Huu ni Ujumbe wa Kajala Kwenda Kwa Mtoto Wake Kwenye Siku ya Kuzaliwa Kwa Binti Yake Huyo.

Miaka 12 iliyopita sikuwahi kujua kama itafikia siku nitajisikia hiki ninachofeel siku ya leo.. nimepitia mambo mengi sana na wewe.. nimepata shida nyingi mno lakini sikukuacha wala kukutupa.. kwenye jua ama mvua, iwe usiku ama mchana katika mitihani yote niliyopitia nilikuwa na wewe tu mwanangu.. ulikuwa kama pochi yangu.. bila kujua kesho utakuwa NANI!! nilikupenda tangu siku ya kwanza nakuona.. nilikuthamini na kuahidi nafsi yangu kuwa nitakufa na wewe katika hali yoyote ile bila kujua wewe una hisia gani juu yangu... wala sikujua kama unaweza kuja kuwa faraja kwangu.. Paula!!! Mtoto wangu wa utotoni.. mtoto ambae nna historia kubwa na wewe..

LEO napenda kumshukuru sana MUNGU kwa kunipatia wewe.. sababu uwepo wako wa miaka 12 kwenye Dunia hii umenipa majibu yote ya maswali niliyokuwa najiuliza... Umekuwa faraja kubwa sana kwenye maisha yangu.. Pamoja na umri wako kuwa mdogo umeweza kusimama na mimi kwenye hali zote.. nimeshuhudia lililoniumiza likikuumiza pia.. umenifanya nione thamani yangu.. umenipa thamani kubwa sana kwenye maisha yako.. katika safari hii umenihakikishia kuwa nina mtu mmoja ambae hata Dunia nzima initenge na kunizomea.. YEYE ATABAKI KUWA NA MIMI!!! Tena kwa moyo mmoja na mapenzi... na mtu mwenyewe si mwingine yoyote.. ila ni WEWE mwanangu.. nakupenda sana Paula!! Na nakuombea MUNGU akukuze kwenye imani na akupe kila la kheri katika dunia hii.. nilikupenda jana ukiwa mikononi mwangu, ninakupenda leo ukiwa binti na naahidi kukupenda milele katika maisha yangu ukiwa kwenye hali yoyote ile.. ulikuwa wa kwangu na utaendelea kuwa wa kwangu mpaka mwisho wa maisha yangu.. HAPPY BIRTHDAY my daughter!!!! NAKUPENDA SANA!

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Post a Comment

28 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wamependeza wenyewe aya ongelen mwaya miaka 12sihaba umejitahid.

    ReplyDelete
  2. Kwel watoto wa kidigital miaka 12.utasema ana26 ivi aya ongereni mama na mwana

    ReplyDelete
  3. mtoto anachachuliwa sana ,,,,,mtu mzima sasa anatafuta kick

    ReplyDelete
  4. Nimewapenda sana,Happy birthday Paula.
    Mpende mama kama anavyokupenda,usimpe maudhi,usimfanyie jeuri,msikilize kila apokuonya.
    HAKUNA KAMA MAMA PAULA,
    MUNGU AWABARIKI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah! mdau umenitoa machozi,God bless you!

      Delete
    2. Thank you,Mungu akubariki na kukulinda siku zote za maisha yako.

      Delete
  5. Kajala anajua kuandika jamani,safi sana.
    Happy birthday Paula.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona eeh! kitu kinaeleweka,hakuna konakona,
      Hongera kajala,paula iga basi kwanini wewe huandiki kama mama?

      Delete
    2. Kweli,na Joyce kiria aandike vizuri,hajui kuandika kabisa.

      Delete
  6. Kajala umenikumbusha mbali Sana! Katika dunia hii akuna kama mama na akuna kama mtoto. Cha msingi mlee mwanao katika maadili ya kuwa na hofu ya mungu, kwani hiyo ndo mboni yako, akiaribikiwa umearibikiwa PIA. Akifanikiwa umefanikiwa PIA. Na maombi kwa mwanao Ni muhimu PIA. Na mungu akubariki kajala na ampe mwanao maisha marefu Sana.

    ReplyDelete
  7. wema tasa uko wapi?

    ReplyDelete
  8. Jaman nana yuko wap cku hizi simuoni!nimemic!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nana siku hizi ni VEE CASH

      Delete
  9. Sijui mwenzangu et we Nana upo ?

    ReplyDelete
  10. WEWE 12:05 ACHA USENGE,KILA UKIINGIA HUMU WEWE LAZIMA UMTUKANE WEMA,ME NINA MASHAKA NA WEWE UENDA MMOJA WA WALE ALIOWASEMA MAMA DIAMOND,KUWA MNAMTUMIA PICHA ZA UTUPU,MAANA KILA SIKU HUNA JIPYA WEMA TASA,SASA UNATAKA KUMFANANISHA WEMA NA KAJALA,KAJALA MTU MZIMA,ANAKIMBILIA AROBAINI,WEMA HATA THERATHINI HAJAFIKA,EBU ACHA CHUKI,TEAM UKWELI NA UWAZI,HUNA HAYA.

    ReplyDelete
  11. nana ndio huyo vee cash mshenzi mkubwa mwenzio amwandikia mwanaye msg nzuri ww wasema atafuta kick kwa kua si swahiba na wema kama zamani. grow up n c da facts kisha ungekua mzazi hungeongea hivo uwa wachafua tu hali ya hewa cjui uwa walipwa. congrats kajala inpite of everything wat counts at the end of the day ur a good mother to ur daughter.

    ReplyDelete
  12. ukimtetea wema wafaidika na nini na wewe da bad thing mwapenda pigia watu debe ambae ata c role model wa maana ni real life would u want ur daughter to grow up n live like wemas life style. uwa mwalipwa sijui mcheeeeeeeeeeeeeewwwwwwwwwwwwwww.

    ReplyDelete
  13. mungu awe nanyi nakuwalinda sikuzote kajala na Paula.raha kuitwa mama naninaona Una enjoy kuwa mama that's good.

    ReplyDelete
  14. NDIO KAZI YA HUYU NANA USHENZI TU NA MALIMBENDE YAKE TWAKUJUA NI WEWE VEE CASH KAZI KUMSHABIKIA WEMA TUUUUU. WAMPONDA KAJALA YA NINI NA AMWANDIKIA MTOTO WAKE. ATAFUTA KICK PIA KWA MANAYE AHHHHHH WEWE KUMBAVU HUNA MAANA.KAJALA ULIVOSEMA NI KWELI HAKUNA KAMA MTOTO MUNGU AWAZIDISHIE MAPENZI NA IMANI KATI YENU AMEEN

    ReplyDelete
  15. Happy birthday Paula. maneno ya mama yako yamegusa sana. Mungu awabarki

    ReplyDelete
  16. Daaa!kumbe kabadilishabjina!homgera maana umebadil jina na matusi umeacha

    ReplyDelete
  17. awache wapi idiolmonger huyo matusi tuuu vee cash. ur a
    good mum kajal ur words touched my heart u remind me of how i am wid my mum. God bless all mothers like u.

    ReplyDelete
  18. Kama ni nana yule aliyekua actress nasikia amefungwa brazil alikamatwa na madawa ya kulevya. Hongera kajala kwa sms yako kwa mtoto. Na paula uwe na moyo huohuo wa kuwajali wagonjwa maana jana nimeona ulienda kutoa msaada kwa watu wenye utindio wa mgongo mungu azidi kukupa moyo wenye huruma mwaaaaaah

    ReplyDelete
  19. actress gani huyo mjinga wa kumtetea wema sijui analipwa

    ReplyDelete
  20. Vee Cash a.k.a Nana wa Mitusi sura kama Ndulii Idiamini yani wewe na mimi sura zetu kama Pacha vile.Hongera kajala kwa kukuza ,mungu mbariki baby Paula akuevema.

    ReplyDelete
  21. Happy Birthday Paula, Mheshimu mama yako duniani hakuna kama mama aliekubali kutunza mimba yako kwa umri mdogo angeweza kukutoa kipindi hicho. Hongera Kajala kwa ujumbe mzuri sana sana kwa mwanao Mungu akutunzie na kumbariki

    ReplyDelete
  22. hahaha umenichekesha anny 10.43 kweli kabisa idiamini dada huyo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad