Aibu:Gari ya Mtoto wa Malecela Lakamatwa Kwa Kushindwa Kulipa Madeni

MKURUGENZI wa Kampuni ya Ntyuka Security ya mjini Dodoma, Samwel Malecela ameingia matatani baada ya gari lake aina ya Toyota Prado kukamatwa kwa ajili ya kupigwa mnada kutokana na kukabiliwa na madeni.

Samwel ni mtoto wa waziri mkuu wa zamani, Mhe. John Malecela ambaye pia aliwahi kuwa mbunge katika Jimbo la Mtera kwa miaka mingi.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa, gari hilo lilikamatwa baada ya wafanyakazi wa kampuni ya Malecela kupeleka madai yao ya mishahara na malimbikizo mengine kwenye Tume ya Usuluhishi mjini Dodoma na kushinda.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, mmoja wa walinzi wa kampuni hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema: “Tupo  21, kwa muda mrefu sana tumesumbuliwa na mishahara yetu, tukaamua kwenda usuluhishi.

“Kweli akapelekewa barua ya kuitwa lakini hakufika, ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana. Baadaye tarehe 15 mwezi wa saba, mwaka huu hukumu ikapitishwa. Sisi tukaonekana tuna haki, kwa hiyo jumla alitakiwa kutulipa milioni nne na laki mbili (Tsh. 4,200,000),” alisema.

Alisema, hata bosi wao alipopewa taarifa ya hukumu hiyo, hakuonyesha ushirikiano jambo lililosababisha wahusika watoe idhini kwa madalali wa Mchinda Auction Mart, kukamata gari hilo kwa ajili ya kulipiga mnada ili walinzi hao walipwe stahiki zao.

Akizungumzia ishu hiyo kwa njia ya simu, Samwel alisema ameshangazwa na kitendo cha gari lake kukamatwa, huku akisisitiza hakuwa na taarifa za kesi hilo kuendeshwa na tume hiyo.

“Mimi nashangaa sana na nitaendelea kushangaa. Sijawahi kupewa notice ya kuitwa kwenye tume ya usuluhishi, kesi imeendeshwa bila taarifa, hadi nakuja kushtukia gari langu limekamatwa.

“Halafu mali inapochukuliwa na madalali kwa kawaida lazima mhusika apewe notice ya siku 14, sijapewa notice yoyote. Halafu najiuliza kwa nini wakamate gari wakati kampuni ina mali zinazofaa kupigwa mnada?” alihoji  Samwel ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
GPL

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watoto waviongozi mmezididhulma hata mlinzipia unawadhulumu? Wewe unawalipa sizaidiya lakinanusu kwa lindo kwamwezi,wewe unalipwa sichini ya laki5 kwalila lindo huoni aibu? Kesho na ww unagombea uraisi,au unakua wazr mkuu si utatuua sote upate ww aaah Kaka linda heshma yako wape hakiayao

    ReplyDelete
  2. Sasa Le Mutuz billionea yuko wapi???? Ubillionea wake uko wapi kama anashindwa kuokoa jahazi la mdogo wake????? Aibu mpaka magazetini...Halafu je hii habari iko kwenye hicho ki blog chake????? Watoto wa vigogo acheni dhulumati. Aibuu halafu baba yenu kaamua kuwalundika wote kwenye hicho Chama, yani nyie woooote ni wanasiasa wapenda vya mteremko. Kweli tutafika jamani????????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad