Ndoto ya kufanya muziki kwa asilimia 100 haijayeyuka, bado ipo kichwani mwa Jokate Mwegelo.
Baada ya kushirikiana na Lucci kwenye Kaka Dada, mrembo huyo amedai kuwa mpango uliopo ni yeye kujitambulisha rasmi kama mwanamuziki kupitia kampuni yake.
“Sasa hivi nataka nijiintroduce kama mimi as a music artist,” Jokate alikiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya ambako alienda kikazi.
“Kwahiyo niwe na single zangu mwenyewe ambazo nazifanyia kazi kupitia kampuni yangu mwenyewe, that’s the way forward.