Serikali ya Rwanda imedaiwa kuwazuia kupita nchini humo baadhi ya askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliotoka kukisambaratisha kikundi cha waasi wa M23 kilichokuwa Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo (DRC) .....
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichozungumza jana na MTANZANIA Jumatatu kimedai wanajeshi hao walitakiwa kuanza safari leo kuja nchini kupitia Rwanda lakini walizuiliwa bila sababu za msingi.
Chanzo hicho kilisema: "Hali ya usalama kati ya Tanzania na Rwanda sio nzuri hata kidogo,Wanajeshi waliomaliza majukumu yao nchini Kongo walikuwa waanze safari yao kurudi Tanzania kesho ( leo ) kwa kupitia Rwanda, lakini katika hali isiyo ya kawaida Rwanda wamekataa kupitisha askari hao nchini mwao.
"Mungu jalia viongozi wetu hekima na busara katika kuamua suala hili zito kwa kuwa kama tutaingia katika vita wanaoteseka ni watoto, wanawake na wazee ambao hawana uwezo wa kwenda kuishi nje ya nchi, sala na dua zinahitajika sana kwa kuwa Mungu ndo kila kitu," mwisho wa kunukuu
Akizungumzia suala hilo, msemaji wa JWTZ,Luteni Kanali Erick Komba alisema hafahamu kama wanajeshi hao walikuwa wameanza kurejea nyumbani, hivyo apewe muda hadi atakapofika ofisini leo ndipo atahakiki taarifa hizo.....
Mgogoro wa Tanzania na Rwanda ulianza kufukuta baada ya Rais Kikwete kumshauri Rais Kagame wa Rwanda azungumze na waasi wa serikali hiyo wanaofahamika kama FDLR, ambapo Kagame aligoma na kuanza kumtolea maneno ya kashifa Rais Kikwete.....
Hata hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya M23 kusambaratishwa na JWTZ walioungana na wanajeshi wengine wa vikosi vya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO).
M23 ni kikundi kilichodaiwa kuundwa na askari wa makabila ya Rwanda, jambo linalopingwa vikali na Rais Kagame.....
Katika hatua nyingine, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa mataifa, Benard Membe alikiri kuwapo kwa uhusiano mbaya kati ya Tanzania na Rwanda.Kauli hiyo aliitoa bungeni mjini Dodoma hivi karibuni alipowasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014/ 2015.
Alisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mbaya kwa sababu kuu mbili kubwa.
"Ni kweli tuna uhusiano mbaya na Rwanda, kwanza tunaogopana kwa kuwa kila upande mmoja ukiongea na hasimu wa mwenzake inaonekana kama kuna hujuma inataka kufanywa.
"Pili kuna watu wanapeleka maneno ya chokochoko.Pia M23 ni wanamgambo wa Rwanda na kuna ushahidi kwamba Rwanda ilipeleka wanajeshi kuwasaidia wakati wa mapigano na serikali ya DRC yakiendelea, ushahidi huo upo," alisema Membe
Tanzania ina historia iliyotukuka katika ukombozi wa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na ndio maana ilichaguliwa kuongoza majeshi ya kulinda amani DRC
Mwaka 2008, makamanda na wapiganaji wa JWTZ waliongoza vikosi vya washirika katika kazi ngumu ya kumng'oa kanali Bacar wa Visiwa vya Comoro na Anjouan.
Uamuzi wa AU kuipa kazi hiyo Tanzania kuongoza mapambano hayo haukuwa wa bahati mbaya, bali ulitokana na kutambua kuwa ni nchi iliyoshiriki na kufanikiwa katika vita mbalimbali ya ukombozi
Si watumie njia waliyotumia walipukuwa wanaenda huko?
ReplyDeleteKweli, wakati wanaenda walipita wapi?. Watumie njia ileile kurudi.
DeleteSi watumie njia waliyotumia walipukuwa wanaenda huko?
ReplyDeleteBalozi za Tanzania,zilizoko nje ya nchi ziwasiliane na Watanzania ,waliok o nje wanataarifa nyingi za hao jamaa,kuanzia tabia zao,na mabalozi wetu wafanye kazi,tushirikiswe ktk usalama wa nchi yetu,ila hatutaki shida ila km itashindikana tupo,tayari,.
ReplyDeletewatarudi vipi kwa njia ya miguu hakuna ndege? nyinyi kumbe wachokozi kila ushahidi mnao halafu mnataka kupita hapohapo hebu tumieni akili zenu.
ReplyDeleteSi wapitie ziwa Tanganyika ?
ReplyDeletewanataka kuchapwa hao rwanda yule kagame masikio kama popo anaroho mbaya mkundu wake
ReplyDeleteHii taarifa ilikanushwa na wanajeshi wetu jana kwawaliockiliza BBC
ReplyDeleteHabari hizi ni za UDAKU, hao wanajeshi wa JWTZ waliko DRC wako huko kama kikosi cha Umoja wa Matifa(UNO), njia ya kurudia kwao ni masuara ya kimatifa na sio kitaifa kuishirikisha TZ, wandishi acheni udaku katika kuvunja mahusiano mazuri na majirani.
ReplyDeleteViongozi wa tz wasenge kweli nyie mliwapeleka kwa njia ya ndege sasa tatizo liko wp mkitumia ndege mbwa nyie mmekalia ufisadi tu sasa ole wenu kaka yangu asirudi salama wakati ameshafanya kazi mliompelekea vizur kudadadeki zenu nawaletea alshababi kama kenya
ReplyDeletewewe 10;52 wacha usenge hoa al shababu ni wasenge wenzio waganga njaa walete wachezee kichapo.
ReplyDeleteChonde chonde kaka/dada, naomba usiwalete al shabab maana tutakuwa hatuna amani nchini kwetu.
ReplyDeleteWewe na wew unamsikiliza boya huyo?alishabab hao wavaa sendozi si wasenge tu!eti wanadanganywa ukiua ndio utakwenda mbinguni kuma nyoko zao.
Delete