Kanye na Kim K watumia zaidi ya milioni 830 kukodi mtoto anaefanana na North West

Familia ya Kanye West na Kim Kardashian imeripotiwa kutumia $500,000 (zaidi ya milioni 830 za Tanzania) kumkodi mtoto mwenye mwili unafanana na mtoto wao North West (body double) kwa lengo la kuwakwepa wapiga picha.

Kwa mujibu wa jarida la Grazia la Uingereza, wanandoa hao wamewafanyia usaili watoto kadhaa huko Los Angeles na wameweza kumpata mtoto mmoja anaefanana na North West.

“There were auditions held in LA at a specialist agency and in the end they found a child who is the spitting image of their daughter.” Chanzo kililiambia jarida la Grazia.

Imeelezwa kuwa wamepanga kumpata mtu anaefanana mwili na mlezi wa mtoto huyo pia ili waweze kumlinda mtoto wao mwenye umri wa miezi 13 dhidi ya  lens za kamera za Paparazzi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahah tisha...wameanza design ya kama vile watoto wa Michael Jackson

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad