Joyce Kiria 'Chid Benz, Edzen, Dudubaya na TID Mwanamke Hapigwi Ngumi, Mmeishiwa Sera, Kapiganeni na Matumla

Ukatili wa kijinsia haukubaliki hata kidogo, wengine tunapambana usiku na mchana kutokomeza vitendo hivi vya Ukatili na Udhalilishaji, cha ajabu watu maarufu sasaivi wamechachamaa kuendekeza vutendo hivyo..

mara Dudubaya akampiga Mke wake, mara Tid akamtukana RayC, Mara Chidbenz akampiga mzazi mwenzake, mara Ezden akampiga mkewe, mara Chidbenz kampiga RayC!!!! jamani jaman jamani kwanini mnachukua uamuzi huo wa kudhalilisha Wanawake???

ChidBenz, Tid, Ezden na Dudubaya nyie ni vioo kwenye jamii yetu, kwahiyo si vyema kufanya vitendo vya kuwapiga Wanawake na kuwadhalilisha...kwani nyie hamkoseagi? kuna siku mmepigwa? sisi sote ni watu wazima kwa hiyo kama tumeshindwana kila mtu anachukua 50 zake kwa Amani.....

Kuna msemo unasema kwamba Mwanaume wa kweli hapigi Wanawake wala kumdhalilisha Mwanamke kwa sababu Wanawake ni Mama zenu. vitendo mlivyowafanyia hao Wanawake mngependa Mama Zenu wafanyiwe???

ushauri: kama wewe unajiskia kupigana basi ni vyema ukaomba pambano na Matumla, Kaseba au Cheka ili tujue kama kweli wewe ni mpigaji..kinyume na hapo ni kuonea Wanawake na kuwadhalilisha kijinsia....

Nawaheshimu sana kama wasanii lakini naomba mjirekebishe tena kuanzia sasa muwe mabalozi wa Kupambana na vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kwa Wanawake. na muwaombe radhi wale mliowapiga na kuwadhalilisha..

Nawakaribisha sana kwenye kipindi cha WanaumeLive ndani ya Wanawakelive tushirikiane sote kutokomeza vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kw Wanawake..

Ney wa Mitego naomba useme na hawa mastaa wenzako ambao naona hawajasikia ule ujumbe wako kwamba Mwanamke hapigwi na mangumi na mateke...waeleze Mwanamke anapigwa na nini! nakuita pia Linex utukumbushe ule ujumbe wako kwamba ndoa haivunjwi na mwanamke pekee bali hata Mwanaume nae aweza vunja ndoa (mahusiano) si lazima uwe umefunga ndoa.

sasa inapotokea mmeshindwa kuelewana au kukubaliana haifai utumie Nguvu ndidi ya Mwanamke wako.. kama mkishindwana mnaachana kwa Amani, msiachane na kutuachia Mangeu...

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JOYCE KIRIA TAYARISHA KIPINDI ITA WOTE ILI UWAPE USHAURI LIVE.

    ReplyDelete
  2. Waambie hao mafala...tumechoka sasa...

    ReplyDelete
  3. mwanamke akzngua makof tu ndo mwake uzallshaj ndo imekua habar ya mjn saiv na ndo maana wanawake wanakua na vbur coz wanatetewa mpka imeptlza uyo mchaga joyc kiria hamna lolote kpnd chake anawapa jeur tu wanawake zd ya wame zao ushackia wap mchaga akamuheshm mmewe yy anajal pesa tu na mamburula ndo wanamcklza yy utazan mungu matokeo yake ndo wanachapwa tu na wame zao

    ReplyDelete
  4. Ndio maana mnabambikiziwa kesi,mwanaume akikupiga mbambikizie kabaka ndugu yako uone wanavyo haha.akatuliie segerea kwa muda tu atatia akili.

    ReplyDelete
  5. Mwanamke bila makofi hii dunia haitaenda popote.akileta upumbavu wake tandika kofi moja ashike adabu zake.ila sio mpaka umtoe manundu sasa.kibao kimoja tu cha kumfunga mdomo chatosha.

    ReplyDelete
  6. Mwanamke ni kama punda bila bakola hawezi kwenda, wewe joyce kiria si malaya tu wewe ni sawa na kunguru asiyefugika asiyekujua nani?acha kupotosha wenzio.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad