Hii Kali:Mwakyembe Amfukuza Mfanyakazi wa Airport Aliyestaafu 2013

Waziri Titus kamani amesema mmoja wa watu waliotangazwa na Mwakyembe juwa wamefukuzwa aiport jana alishastaafu tangu 2013 na sio mfanyakazi wa serikali tangu wakati huo.

Waziri Kamani amesema ameshangazwa kuona mstaafu anatangazwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa wizara yake kama alivyotangaza Mwakyembe jana.

Hata hivyo waziri kamani amesema anasubiri taarifa zaidi toka kwa Dr Mwakyembe kuhusu hatua alizotangaza jana kufukuza wafanyakazi wa wizara yake waliokuwa wakifanya kazi JKNIA.

Source:Radio one Habari

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa

    Ujinga mtupu mambo ya maana yanawashinda kitu kidogo anakusanya waandishi.mkubwa mzima apenda misifa ya kijinga.ndio maana kachemka


    ReplyDelete
    Replies
    1. he he he..mbona unatoka povu hivyo mkuu.. na wewe ni victim nini?

      Delete
  2. Mbona Waziri Mwakyembe ni kama vile yuko so much uninformed. Nadhani ile line of communication na wasaidizi wake itakuwa mbaya sana. Kwa maana haiko that effective. Hii ni kama mara pili au tatu kwa Waziri Mwakyembe kuchukua hatua za kiutendaji zinazoleta walakini. Sasa tatizo liko wapi???? Hii ilionekana kuanzia ile issue ya Masongange. Je hao wasaidizi wake ni kweli wana nia njema na Waziri Mwakyembe au wako hapo kumdhoofisha. Ni suala linalotakiwa kutupiwa macho ikiwamo kuwafukuza kazi wale wasaidizi wake. Inakuwaje leo hii Waziri mzima anaende kumfukuza kazi mtu ambaye tayari hayuko kwenye ajira. I mean hicho ni kichekesho na aibu kwa Wizara kama sio Waziri mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. Hii inaleta taswira ya utendaji mbovu uliotukuka wa Serikali ya Tanzania na watendaji wake. Unajaribu kufikiria kama Waziri Mwakyembe anaweza kufanya makosa ya kipuuzi kama haya. Vipi kuhusu Mawaziri wengine na watendaji wale wa kawaida ndani ya Serikali???? Kwa kweli hili ni jambo la aibu kwa Serikali ya Tanzania na kwa kweli linasikitisha. Inaonyesha jinsi gani Watendaji wa Serikalini wasivyokuwa makini/serious na kazi zao.

    ReplyDelete
  4. Sio mzima huyu baba, pia wale waliofukuzwa kazi kwa sababu ya kumpitisha masogange si warudishwe wakati mhalifu yupo huru. Mimi nahisi huyu baba hata hawazagi akiamka anasimama na msimamo mmoja tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Actually sio yeye bali ni wale wasaidizi wake ndio wanaomuangusha. Kwa sababu kiutaratibu kabla Waziri yeyote hajafanya Press Conference ile Report atakayo submit pale inatakiwa iwe edited na wasaidizi wake kwa kuzingatia Facts za ile report. Wasaidizi wake ndio wanaomuangusha.

      Delete
  5. I don't think he is a parrot......NO NO Please. Hii ni taswira ya utendaji mbovu uliotukuka wa Serikali ya TZ

    ReplyDelete
  6. kwanini wasaidizi wamshikie akili zake.?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haitakuwa sahihi kumlaumu moja kwa moja Waziri Mwakyembe hasa ukizingatia Ukubwa wa Wizara anayoisimamia pamoja na majukumu yake. Huyu ni Waziri mwenye majukumu mazito. Wasaidizi wake kimsingi ni watu wa hovyo hovyo tu. Hawana ile competence, skills na knowledge enough ya kumshauri Waziri. Sasa hilo ndio tatizo linalomfanya Waziri Mwakyembe aonekane hafai. Lakini Waziri Mwakyembe ni highly effective leader katika hiyo Serikali ya Tanzania.

      Delete
  7. we vp kazi km iyo awezi fanya peke yake lzm kuna wasaidizi wake ndiyo waliomuharibia sbb mwakyembe apendi ujinga

    ReplyDelete
  8. sio kwamba watu wake ni wa ovyo,huyu anatafuta kiki ya uprezidar sasa anakaa na wana ccm wenzie wanajifanya kwamba yuko makini sasa anakuta kuna watu awataki upuuzi wake wanamchana live

    ReplyDelete
  9. anasubiriwa bungeni watampasha live

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad