Kifo Cha Mke wa Askari Aliyefia Chumbani Kwa Dereva wa Bodaboda Utata

Wingu zito limegubika kifo cha mke wa askari polisi wa wilayani Mwanga, Kilimanjaro aliyefia chumbani kwa dereva wa bodaboda. Uchunguzi wa awali wa polisi unadai kuwa mwanamke huyo alilala chumbani huko usiku mzima wa kuamkia Jumapili, siku ambayo maiti yake iligunduliwa saa 12 jioni.

Uchunguzi huo pia unadai kuwa mtuhumiwa ndiye aliyempigia simu shangazi ya mwanamke huyo na kumuita nyumbani kwake kwa dharura.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema jana kuwa baada ya shangazi kufika, alishuku jambo baada ya kuona mtuhumiwa anaweweseka bila kumweleza alichomwitia.

“Akiwa amesimama nje ya chumba cha huyo bodaboda ambaye alionekana kama mlevi hivi, aliona kwa ndani kukiwa na mwanamke aliyekuwa amelala sakafuni,” alisema na kuongeza kuwa shangazi huyo aliamua kusukuma mlango ndipo alipomkuta mtoto wa kaka yake akiwa amelala sakafuni.

“Shangazi aliita majirani na katika hekaheka hiyo polisi waliitwa na kukuta mwanamke huyo akiwa amekufa na ndani ya chumba kulikuwa kumezagaa paketi za pombe,” alisema.

Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi wilayani Mwanga huku taarifa ya chanzo cha kifo hicho zikisubiri uchunguzi wa mwili wa marehemu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad