WACHEZAJI Neymar na Oscar wamepeleka vilio Croatia baada ya kuipa ushindi wa mabao matatu timu yao ya Brazil kwenye mechi ya ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia 2014 zinazofanyika nchini Brazil.
Croatia walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 ambalo ni la kujifunga likiwekwa kimiani na beki Marcelo wa Brazil.
Baadaye wenyeji Brazil walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wao mahiri anayefananishwa na Pele, Neymar kwa shuti la mbali lililomuacha mlinda mlango wa Croatia, Stipe Pletikosa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Neymar aliipatia Brazil bao la pili kwa mkwaju wa penalti ambao kipa Pletikosa alijaribu kuupangua lakini ukajaa wavuni na kuwapa wenyeji ushindi wa 2-1 dakika ya 71.
Mchezaji wa Chelsea, Oscar alihitimisha furaha ya waandaaji fainali hizo kwa bao lake la tatu dakika ya 90 ya mchezo.
Mpaka mwisho, Brazil 3, Croatia 1.
Leo michuano hiyo itaendelea ambapo Cameroon watavaana na Mexico, Uholanzi wakikwaana na Hispania huku Chile wakipepetana na Australi
wangefungwa ingekuwa aibu maana haijawahi tokea katika michuano ya kufungua kombe la dunia wenyeji wakafungwa
ReplyDeleteBureeee. wamebebwa. haikuwa penalti. Bureee kabisaa referee
ReplyDeletewangefungwa mashindano yasingefanyika fujo kama kawa
ReplyDelete