Instructor)
    SIMU: O784300824, 0715300824, 0767300824
    BARUA: Kwamanjunju,
    Mwananyamala B
    P.O BOX 61613
    Dar es salaam


    ReplyDelete
    Replies
    1. kisa umesijika ajira kwa vijana ni janga, basi ungetanza kiheshima labda watu wangeshtuka, sasa hapo ume comment au umetangaza? Tumia akili kuwavuta watu, wewe na hao waganga hamna mwenye tofauti, kasoro wao wameongeza na ku-do ila wote matapeli tu.

      Delete
  3. sasa kuliko kuComment matusi si bora kupost hiyo vijana wapate kazi? Haikuhusu unakaa kimya au unaendelea kupost matusi kama ulivyozoea.

    ReplyDelete
  4. Acheni kudhalilisha wanawake mbona humusemi mkewako mbwa wee

    ReplyDelete
  5. Aseme mke wake achekwe

    ReplyDelete
  6. Kwa mtu mshirikina kama mwigulu mke wake amepona kweli?

    ReplyDelete
  7. It might be true

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad