Joyce Kiria: Ushauri wa Bure kwa Akina Bushoke Majumbani Mwetu Tumewachoka

Nimekunwa mnoooooo na hii post ya Mange huko www.u-turn.co.tz hii post nimecopy Kirohoo Safi ukitaka orijino ya Mange nenda www.u-turn.co.tz

MANGE ''Hivi siku hizi ndo imekuwa fashion ndoa zikiharibia mnaenda elezea kwenye media? sijaelewa……''

JOY 'Marioo wanaomba uruma ya watu badala ya kuangalia tatizo la msingi...
Dida nakuaminia mwakani ndoa ya nne, chezea Dida wewe mbona wao wanaoa na kuacha kutwa napenda kuona wanawake nao wakivaa suruali lol…..''

JOY 'Mie nilisema hata 100 ntafunga nini nne'

MANGE ''PS. Wanaume wengine wanachekesha, mtu hela huna alafu unataka kumchunga chunga mkeo, hivi mmenotice kuwa matajiri hawanaga hizo za kuchunga mke?

Maana anajiamini anajua anakulisha anakuvisha huwezi kwenda popote, wasio na pesa sasa? uwiiii ni headache atataka akugande ka luba maana anajua dizaini akitokea mwenye nazo waweza sepa lol……''

JOY ' Fact

MANGE ''Bongo ni noma mwanaume anasema kabisa kwenye video nilimchampa vibao na nikamchapa na mikanda kwenye makalio and nobody does nothing, (Joy ' Halafu tunajiita watetezi wa Haki za Wanawake TZ!) ..

MANGE 'Kukaa ukae kwangu mikanda unitandike, hapana aisee….Joy 'huyo mwenyewe alochapwa hajaenda polisi wala hajasema kitu, hapo utamsaidiaje?

Na kama mtu kama Dida ananyamaza bila kupaza sauti wale weenzangu na mie waoga wataweza kuvunja ukimya kwa Ukatili wanaotendewa? uliona yule mwanamke aliyefumuliwa rasta bila chanuo? nilifuatilia nikaambiwa yule ni mahaba ninyonge!

MANGE ''Nimeona kuna wale wanaosema huyu kaka anaonekana mtu fresh kutokana na maelezo yake kwenye video ila Dida ndo hana heshima, naona nyie hamuwajui wanaume.

Hata siku moja usim judge mwanaume akiwa kapupu, mjudge mwanaume akiwa na pesa. Wakiwa hawana kitu wana jua maadili yote, Quraan nzima wanaijua, dini wanaiheshimu, wake wanawaheshimu yani wewe mwanamke ndo utaonekana chizi.

Sasa subiri apate pesa ndo utamjua yeye ni nani hiyo dini ataiwekea na remix zake mwenyewe na hivi mwuislamu basi akuletee na bi mdogo……'' hapa sitii neno dada Umesomekaaaa ILA UMESAHAU MAHABA YOTE UTAPATA...

MANGE HAPA UKAZIDI KUNIPA GAGA SUKO LA MOYO ''Embu ulizeni wanawake waliotoka mbali na waume zao walioanza nao tangu wanapanda mabasi wengine wanakwambia mume wake alikuwa kashika dini hata pombe hanywi baada ya kuzipata weeeeeeeh ni balaa.

Kwa hiyo hata huyu mume wa Dida lazma awe mpole hivyo na mkarimu na kutaja mambo ya Quran sijui nini, ikitokea siku akapata pesa ndo true colors zake zitatokea.

Lazma awe na busara hivyo mtu unaishi kwa mwanamke alafu ujitie mjanja si ndo maana inabidi awe mpole…..'' NOTED au MSG DELIVAD

HAYA SASAAA MANGE HAPA NDO UMEUA ''Ila na huyu kaka nae iwe fundisho kwake next time aende akachukue mke kijijini amlete mjini, yani mwanamke atamweshimu vile anavyotaka yeye.

Maana akifikiria mume wake kamtoa kijijini kamleta Daslam, kamnunulia weaving hata zile za wachina za sh. elfu 8, uwiii mwanamke mbona atamwamkia na yeye kweli hapo atakuwa baba mwenye nyumba na heshima zote anazotaka atapewa.

Ila akienda tena kuoa mwanamke aliemzidi akaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke alafu afikirie atakuwa anatengewa chakula mezani na kuwekewa maji bafuni akaoge atakuwa hayuko serious.

Amake sure next time yeye ndo provider la sivyo itakuwa kila mwaka anaenda magazetini kulia lia mke hamweshimu……..'' VERY TRUE! kama unataka kumfunga kamba kuku wako kamchukue bushi...

NYONGEZA...
Mwanaume suruali inahusu wakina mama wenzanguuuu? jamani tuache unafiki Mapenzi mwenzake Pesa! wanaojua hivyo tunajituma hata usipopata nyingi lakini unaonekana mtu unavyobangaiza!

Mtu unatakiwa usiwe keroro kwa mwenzako jamani! hakuna mwanamke anaependa mwanaume ambae ni tegemezi jamani eh! Kama ambavyo sasaivi hakuna mwanaume anaetaka mwanamke Goli kipa.

Maisha ya sasa ni magumu sana sana. kwa hiyo pambana ili uweze kulipa japo some bills kwa mahitaji yako na ya familia yako!

Heshima ndo inakuja hapo bandugu! heshima si kucheza ngololo! eti umeolewa badala msaidiane maisha inakuwa ndo umejitwika ZIGO! ni shiiiidraaaa jamani mwe! Bill za maisha ugaramie wewe, za watoto na za mwanaume tena kijana mwenye nguvu zote ugaramie wewe kweeeli! kiruuu haihusu kweliiii...

Mwanamke unajitahidi kufanya kazi usiku na mchana, mwenzako kazi ni kuingia sheli na kwenye mabutiki kwa pesa ya mkewe, kutwa yupo Insta na FB halafu anasubiri na usiku acheze ngololo! halafu anataka akupande kichwani MBUTAAAAAA..Hiyo haipo ivyo...

TANGAZO TANGAZO

TUMESHAWACHOKA NA TUMEANZA OPERESHENI TOKOMEZA MARIOOO NA KINABUSHOKE, TUNATAKA KUWAONA MKIJITUMA KUHUDUMIA FAMILIA ZENU NA WAKE ZENU, Ngololo tumezichoka na zinatuzeesha! Mwanamke tangu ujiozeshe hujui hata mafuta ya AYU toka kwa mpenzi! yaani wewe tuu ndo unamnunulia kila kitu jamani ote mae!

Hii ishu imekuwa ngumu sana kwa sisi wanawake kuiongelea, kazi tumebakia kuongelea masalon, mabotiki na sehemu zingine ambazo tunakutana lakini si kwenye majukwaa na wao wayasikie.

Nimewahi kuwashawishi kwamba njooni kwenye kipindi tuliweke wazi hawa kina Marioo wajijue na wajitambue huenda wakajirekebisha maana tumewachoka, waliruka kimanga! kwa kifupi Wanawake wengi si wote bali walio wengi haya ndo maisha yetu siku hizi.

hadi tunatamani kurudi zamani, ambapo mama zetu kazi yao kubwa ilikuwa ni kuzaa.. siku hizi tunatafuta pesa mpaka dakika za mwisha kabisa yaani mtu unatoka kazini unaenda LEBA kuzaa!

Wanaume kuweni na Huruma! kama haitoshi mahari tunajilipiaga, gauni la harusi twajinunulia hadi suti ya mumeo wanunua Harusi tunafanya Yeleuuuuwiiii!!! kuna Mwanamke mmoja aliniambia kwamba asipoimba yaani asipopata dili ya kwenda kuimba nyumbani hawali..mumewe anategemea sauti ya mkewe tuu.

Mwanaume ana nguvu zake, ana akili zake, tatizo ni USHARO UHARO hawataki kujituma....SWALI TUNALOJIULIZA NI KWANINI HAMPENDI KUJITUMA KUTAFUTA PESA??? MNAPENDA SANA MATUMIZI KULIKO KUTAFUTA PESA NA MNAJIDANGANYA NA NGOLOLO MWE!

Tumeshawachoka kuwabeba sasa tunawatua chini tunawabwaga mazima, na sisi tunadandia wenye kujituma na kutambua wajibu wao kwetu na familia bila kusukumana! yaani kuna watu wanajua kujali jamani, anajali mke hadi watoto.

Kwani sisi hatutaki kula Raha kama MANGE? na sisi tumeshtuka tunataka tuonje Raha babue, mtu unashindwa kwenda hata MIKUMI mbugani! kisa mzigo wa familia umekuelemea hadi unatembea upande na mume unae lakini kazi ni USHARO UHARO!

HITIMISHO
Kwa sasa tunawatazama tuu mnavyogombania Media mkijitetea tuu huku HOJA ya msingi hamuigusi kabisa! bora Shem E hapo kideoni kagusia kidunchu kwamba wife ndo anaprovide na kwamba alihamia kwa wife..

Sasa hapo anajua mlipa pango? na magari je anajua nani kanunua? maana kuna wengine mnapenda kuendesha tuuu lakini hampendi kujua yametoka wapi!.

Yule mwingine nae anajitetea 'oh nilikubali kuwa BUSHOKE kwa sababu nakupena sana!' IVI UNAFIKIRI WATU NI WAJINGA KIASI HICHO? WEWE SEMA KWAMBA ULIKUBALI KUWA BUSHOKE KWA SABABU YA PESA PESA PESA PESAAAAAAAA . kina Marioo Mgombaniege Media salama SISI HATUNA HABAREEEEEEEE.......

NOTE
Sifurahii Ndoa ya mtu yeyote kuparanganyika! napitisha HOJA tuu ujumbe ufike... Maisha yakiwa ni magumu sana Ndani ya Ndoa hata furaha ya Ndoa hutaiona.

Pia tukibaki kutegemea mtu mmoja tuu nayo inachosha sana.. ndo maana tunafika huku kwa kutafuta press kwa ajili ya Ndoa yako.... so tuchukue tahadhari hiyo... Poleni mliopo kwenye tafrani kwa sasa. tujifunze pale tulipojikwaa na si tulipoangukia... AMEEEEN

Quote of the Day

You are always a student, never a master. You have to keep moving forward.

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ujumbe umewafikia wahusika hahaha jamani

    ReplyDelete
  2. Huo ujumbe ni mrefu mpaka una bore kuusoma. Jamani jifunzeni ku summarise hoja. Inawezekana ikawa nzuri lakini dah ni ndefu mno na inajirudiarudia.

    ReplyDelete
  3. Huyo Joyce Kiria si ndio yule mke wa mwanasiasa uchwara. Au sio yeye. Huyu mwanamke ni majanga hajui hata ni kitu gani anachokisimamia katika maisha.

    ReplyDelete
  4. we naye jaribu kupanga point ueleweke. mwandhishi gani unachanganyachanga habari? nukuu zenye umenukuu ovyoovyo, pointi zako pia hazijaeleweka..dah jamani shule nzuri asikuambie mtu.Joyce kiria, kiroho safi acha kujipendekeza kwa mange, hata kama alikuwa na meseji nzuri lakini kwa mtiririko ule naye alichemka tu. we mbona ulisemaga unalipa kodi ya nyumba, sasa hapo tuseme nawe ndo unamhifadhi huyo mumeo naye tumwite marioo? kwanini tusikubali kwamba kusaidiana kutokana na maisha jinsi yalivyo ndo mpango mzima. mume wa dida kukaa nyumba aliyopanga dida haimaanishi alikuwa hachangii garama unless yeye dida athibitishe hilo. huyo mange kutwa na biashara za nguo, si ili wasaidiane maisha na mumewe? hata kama pesa hiyo ni yake lakini badala ya kumtegemea mume kwa 100% mengine utafanya mwenyewe....siwatetei marioo bali nataka niweke wazi zama hizi ni za kusaidiana sasa kama kuna wanawake wameamua wao kuwa ndo bread earner katika familia zao labda hilo ni tatizo lao...inawezekana wamejitongozesha ili waonekane wako kwenye ndoa, au ndo ile kujipendekeza ili mume asikuache....sasa hapo hilo ni tatizo lingine. acheni kupotosha kana kwamba asilimia mia moja mnahudumiwa wakati hata kodi za nyumba mnalipa.

    ReplyDelete
  5. Joyce bhana yan sijui umekunywa mnazi unaanza kupoteza mwelekeo kwahiyo km ww ni mwanaharakat wa wanawake ndio umtete mtu hata km kafanya kosa? fata mambo ya maana ya kujenga jamii angalia usituboe umeanza kutuchefua alafu nshakustukia haupo vizuri kimaadili umeficha ficha lakini jua its too hard to hide nature pumbavu zako!

    ReplyDelete
  6. Hivi ikitokea mumeo kwa bahati mbaya mambo hayajakaa sawa yaani kipato kimeyumba mke akalipa kodi ni mbaya kama mume always huwa analijua jukumu lake na analitimiza?? hiyo ni tofauti na mwanaume anayehama kwake na kuhamua kwa mke na kuanza kulelewa kila kitu kuanzia kodi mpaka mavazi, chakula, transport, bili za maji umeme yeye kazi yake tendo la ndoa tu inahuuuuuuuu achape lapa muda wa kulea ma bushoke umepitwa na wakati. Halafu wangekuwa na nidhamu hao mabushoke wenyewe nyodo kibao na kujidai wakali kisa anajua unampenda so anataka kukunyanyasa hela yako halafu akupe presha kisaaaaaaa dawa yao kuwatimuaaaaa tuuu ili waone chungu ya kusaga lami kutafuta hela ndo watakuwa na discpline.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah mdau hapo juu anonymous 5:09 PM kwa kweli umeua. Maana point zako zimesimama vizuri. Natamani kama ndio ungekuwa Joyce Kiria. Umeelezea vizuri sana na kwa ufupi. Kwa mtu ambaye hajakuelewa huyo atakuwa pimbi. Wasalaamu!

      Delete
    2. Nihivi maisha ndioyanatupeleka huku tulipo now.ni magum kilamtu anajua.ila kwahatuailivyosasa mwanamke akichakarikasana akapata hela hv hlf mwanaume ukawahuna nabado unaleta ujuaji hamuwezi kudum kabisa ktk ndoa.mtaparagana tu yes mume nikichwa cha familia ndio pambana basi ushike madarakayako.usitumie ubabe.namnapokuta wanawake tayari wanamaisha mazuri ukaenda kuoa kubali matatizo.sababu hujui pesa alipatiawapi ukamuona hivyo ukamuoa.sapot unajua ilitokawapi we oa hlf pambana uinuke umzidi heshima itakuwepo tu.hvhv mtalaumu buree.kumbadili mtumZma tabia ni ndoto.

      Delete
  7. jaman mi hata nimeshindwa kusoma. ..summarize pls

    ReplyDelete
  8. Wanawake ni viumbe wa ajabu sana. Wenyewe wanadai usawa duniani lkn wakiupata wanaanza kulalamika. Sehemu nyingi duniani imezoeleka wanawake ndio wanaowategemea wanaume kimaisha. Wanaharakati wakaanza kudai usawa kwamba na wao wapewe fursa ambazo wanaume wanazo ikiwa ni pamoja na kuhudumia familia. Sasa inapotokea familia ya namna hii ambayo mwanaume ni mtegemezi kwa kipato cha mwanamke wanageuka tena na kuanza kulalama. Nilidhani wangeanza kushangilia ushindi wa mabadiliko ya mfumo dume. Huyu Kiria kama angekuwa anajua anachosimamia kamwe asingeshabikia hoja hii. Wanawake wanapodai usawa wakubali na hili pia la kuhudumia wanaume inapptokea. Mbona asilimia kubwa ya familia ni wanaume ndio wanaohudumia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. na kuuzaa na nyie mzae basi siku hizi asilimia ya wanao hudumia ni wanawake na si wanaume.

      Delete
  9. Nenda shule!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Mimi nao wanawake wote tuoe akikuzinguayeye ndio abebe bagi achape lapa muda wa kuabudu wanaume umepitwa mnasemaje wanawake wenzangu? Ila tujitume tufanye kazi kuna siku wanaume watatuheshimu. YES WE CAN

    ReplyDelete
  11. Oyooooooo Chaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. Mapenzi hubeba mambo mengi cna sion mbaya ila vikizidi mno ni mbaya sana

    ReplyDelete
  13. Mmh sikujua Kama huyu Joy nae ni wale2, hivi kumbe malaya anatetea malaya mwenzie, hivi wewe Joy kutetea haki za wanawake ndio mnatetea wanawake Kama Dida!! Basi hii dunia kile kizazi cha mama bora na heshima ya Mama Kama akina Tecla Mjata, kitakua kimepotea kabisa, hivi wewe Joy nae aliekuoa we mdada naona anakufa na tai shingoni bila yéyé kujua, hivi kwa tabia hii ya kumuacha mumeo na kwenda big brother we unaona ni sahizi? Mbona wewe hujaenda, nijuavyo mimi Edzen ni staff somewhere Sasa analelewa vipi hapo, umalaya Wa huyu mdada kupenda nguo za watoto(dogodogo) ndio hivyo zimembana, lol! Hlf siku hizi we Joy unaropoka2 hadi unachosha sijui umerogwa!! Acheni kushauriana ujinga huyu Dida ni bibi bomba sahizi angekaa chini atulie ujana una mwisho na mwisho Wake umefika khaaa!!!

    ReplyDelete
  14. Kwahiyo unavyosema umefurahi, mimi sioni hâta kilichokufurahisha hapo, unahakika Kama pesa anayokupa mumeo kaitolea jasho yote?? Mmh hujui tu ungetulia Joy, hii Dar ni kubwa binti!! na dunia ina mambo hiyo? Haya sisi tunawacheki tu, muangalie hao watoto wenu wanakua mtakuja kukutana kwa bwana mmoja msipokaa chini

    ReplyDelete
  15. Jamani nisaidieni hivi mtoa mada ana elimu gani?

    ReplyDelete
  16. Joy vip?unakula bang skuiz.me sju imliiochangia Mmesomaje mana li habar sjui lihusia alielewek nimeambulia kuzichosha mboni zangu.

    ReplyDelete
  17. Mlevi nini......?Utu wa mtu ni utu wake na si mali

    ReplyDelete
  18. bhaaasi akianzisha mtu kumponda mtu fisi wote hufuata mkondo pumbafu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad