Audio: Diamond awapa baraka zote wanaotumia sura yake kufanya biashara

Diamond Platinumz’ ni jina ambalo linakubalika zaidi ama jina la msanii wa bongo flava mwenye mashabiki wengi zaidi nchini Tanzania, lakini umati wa mashabiki wanaompenda Diamond ni soko la wajasiriamali ambao wanalitumia kuingiza siku.

Hivi sasa wapo wafanyabiashara wanaouza fulana zenye jina au picha ya Diamond bila makubaliano yoyote na msanii huyo.

Hata hivyo, wafanyabishara hao hawatakiwi kuwa na hofu. Mwimbaji huyo amefunguka katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm na kuwapa ruhusa wale wote wanaofanya hivyo.

“Kuwekwa tu pale kwangu mimi nimefurahi, nisiwe mnafiki. Siwezi kusema nimesikia uchungu eti kwa nini ametumia sura yangu hivyo. Yaani nimefurahi kwa sababu ninaona kama taifa limeni-appreciate kazi yangu na mtu katengeneza t-shits na kauza imeuzika kweli kwa sababu inaweza kuwekwa bwana ‘Salamu’ isiuzike (kicheko)…..mimi kwangu ni rukhsa” Amesema.

Ruhusa hii imepekwa hadi kwenye  saloon.

Hata hivyo, ametahadharisha kutotumia brand ya ‘Wasafi Classic’ kwa sababu hiyo ni brand yake. “Labda mtu atumie ‘Wasafi’, hapo tatizo lingine.”

Quote of The Day: Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We Fala tuwekee story ya mange mwizi wa mawig bwana

    ReplyDelete
    Replies
    1. nenda u turn blog utapata majibu ya unayoyataka mbweha wewe maskini wa nafsi usietaka maendeleo ya mwenzio nyooooo Mange anawachoma Moyo

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad