Wanawake CCM Wamfariji Vicky Kamata Baada ya Harusi Yake Kukwama

Wabunge wanawake wenye muda mrefu bungeni pamoja na mke wa waziri mkuu, Mama Tunu Pinda juzi walimuandalia sherehe ya kumfariji mbunge wa viti maalum (CCM), Vicky Kamata baada ya harusi aliyotarajia kufunga wiki iliyopita, kukwama.

Sherehe hiyo ya faraja, ilifanyika Hoteli ya Dodoma kati ya saa 1.00 jioni na saa 6.45 usiku juzi mjini hapa.

“Unajua hata yeye mwenyewe tulim-surprise (tulimshtukiza). Alijua kuwa ni chakula cha jioni, lakini alipofika alikutana na muziki, kwaya na wabunge wengine waliompokea kwa vifijo na nderemo,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria hafla hiyo. Sherehe hizo zilitumbuizwa na kwaya ya kikiristo ya Mvuke ya kanisa la Anglican mjini Dodoma.

Alisema Vicky alijua kuwa amealikwa na mbunge wa viti maalum (CCM), Magreth Sitta kwa ajili ya chakula cha jioni lakini alipofika aka kutana na sherehe.

“Tuliona ni vyema kumuandalia sherehe kidogo ili kumpa moyo kwamba hayo yametokea kwa sababu Mungu alitaka kumuepushia na mambo makubwa siku za usoni,” alidokeza mmoja wa waliohudhuria sherehe hiyo.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria ni wabunge wa viti maalum kutoka CCM ambao ni Magreth Sitta, Anna Abdallah, Felister Bura, Hilda Ngoye, Agness Hokororo na Anastazia Wambura.

Wengine waliohudhuria ni Asumpta Mshama (Nkenge-CCM), Anne Kilango (Same Mashariki-CCM) na Waride Bakari Jadu (Kiembe Samaki-CCM). Chanzo hicho kilisema wabunge Anne Kilango, Magreth Sitta na Anna abdallah, walielezea jinsi baadhi ya wanawake viongozi walivyokumbwa na mikasa kama ya Vicky na wengine hata kuacha wakiwa makanisani.

“Wengine walieleza jinsi walivyoteswa na wenza wao na kwamba amshukuru Mungu pengine amemuepushia mambo makubwa ambayo yangeweza kutokea kama ndoa ingefungwa,”alisema shuhuda huyo.

Alisema sherehe hiyo ilikuwa kama ibada maana muda mwingi ulitumika katika kumuhubiria Vicky na kumsihi asikatishwe tamaa na badala yake asonge mbele.

Alipoulizwa kuhusu sherehe hiyo, Vicky alikiri kufanyika lakini akakataa kuielezea kwa kina.

“Mimi niliitwa kwenye chakula cha jioni lakini nilipofika pale nistaajabu kukutana na sherehe,”alisema Vicky ambaye alikataa kuelezea kwa kina kuhusu sherehe hizo.
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bora ndio maisha my dear

    ReplyDelete
  2. Be strong mdada

    ReplyDelete
  3. Aache nyodoooo

    ReplyDelete
  4. na bado io ni trela

    ReplyDelete
  5. Muosha, huoshwa dont forget that eeh....,.....!!!!

    ReplyDelete
  6. Mibunge mingine bwana!Rest in peace Amina chifupa

    ReplyDelete
  7. Mijitu inayo sympathy na hili javi la wageni inaniboaaaa?

    ReplyDelete
  8. Watu wengine wana bahati kapelekwa na mume Wa .... Uingereza kusoma,karudi kapewa ubunge,this world is fucking unfair.

    ReplyDelete
  9. Vicky alipomchakachua mh.amina chifupa,wabunge wanawake mafisadi wa ccm waliona na kukaa kimya,leo kwa unafiki wao wanaitisha hata kwaya,wanamjua Mungu gani hao?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Mungu wao wanaomuomba atakuwa Mungu Wa maboksi,Si MUNGU aliyeumba mbingu na nchi.

      Delete
  10. mume wa zamani wa mama Kilango, mzee Nyange alimtesa sana yeye na watoto kwa umalaya na mwisho kuwatelekeza. Mama huyoo akabeba watoto wake na kuwalea mwenyewe, she is a very strong woman.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad