Wanajeshi wa kupambana na ugaidi nchini Kenya (ATPU) wanawashikilia raia watatu wa Tanzania waliokamatwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Somalia na Kenya ili kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.
Kamanda wa Polisi Lamu Mashariki amethibitisha kukamatwa kwa watatu hawa ambao wote wana umri chini ya miaka 22 ambao kwa sasa wanashikiliwa na maafisa wa kupambana na Magaidi Kiunga mpaka wa Kenya na Somalia ambapo baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Kukamatwa kwa watatu hawa kunafikisha idadi ya vijana sita wa Kitanzania waliokamatwa nchini Kenya ambao wanatuhumiwa kujiunga na mtandao wa kigaidi ambapo wengine watatu wanashikiliwa kwenye gereza la Kamiti waliokamatwa Kiamboni.
Miongoni mwao ni Bakari na Daudi ambapo walipohojiwa wamesema >>> ‘Tumeambiwa kwamba Somalia kuna Waislamu na wako katika hali ngumu, kuna majeshi mengi yanawanyanyasa Waislamu kwa hiyo kama Muislamu inabidi uende kutoa support kwa ndugu zako, kutokana na imani yangu kujengeka katika dini ndio nikajikuta naunga safari’
Haya yanajiri baada ya vijana kadhaa wa Kenya kukamatwa mpakani walipokua wakifanya mpango kuvuka mpaka na kuingia Somalia vilevile msajili wa kundi la Al Shabaab amekamatwa akiwapeleka vijana wawili wa Mombasa kwenda kujiunga na Al Shabaab mjini Garisa.
Wakati huohuo Polisi wanawasaka vijana waliotumwa na Al Shabaab kwenye mataifa ya Kenya na Tanzania kusubiri kupewa maagizo ya kundi hilo kutekeleza mashambulizi.
Unaweza kuwasikiliza wakiongea hapa chini.