Balozi wa Libya Ajiua kwa Risasi Ofisini Dar

 Balozi wa Libya nchini Tanzania, Ismail Nwairat, amejiua kwa risasi jana ofisini kwake, katika tukio la kwanza la aina yake nchini kwa kigogo wa ubalozi kuondoa uhai wake.

Hadi sasa haijafahamika sababu za kujiua kwa balozi huyo ambaye alikuwa akipingana waziwazi na sera za utawala ulioondolewa madarakani wa Kanali Muhamar Gaddafi, aliyeuawa wakati wa mapinduzi Oktoba 2011.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa zilisema kuwa Nwairat alijifungia kwenye ofisi yake iliyopo Mtaa wa Mtitu, Barabara ya Umoja wa Mataifa na kujifyatulia risasi upande wa kushoto wa kifuani.

Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally alisema baada kusikia mlio wa bunduki majira ya saa 7:00 mchana, maofisa ubalozi walivunja mlango wa ofisi hiyo na kumkuta Nwairat ameanguka chini.

“Tumepata taarifa hizo na kubaini kuwa lilikuwa ni tukio la kujiua, marehemu alikutwa na risasi moja kifuani,” alisema Ally.

Alisema baadaye walimpeleka balozi huyo Hospitali ya AMI, Oysterbay ambako ilielezwa kuwa alikuwa ameshafariki dunia. Kwa sasa mwili wa balozi huyo umehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhifadhiwa kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Libya.

Ally alisema hadi sasa hawajafahamu sababu za balozi huyo kujiua kwa kuwa hakuacha ujumbe wowote.

Nwairat anajulikana kwa kuwa mpinzani wa wazi wa utawala wa Gaddafi, ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi wa Libya tangu alipoingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 1969.

Katika hafla ya kuadhimisha miaka mitatu ya mapinduzi ya Libya iliyofanyika Machi 9 jijini Dar es Salaam, Balozi Nwairat aliuelezea uongozi wa Gaddafi kuwa wa ukandamizaji, wa kiimla, usiotumia katiba na ambao uliwanyima wananchi wake haki ya kujieleza ndani na nje ya nchi hiyo.

Kuhusu taratibu za mazishi, Ally alisema kwa sasa Wizara inafanya inafanya jitihada kushirikiana na wafanyakazi wa ubalozi huo pamoja na ubalozi wa Tanzania Libya kuangalia taratibu za kusafirisha mwili huo.

“Serikali itawapa ushirikiano wote watakaohitaji ili kufanikisha mwili wake kusafirishwa na atapewa heshima zote za kidiplomasia kama inavyotakiwa na kama wafanyiwavyo mabalozi wote,” alisema.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, pamoja na kueleza kufahamu tukio hilo, alisema angetoa maelezo ya kina leo katika mkutano maalumu na wanahabari.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na bado Damu ya Gaddafi inawarudia

    ReplyDelete
  2. shenz kbisaaa watajiua sana walivyomfanya Gaddafi vile mbwa kbsa angejipiga nayakinyeo kbisa

    ReplyDelete
  3. Why?labda alijijua kwamba labda Ana maradhi yasiotibika?why ajiue then?

    ReplyDelete
  4. mzimu wa gaddaf3 July 2014 at 15:21

    Labuda alikua ma ukimwi atajiuaje?

    ReplyDelete
  5. malipo hapahapa duniani watajiua mpaka mama zao makatili wakubwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad