Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
KAMATI ya rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania, TFF chini ya mwenyekiti wake, mwanasheria Julius Lugaziya leo mchana inaendelea kumalizia kujadili rufani ya mgombea aliyeenguliwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, Michael Richard Wambura.
Kikao cha kamati hiyo kilianza jana majira ya saa 5:00 asubuhi katika hoteli ya Courtyard, Upanga, jijini Dar es salam na kuahirishwa saa 4:30 usiku, lakini ngoma ililala bila kufikia maamuzi na leo hii kamati inatarajia kukutana tena saa 6:00 mchana ili kumalizia na kufikia maamuzi ya mwisho.
Hamu ya wadau wengi wa soka na wanachama wa Simba wanahitaji kufahamu kama Wambura anarudishwa au anaondolewa rasmi katika kinyang`anyiro hicho.
Jana kamati ya Lugaziya alifikia sehemu nzuri kwa kuhoji pande zote mbili kwa maana ya wakata rufaa na wakatiwa rufaa na leo wanaanza kupitia maelezo yao na kuyapima uzito na kufanya maamuzi.
Mtandao huu umekuwa ukipokea simu na jumbe fupi za simu kutoka kwa wadau wake wakiuliza nini maamuzi ya kamati ya rufani ya TFF iliyokutana jana.
Jana timu yetu ilipiga kambi maeneo ya Courtyard kufuatilia `ngado kwa ngado` kinachoendelea kwenye kamati hiyo ili kuja na jibu sahihi, lakini kulikuwa na usiri mkubwa mno, japokuwa kila mtu alikuwa anasema lake.
Hata siku moja, mtandao huu hauandiki taarifa ambayo haijathibitishwa na vyonzo makini.
Ukipita kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi wanaandika kuwa Wambura karudishwa wengine wanasema kaondolewa.
Taarifa hizi si rasmi kwasababu maamuzi hayajafikiwa mpaka sasa.
Kuna uwezekano hatima ya Wambura ikajulikana leo jioni, kwahiyo wadau wetu kuweni na subira.
Taarifa za kwenye mitandao si za kiziamini kwa asilimia zote kwasababu kuna uhuru wa kuandika na kuchapisha habari. Wengine wapo kwa ajili ya kuwavutia wasomaji, lakini sisi hatufanyi kazi kwa misingi hiyo.
Hatujapata taarifa rasmi na wahusika walisema wanakaa tena leo, kwa maana hiyo taarifa rasmi itatoka leo.
Asante kwa kuwa nasi na tutazidi kuwafahamisheni kinachoendelea kwa wakati huu.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=1833#sthash.cvx32ghD.dpuf