Dr Dre ashitaki Makampuni ya kichina yaliyoingiza $ Billion 135 kwa kuuza headphones fake za 'Beatz By Dre'

Dr Dre na Jimmy Lovin ambao wanaendelea kushangilia kuwa mabilionea baada ya kuwauzia Apple kampuni yao ya Beatz Electronics kwa $ Billion 3 tu, wamepata mshituko baada ya kugundua kuwa Makampuni ya kichina yameingiza pesa hiyo zaidi ya mara 40 kwa kuuuza headphones fake za ‘Beatz By Dre’.

Kwa mujibu wa TMZ, makampuni mengi ya China yamegundulika kuwa yalikuwa yanatengeneza headphones zenye logo ya Beats na kuuza kwa bei nafuu dunia nzima kwa njia ya mtandao wakitumia tovuti mbalimbali.

Dr Dre amekasirishwa na hatua hiyo na amefungua mashtaka dhidi ya makampuni hayo na kitu cha kwanza alichoiomba mahakama ni kuhakikisha kwanza wanachukua majina ya ‘domain’ za tovuti zote zinazofanya biashara hiyo na pia kuhakikisha faida zote zinazopatikana kwenye mauzo hayo.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona hata bongo ndo hizo mnatamba nazo barabarani! Headphones hizo original ni zaidi ya laki tano za kibongo..mje mabishoo wangapi wangezimudu?!!

    ReplyDelete
  2. Mbona hata bongo ndo hizo mnatamba nazo barabarani! Headphones hizo original ni zaidi ya laki tano za kibongo..mje mabishoo wangapi wangezimudu?!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad