Kituko kingine alichofanya Balotelli uwanjani hiki hapa

Baada ya kukaa kimya kwa muda mfupi, staa wa soka asiyeisha vituko Mario Balotelli amerudi tena kwenye ‘headlines’ za vyombo vya habari ulimwenguni.
Balotelli ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akijiandaa na msimu mpya kwa pamoja na wachezaji wenzie wa klabu ya AC Milan, jana wakiwa kwenye mechi ya pre season dhidi ya Manchester City, Balotelli akafanya kituko kingine kilichowaacha watu midomo wazi.
Wakati mchezo ukiwa unaendelea mashabiki wawili wa AC Milan waliingia uwanjani na kwenda moja kwa moja kumvamia Mario Balotelli, huku walinzi wakiwa wanawakimbiza kwa nyuma, mashabiki hao wawili walitoa simu na kumuomba Balotelli kupiga nae picha

Balotelli alionyesha kufurahishwa na hilo suala na kutoa ushirikiano kwa mashabiki hao kwa kupozi nao na kupiga ‘selfie’ – kitendo ambacho kiliibua shangwe za kutosha kutoka mashabiki wengine waliojazana kwenye uwanja wa Pittsburgh.
Mchezo huo uliisha kwa Manchester City kuifunga AC Milan 5-1.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ballotelli anakubalika one day atatulia yupo kwa sasa kwenye foolish age. Trust atakuja kuimprove

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad