Web

Ikulu: Wanaomkosoa Jakaya Kikwete Kuhusu Katiba Hawako Sahihi

Ofisi ya Rais imesema kuwa wanaomkosoa Rais Jakaya Kikwete kuhusu msimamo wake katika mchakato wa Katiba Mpya hawako sahihi kwa kuwa ni mlezi na ana haki ya kutoa maoni yake kama mkuu wa nchi na kama mwanasiasa.

Pia, imewataka wasiokuwa wajumbe wa Bunge la Katiba waiache kazi hiyo mikononi mwa Bunge hilo kwa sasa hadi hapo rasimu itakapowasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya kuikubali au kuikataa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu ikiwa ni siku moja baada ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), kutoa tamko zito kwa Rais Jakaya Kikwete ikiishangaa kauli yake ya kupinga mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya Watanzania.

Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa na taasisi na watu binafsi baada ya kulieleza Bunge la Katiba kuwa kuna baadhi ya mambo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo hayawezekani kutekelezeka, akitoa mfano wa muundo wa Muungano wa serikali tatu, jambo ambalo CCT ilisema jana kuwa alitakiwa alifanye wakati Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikimfuata kumweleza maendeleo ya kazi yao.

Hata hivyo jana, Rweyemamu aliliambia gazeti hili kuwa: “Kinachoendelea kwa sasa kwa baadhi ya makundi ya kidini kutoa matamko dhidi ya Rais si sahihi, kwa kuwa Rais ni mlezi na ana haki ya kutoa mtazamo wake kama mkuu wa nchi na kama mwanasiasa.”

Alisema kimsingi mchakato huo ni wa kisiasa na Rais ni mwanasiasa, pia ni mkuu wa nchi hivyo ndiye mwenye uwezo wa kutoa ushauri na kutoa angalizo pale inapohitajika, hasa anapoona kuna jambo lisilokuwa sawa, hivyo hakuna haja ya kuendelea kusimama kupinga kile alichokielekeza nje ya Bunge.

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kama rais alikuwa tayari ana majibu sahihi ya kinachotakiwa kwa nini aliunda tume na kutumia mabilioni kwa suala ambalo tayari alikuwa analijua .......... acheni uhuni ... rais kama binadamu kafanya makosa... msilete utawala wa nyerere , hakutaka kukosolewa hata penye kosa... usiyependa rais akosolewe ndiyo hauko sahihi... asiyekosolewa ni MUNGU tu.. huyo JK hawezi kamwe kufanana nae.... rweymamu ume loose point kabisa na hufai kuwa mwandishi wa rais sababu huna uelewa wala mantiki yoyote... walio toa maoni yao ndiyo wanahoji kwa nini rais anayapuuza na kuingiza ya kwake? wenye nchi wametoa maoni yao kupitia tume, wameteua kupitia kwa rais wao,,, sasa kwa nini wasihoji ukiukwaji wa rais.. NOTE: rais kaajiliwa tu, nchi sio yake... wenye nchi watahoji tu utake usitake


    ReplyDelete

Top Post Ad