Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limetangaza orodha ya viwango vya ubora wa soka, ikiwa ni juma moja baada ya kukamilika kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.
Orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi, imezingatia matokeo ya michezo ya fainali za kombe la dunia, ambapo mataifa makubwa kama Uingereza yameonekana kutupwa mbali.
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia Brazil nao wameonekana kuanguka kwa kiasi kikubwa, ili hali waliokuwa mabingwa wa fainali hizo mwaka 2010 Hispania wameporomoka kwa kasi ya ajabu wakitokea nafasi ya kwanza.
Mabingwa wapya wa fainali za kombe la dunia, Ujerumani wamekalia kiti cha orodha hiyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa walipokuwa nchini Brazil, ambapo walicheza michezo saba pasina kufungwa mchezo wowote.
Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi July mwaka 2014.
1. Ujerumani (+1)
2. Argentina (+3)
3. Uholanzi (+12)
4. Colombia (+4)
5. Ubelgiji (+6)
6. Uruguay (+1)
7. Brazil (-4)
8. Spain (-7)
9. Uswisi (-3)
10. Ufaransa (+7)
11. Ureno (-7)
12. Chile (+2)
13. Ugiriki (+1)
14. Italia (-5)
15. Marekani (-2)
16. Costa Rica (+12)
17. Croatia (+1)
18. Mexico (+2)
19. Bosnia na Herzegovina (+2)
20. Uingereza (-10)
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
87. Uganda (-1)
95. Kenya (+13)
96. DRC (-12)
106. Tanzania (+7)
109. Rwanda (+7)
126. Burundi (+2)
Orodha kamili http://www.fifa.com/worldranking/rankingtable/
Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”