Kwanini Wanawake Wanawahi Kusahau Shida Walizopitia
7
July 08, 2014
Unamkuta binti kijijini kachoka, kapigika hata mafuta ya kujipaka hana anavaa kandambili za kuunga lakini kwa kumuangalia tu ana sura nzuri japo haina matunzo ukioa ukaja nae mjini ukamfungulia kamradi akaanza kupata hela anasahau shida zote za kijijini na kuanza dharau kwa mmewe na akumbuki tena alipotekea, ipo mifano mingi sana ambayo inafikia hata wanaume kujiua kutoka na usaliti wa Aina hii , Sio la kutoka kijijini tu pia hili la unakuta mdada hana hili wala lile anatokea jamaa anajitolea kumsomesha mpaka chuo ila akishamaliza tu chuo na kupata kazi jamaa aandike maumivu ndo basi tena......Dharau mtindo mmoja kashasahau alipotoka......
mademu ndo zao
ReplyDeleteUongo mtupu! unapoedit badilisha basi ni kiblouse Mfyuuuu.
ReplyDeleteYamekukuta?pole wee!
ReplyDeleteHata wanaume ndo zaidi. Unakuta mkaka hovyo tuu...unamvumilia na kumsupport mwishoe anakuletea mwanamke mwenzio. je hiyo nayo ni kusahau shida au ni tabia ya mtu tu. Mi nadhani ni mtu anakuwa na tabia yake..ila hana vifaa vya kuionyesha...akipata vifaa tu ndo anapocharuka. Yaliyonikuta mimi..siwez sahau. so jhata wanaume mmo sana tu kwenye huo usahaulifu wa walikotoka.
ReplyDeleteHata wanaume pia, hawana shukurani una mkuta hana hili wala lile, unamvumilia wee akisha pata tu anakuona hufai umetafuta nae ume mvumilia shida zake zote akisha pata ana tafuta wa kula nae, kwa hiyo hata wanaume pia huwa wepesi wa kusahau walipo toka
ReplyDeleteJamani wote nisawa yaan wanawake na wanaume. Ila kilichopo ni wote kujitambua na kuwana msimamo.
ReplyDeleteusioe mtu maskini, ukajidai kumsaidia. tafuta mtu wa class yako.. matajiri waoe matajiri, maskini waoe maskini narudia usijaribu kumtoa mtu kijiji kama unaishi mjini, oa hapo hapo mjini mambo ndiyo yatakuwa sawa
ReplyDelete