Mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”
komaaa kaka utashinda2 hakuna kinachoshindikana kwa mungu. kama hujabako bas mungu atakusaidia.
ReplyDeleteKabaka huyo ila pesa ndio kila kitu kesi itaisha tu na atarudia ufuska wake kama kawaida.Tabata Kimanga tusha mzoea.
ReplyDeletehe makubw kumbe rapist
ReplyDeleteJamaaa mbakaji kishenzi. Kaishabaka Tabata Kimanga nzima lakini ndio hivyo ana survive.
ReplyDeleteAnonymous 9:37pm ropokaropoka sana omba Mungu yasikukute wewe wala kaka yako hasa Kama awe amebambikiwa
ReplyDeletejamani wadau fikirieni kabla hamjasema chochote kuhusu huyu mtu. iv wewe anonymous 9:37pm unamjua sana unavyosema hivyo?muogope sn muumba wk
ReplyDeleteMtangulize mungu kwa kila jambo,hakuna linaloshindikana chini ya jua.
ReplyDeleteTUMWACHIE MUNGU NDIE ANAYE FAHAMU KUWA KABAKA AU LA TUSIHUKUMU BALI TUWAOMBEE WAWE NA MAISHA MAZURI
ReplyDelete