Davina wa Bongo Movies Apewa Kichapo cha Nguvu na Mmewe Baada ya Kukutwa Akiongea na Simu Kimahaba

Na Musa Mateja
KIBANO! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kupewa kipigo kikali na mumewe, muda mfupi baada ya kukutwa akiongea kimahaba na simu iliyodaiwa kupigwa na mwanaume mwingine.


Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa msanii huyo, Mbezi-Beach, Dar, Julai 22, mwaka huu ambapo Davina alikutwa akizungumza na mwanaume ambaye haikujulikana mara moja ni nani ndipo mumewe alipomshushia kipigo ‘hevi’.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu familia hiyo, mume wa Davina aliibua timbwili hilo baada ya kumsikiliza kwa makini mkewe huyo na kugundua anazungumza na mwanaume mwingine wakiahidiana kitu f’lani.

“Mumewe alitega sikio kwa makini na kugundua alikuwa akizungumza na mwanaume, akamsogelea karibu na kunasa mazungumzo yao, akamuoma simu mara moja, Davina akaanza kujitetea ndipo mtiti ulipoibuka, mume akaanza kumpiga mke ingawa hakumuumiza kiivyo,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya data hizo kutua kwenye Dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimvutia waya Davina ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa hakuwa akiongea na mwanaume huyo kwa lengo baya zaidi ya maongezi ya kikazi.

“Dah! Umejuaje hii ishu ni ya kifamilia hivyo! Mmh...kweli ninyi ni noma, anyway ishu ni kwamba, mume wangu alinifuma nikiongea na simu ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ananipigia ili anipatia fedha zangu ambazo zilibaki baada ya kufanya tangazo moja linalohusiana na mambo ya Ukimwi.

“Wakati naongea, yeye (mumewe) hakujua nini kinaendelea zaidi alikuwa akisikia sauti ya mwanaume tu na majibu yangu kweli akajikuta amepaniki na kunivaa akiwa ana hasira, si unajua mtu yeyote anayekupenda wivu huwa ni kitu cha kawaida tu lakini nilimwelewesha baadaye akanielewa na maisha yanaendele kama kawaida,” alisema Davina.
GPL

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo Bongo kila mtu ni staa wa filamu za kibongo. Hivi kuna ma staa wangapi. Na soko lenyewe la kuwapa ustaa liko wapi????? Kwa kweli kazi ipo. Jamani shikeni majembe mkalime acheni huo ustaa hewa na umalaya uliotukuka. Staa gani huna Management ya kufuatilia mambo yako. Mpaka unaanza kufanya umalaya kwenye simu mbele ya mume wako lools.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mm nahisi wangejifunza kuuelewa maana ya staa na msanii kama nje wa fanyavyo. Sasa utakuta mtu ameigiza movie moja tu tayari ataitwa star. Apo ndo ninapoona ujinga wa hawa waandishi pamoja na ao bongo movies na bongo flava kujita mastaa ili hali maisha wanayoishi hayafanani na maisha ya kistar

      Delete
  2. Uyo mwanaume wacha yamkute kwani yeye pia alimtenda mwanamke wake wa mwanzo kabla ya davina tena amlimtenda vibaya na utapeli juu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad