Na Gabriel Ng’osha
MWANADAFADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.
Batuli alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu, matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika nchi zenye misimamo mikali.
“Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia,’’ alisema Butuli.