Wiki Ijayo Alikiba atakuwa mgeni katika kipindi cha runinga cha The Sporah show. Katika promo ya mahojiano yake na Sporah inayoendelea kurushwa kupitia Clouds TV, Alikiba amemzungumzia Diamond Platnumz ambaye huwa inasemekana wana-beef.
katika promo hiyo Sporah amemuuliza Alikiba kama Diamond ndiye amechukua nafasi yake kwenye muziki kwa kipindi alichokaa kimya, na majibu yake yanaongeza hamu ya kutokosa kukiangalia kipindi hicho.
Alikiba amejibu kuwa Diamond hajachukua nafasi yake, na kusindikiza jibu lake na mfano wa (nafasi yake) ni sawa na kiti kilichopata vumbi (kwa kutokaliwa siku nyingi) hivyo muda wowote akiamua kurudi anaweza kuamua kukifuta na kukikalia tena. Pia aliongeza kuwa Diamond amekaa kwenye kiti tofauti na yeye, lakini ni yuko ‘back seat’.
Kupitia 255 ya kipindi cha XXL pia leo Alikiba aliulizwa swali kuhusu yukoje sasa hivi na Diamond , haya ndio majibu ya hit maker wa ‘Cinderella’.
“Mimi niko okay sana sema sifikirii kuongea naye tu basi lakini niko very okay yaani. Yaani sijawahi kufikiria si unajua kuwa na mtu okay ni kuzungumza na kuwa karibu unajua hivyo vitu, yaani sijawahi kufikiria hata hivyo. Mi niko okay na sina chuki na sana sana nampongeza lakini sina chuki, simaind yaani niko veeery okay”.
Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”
Ali kiba my favourite, Ila ongeza ujanjaro
ReplyDeleteZitto kabwe mali unazouza sasa ili uimarishe Chama chako kipya cha siasa ACT itakula kwako mazima kwani kilibuniwa na Wassira,na sasa ccm wako bize na Ukawa.Nakushauri dogo uhifadhi mali hizo zikusaidie uzeeni kwani siasa ni mchezo mchafu usiotabirika
Deleteachen usenge nyie kama huna beef nae kwa nn? unasema hujiskii kuongea nae? ally k mm shabik wako mkubwa xana ila sio fresh kuish kwa mabef. hiyo sio picha nzur best.
ReplyDeleteilv ally k
ReplyDeletehata ukiwaangalia hapo juu utaona sura gani ndio imekaa kinuksi nuksi yaani kinongwa nongwa. Ha ha ha ha!
ReplyDeleteJust jokes.
mi nafikiri ali k hana matatizo ali domo ana matatizo kinyongo kwake hakiishi.angalia hata domo alivoachana na wema hata ile pesa aliyomtunza pale jukwaani alikataa kuipokea.......ss hatuwezi jua nyuma ya pazia..ila km watayamaliza itakua poaaaaaaa
ReplyDeletei real love alli kiba he is my favorite musician.
ReplyDeletekiba kama vile nipate namba yako niwe mshauri wako. asante
ReplyDeletebg up ally k.kwa kuwa na msimamo na endelea kuwa na msimamo wk kutokubonga na mtu c kwamba una bf nae .we endelea na mishe zk bro
ReplyDeleteAli is history meen, diamond platnumz is the new sheriff in town!
ReplyDeletekwenye sector ya muziki,ukianguka ndio basi,kuinuka kazi sana,tukubali tu kiba kabaki jina,kam nice na wengine
ReplyDeletebig up ally k i like ur personality huna uswahili kama domo dats wat i like abt u. its true diamond nimtu wakuweka chuki like da way alikataa pesa za wema
ReplyDeleteWewe Ali Kiba fanya muziki. Achana na huo utoto oohhh niko okay kabisaaaa. Ndio nini hiyo?? Fanya kitu kinachokuweka mjini. Acha mambo ya ghubu wewe mwanaume.
ReplyDeleteRoho ya Kike hiyo mdogo wangu wanaume wakikoseana wanaambina Yanakishwa acha ushamba.......
ReplyDeleteOhooo kiti changu kinavumbi nikikitaka na kung'uta vumbi mwaka wa wangapi huu...unatoba mafans wako wenzako wanakwenda mbele ww hupo palepale na GHUBU lako km SHORI
ReplyDeleteNakuaminia Sana ally kiba WW Ni jembe Sana! Napenda Sana nyimbo zako Ni nzuri Sana mpaka kesho. C za domo zote mapenzi mapenzi na yeye. Tumechoka na mapenzi ya nani amenunaa wemaaa!! Ally kiba unatisha Sana penda wewe Sana kazi nzuri!
ReplyDelete