Kutana na Golkipa wa Ajabu Kombe la Dunia mwenye Vidole Sita Mkononi

Brazil. Inawezekana kuwa Mexico imetolewa ‘kikatili’ kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

Visa vya winga wa Uholanzi, Arjen Robben kujiangusha na hatimaye kupata mkwaju wa penalti vilikatisha safari ya Mexico.

Hata hivyo, wakati ikirejea Mexico City, timu hiyo imeacha simulizi kubwa kwenye fainali hizo, na hasa juu ya umahiri wa kipa Guillermo Ochoa langoni.

Ochoa, ambaye ana umri wa miaka 28, aliwazuia washambuliaji wengi kutikisa nyavu zake, wakiwamo wa Brazil walioongozwa na Neymar katika mchezo ulioisha kwa timu hizo kutofungana.

Kipa huyo alikuwa kizingiti kwenye lango la Mexico, lakini ana kitu cha ziada; ni mwanadamu mwenye vidole sita vya mkono wake  wa kulia.

Ochoa, mwenye umri wa miaka 28 ambaye msimu ujao hana timu bada ya klabu yake ya sasa Ajaccio ya Ufaransa kutompa mkataba mpya, alikuwa kivutio kwa mashabiki wa nchi hiyo kiasi cha wengine kumwita “rais”

Ameichezea klabu hiyo mechi zaidi ya 100. Umahiri wake langoni utaweza kumpatia timu.

Hakuna shaka, klabu za barani Ulaya kama Arsenal na Manchester City zimevutiwa naye, ingawa yeye anapenda kubakia Ufaransa.

Safari yake ya kwenda Ufaransa mwaka 2011 ilikumbwa na kiwingu baada ya kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya. Alikuwa miogoni mwa nyota watano waliokumbwa na kashfa hiyo. Alitiwa hatiani kwa kutumia dawa aina clenbuterol na kufungiwa.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hakuna ajabu hapo Babu yangu alikuwa na Vidole sita

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad