Leo naomba mnipe nafasi nijaribu kuwasaidia baadhi ya ndugu zangu Wabongo ambao hawajafika Majuu na wanaota kufika huko, kwenda kutafuta maisha maana wanaamini kule ni Paradise.
Binafsi nilikuwa na hiyo ndoto nikaitimiza na kujionea mwenyewe na nikajifunza kwamba sio kila kinachong'aa ni dhahabu. I was once a believer of that theory kwamba Majuu ndio kila kitu mpaka nilipofika huko na kujionea mwenyewe kwa macho yangu baada ya kuishi huko miaka 30.
- Kwanza ukifika tu kama nilivyokwenda New York City/USA wabongo wenzako hata unaowajua wanakukimbia maana hawawezi kukusaidia, tatizo la kwanza makaratasi ya kukuwezesha kufanya kazi tena kazi ambazo kwenye maisha yako hapa bongo hukutegemea kuzifanya infact ni kwa mara ya kwanza nikaona Singa singa anafanya kazi kituo cha mafuta sikutegmea kuona hayo hata siku moja.
Huna makaratasi na huna pa kukaa kama umeenda kama nilivyokwenda mwenyewe kivyako vyako, itakuchukua miezi kama 6 ya kusota sana ndio uweze kupata ID na Card ili uweze kupata kazi angalau ya kulea wazee au matahira.
- So kwa mara ya kwanza katika maisha yako unakutana na kitu kinaitwa Kodi, au taxes maana hapa bongo tunacheza cheza tu na kodi kule ni serious ishu, panga pangua huwezi kupata mshahara unaozidi Dola 500 za kimarekani kwa wiki kati ya hizo watakukata angalau 100 za kodi so utabaki na 400 tu chumba 150 kwa wiki, nauli ka kwenda na kurudi kazini, halafu unagundua ili upate hgela extra ni lazima ufanye kazi masaaa mengi, so kwa mara ya kwanza unajifunza kuishi kazini maisha yako yanakuwa ni kazini tu,
- Wazungu wana akili sana System yao wameitengeza makusudi kwamba mtu kama wewe mbongo ukienda unaichangia Uchumi wao tu, uwezekano wa wewe kuwa tajiri kwa kufanya biashara kule haupo kabisa unless uuze madawa ya kulevya, ninasema tena uwezekano wa wewe mbongo kutajirika
Majuu ni haupo kabisa labda ujiunge na kuuza madawa ambayo haitachukua muda mrefu watakushika unajua kwa nini watakushika ni kwa sababu Polisi wa majuu wana akili sana wanajua kwamba hawawezi kuzuia kabisa kuuzwa madawa ya kulevya kwa sababu moja kubwa sana nayo ni Law Enforcement ya kuzuia drugs inaajiri karibu wananchi Millioni 2 wa taifa lao.
Sasa ukizuia madawa ina maana hawa hawatakuwa na kazi kwa hiyo wanavyojifanya wanazuia madawa ni waongo sana nalijua hili kutokana na kusoma Criminology nchini kwao, so wanachofanya ni kwamba kwa mfano Mjini New York.
Polisi wameugawa mji mzima kwa vipande vipande na kukata maeneo ya wauza drugs, wanaowajua one on one lakini hawawashiki hata siku kwa sharti moja tu kwamba wasiue au wasuze ile drugs ya kujipiga sindano, kwa hiyo any crime ikitokea kwenye lile eneo polisi wanamfuata muuza drugs mkubwa pale waliomkabidhi eneo ambaye siku zote ana wafanyakazi wengi mtaani kwa hiyo anajua nani amefanya anawaambia.
Polisi mara moja unashikwa, sasa wewe mbongo kwa vile hujui hii system unajiingaiza na kuanza kuuza drugs, mwenye eneo anakujua mara moja na kuwashitua Polisi ndio mwisho wako na Polisi wa Majuu hawana haraka wanaweza kukuwinda hata mwaka mzima nia na madhumuni yao kukamata system yako nzima na watakushika tu.
- Biashara ya halali huwezi kwa sababu kwanza huna capital ya kutosha na besides Wazungu wameshazoeshwa majina makubwa so siku zote wananunua kwenye maduka yenye majina makubwa, pili kodi ni kali sana huwezi kabisa maana kwenye kulipia kodi utashindwa tu so wabongo wengi majuu wanaojifanya kufanya biashara ninasema ni waongo sana always wana biashara nyingine kuliko wanayoionyesha.
- So huna choice ila kufanya kazi tu kama mbwa, ukitoka kazini ni kulala tu na kukaa ndani ya nyumba kuangalia TV hela huna mpaka mwisho wa wiki ukilipwa Wazungu wajanja sana wanakulipa kila mwisho wiki kusudi uweze kuzitumia hela zote by jumatatu ndivyo uchumi wao unavyosimama imara.
Wazungu wanajua kuwa hela wanazokulipa mshahara hazitoshi kwa hiyo wamekutengenezea system ya Credit Card yaani unapewa Card bila masharti magumu ukope, kufumba na kufumbua una madeni kuliko uwezo wako, hatimaye wanakufikisha mahali unakuwa unalipa madeni yako on interest tu bila kugusa deni lenyewe hasa deni linaendelea kuwa kubwa mpaka mwisho maisha yako ni madeni tu,
- Huku home ndugu na jamaa wanakuaminia kwamba sasa upo vizuri kumbe sio kabisa, kutuma hela huwezi wewe mwenyewe huna hela extra maana ile system haikupi hiyo nafasi, so Rafiki yako wa bongo akija unamkimbia maana huna hela extra ya kumsaidia unajificha mpaka usikie amekuwa sawa ndio unajitokeza na kujifanya kumjua sana na kwamba ulikuwa umesafiri, ndugu yako akija unamkimbia maana huwezi kumsaidia hatimaye unakata mawasiliano na home bongo maana huna pesa.
Pole pole unaanza kuwa kama Wazungu ukitembea unaongea mwenyewe kudadeki madeni yamekukaba mpaka shingoni, zamani ilikuwa rahisi ukizidiwa madeni unaenda Mahakamani una-file kufilisika wanakusamehe siku hizi hamna tena hiyo mpaka ulipe tu.
- Sasa unaanza kukumbuka bongo, hapa ulikuwa na kazi nzuri ulikuwa unaweza kula mara tatu kwa siku unaweza kwenda bar kunywa kidogo, unaweza kwenda uwanja wa Taifa kuona mipira mikubwa.
Majuu forget it it will never happen huwezi so huna pa kwenda matokeo yake mbongo mmoja akifanya party ya birthday hata ya mtoto mchanga wote mnakimbilia huko watuwazima unakuta mmejaa nyumbani kwa mbongo, kijumba kidogo mnabanana humo humo na kuanza kupiga picha za kutuma bongo kuwakoga wajinga kwamba upo majuu.
Pale kwenye party inatakiwa uwe very careful kwenye kupiga picha unatafuta angle ya kuonyesha upo kwenye bonge la nyumba kumbe mazishi matupu, umevaa nguo za kukopa dukani kwa credit card, kesho kazini mapema sana so hata pale kwenye party huna raha ila unajifanya kuwa furaha sana kumbe uongo mtupu madeni yamekukaba mpaka shingoni masikini wa Mungu,
- Matokeo yake unaanza kuja kwenye mitandao na kuanza kutukana Serikali ya Tanzania na Viongozi wake kisa na mkasa yamekushinda huko Majuu, na kurudi huwezi wengi wao wanaanza ku-develop tabia za ajabu na kutisha sana kisa maisha ni magumu na sivyo walivyotegemea lakini hawawezi kukubali na kusema wazi maana ni aibu.
Wazungu wametengeneza system yao ya maisha ili wanasheria na madakitari tu ndio wale bataz so wewe ukienda kule bila kusoma utachekesha tu, na uzuri wa Wazungu ni kwamba no matter what utakula tu maana kwa mfano usiku fast food zote wanatakiwa ikifika saa sita kutupa chakula kama kipo hakiruhusiwi kwenda next day kwa hiyo ukienda pale watakupa bure maana hawaruhusiwi kukitupa mpaka wahakikishe hakuna mtu anayekihitaji kwanza ni sheriaa.
- So unaanza pole pole kukumbuka bongo, furaha yako yote haipo tena Wazungu kama kawaida yao hawapendi weusi popote unapokwenda wewe ni nothing but nigga, huna thamani yoyote ni good for nothing halafu maisha majuu ni sheria asubuhi mpaka saa ya kulala!!!.........
OK GUYS KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA NEXT NIKIWA NA TIME KAMA YA LEO WILL DO SOME MORE!!
Le Mutuz
Quote of the Day
You are always a student, never a master. You have to keep moving forward.
acha kututishia ww ww..kama umeshindwa ni ww..acha ufala msenge ww,Lemutuz Lemutuz utakuwa tuzi siku moko
ReplyDeleteKweli kabisa mimi nimetapeliwa hela na jamaa mmoja anaishi Ulaya.Kanishawishi nitume hela aninunulie gari bei nzuri.Miaka mitano imeenda gari kadai liliibiwa na kakata hata mawasiliano,na chenji katia ndani.Nawashauri wote wenye tabia kama ya huyo jamaa yangu mkiona maisha yanawashinda huko majuu rudini nyumbani badala ya kuwa tabia za kitapeli.
ReplyDeleteKwa kweli Le Mutuz hapo umetisha. Wabongo wengi wametaabika na ile hali ya maisha hapo majuu. Wanajifanya kujitahidi lakini ni kwa shida mno. Nilijifunza kwa hilo kwamba kama naweza kutumia nguvu nyingi namna hii katika kupata unafuu hapa majuuu what about nikitumia the same energy and effort nikiwa hapo nyumbani Tanzania????? Unajiona unapoteza muda na nguvu hivi hivi katika Nchi za watu badala ya kuwekeza hizo nguvu pale nyumbani Tanzania. Jamani waTanzania tubadilike. Tafuteni yale ya muhimu huko majuu kama vile Elimu halafu elekezeni nguvu na hayo maarifa mtakayopata pale Nyumbani Tanzania. Hakuna kitu kinachoshindikana. Tusijidanganye na hizi system za huku za kupangusa mavi na udenda hawa wazungu. Hatutafika popote. Jamani majuu ni kwa wale tu ambao wako sawa. By the way kuna discrimination ya hali ya juu. Majamaa huku ni ma racist kishenzi. They don't care sijui babako Waziri au Rais wa Nchi they don't. Wana ku treat kama shit fulani hivi. Jamani rudini pale Nyumbani mshike majembe mkalime. Hiyo at least itakuwa ni jambo la busara sana.
ReplyDeletesasa umeanza kukuwa lemutuz kidogo Leo nimekuelewa jitaid .
ReplyDeleteSasa weka wazi Ni mtanzania gani ambaye hana ujuzi wwte anaweza kwenda mkoa wwte hapo bongo na kulipwa $100 kwa wiki wewe ulikuja kutafuta mabwana sio maisha ndio maana ulikuwa unatafuta pakulala mtu wa chini mtz anatengeza $550 kwa wiki pimbi we
ReplyDeleteHizo hesabu zako ni so fake. Hela unayozungumzia ni before deductions. Tueleze after deductions unabaki na savings kiasi gani. Unless unaishi chini ya mti. Na kama ni kazi ambazo hazina ujuzi ndio hapo tunapo suggest that why don't you go and have your skills uweze kurudi nyumbani na kuendeleza gurudumu la maisha. Don't get twisted bro maisha hapo ni kaputi na sio utani watu wengi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania wako kwenye denial. Ni either wanatamani kurudi makwao lakini licha ya kukosa uwezo wa kurudi pia wanaona aibu ya kurudi kwa sababu hawana kitu cha maana cha kujivunia pale nyumbani. Jamani nyumbani ni nyumbani nendeni pale mkashike majembe mlime duh.
DeleteNa hata nyumbani wako wanaolala chumba kimoja watu sita,tena wengine wanalala stand za mabasi,sio kwa kupenda,na sio vichaa ni hali ya maisha inagonga,kwa ujumla maisha hayana mfumo maalum.ni kuomba mungu,wako watu na elimu zao lakini utawaonea huruma,ni choka mbaya,wako watu hata kuandika jina lake hajui ana maisha ya juu utashangaa.
DeleteHiyo ya kutueleza eti Mtu hajui kuandika jina lake lakini ana maisha ya juu ni sawasawa na mazingaombwe.
DeleteMpuuzi ww kubwa jinga umekaa ulaya ulikua marioo tu story yako tunayo na ulikimbia mke na watoto saiv umerud hapa choka mbaya unakatisha wenzio tamaa kwendraaa...mavi yako
ReplyDeleteWewe uliishije miaka 30?
ReplyDeleteSi bora sisi huku tuwalipwa dollas 500 kwa week.....huko Tz vibarau wanalipwa sh ngapi kwa week ww bweha....hasiwatishe uyo njoo huku tubanane.....kama alishindwa yy kivyake
ReplyDeleteHahaha wewe anonymous "sisi huku tuwalipwa dollas 500." Unatia na huruma. Rudi kwenu ukalime.
DeleteUnakuta waTanzania wengi wanakufa vifo vya ajabu ajabu sana pale overseas. Na sio kwamba hivyo vifo sio preventable bali ni kwa kushindwa ku afford ile health insurance kwa hiyo matokeo yake wanaishia kwenye zile hospitals za vichochoroni kwa sababu hawawezi hata afford ile co-pay au consultation fee. Kama hauko sawa cha msingi ni kurudi kwenu kuliko kuendelea kutaabika kwenye nchi za watu kwa ku kiss ass.
ReplyDeleteBora Kutaabika ulaya ...Kurudi bongo ni tabu MARA 10000
DeleteUkitaka kufanikiwa Ulaya nijitihada yako,,na bidii,lemutuzz anaelezea alivyo ishi na matatizo aliyopitia,maisha ni popote,mimi ninaishi hapa nimesoma nafanya kazi,,na biashara ,nyumbani nimejenga nyumba za kupanga,na restaurant naona maisha ni mazuri kwa upande wangu,nasomesha ndugu zangu,nyumbani,hata bongo kuna wavivu,walevi,na wezi,bado maisha yanawashinda,lemutuzz tutamkaribisha ,atueleze vizuri alivyopigika akiwa new york,state nyingine tuna mifuko yakusaidia waafrika waliofika na hawana msaada,ila k
ReplyDeleteMuongo mkubwa wewe. Tueleze ni kitu gani ulichosomea na ni kazi gani ya maana unayoifanya hapo kama sio desk officer. Ni kinachikufanya usirudi nyumbani na kusimamia kwa karibu hiyo miradi yako kama ni kweli. Acha longo longo zako. Kama wewe ni mkweli na mwenye haki rudi pale Kijijini kwenu ukawasaidie wale waathirika kwa ukaribu zaidi kuliko kupiga zile longolongo hapa kwenye blog.
Deleteili libaba lisiwaongopee me nipo uku Huu mwaka wa ishirin na nna mambo yangu namafanikio nayaona acwaongopee nyoko uyo ukipata zar njoo uzisake kama nikusoma biashara kujiuza no iyo skushaur.
ReplyDeleteMimi nawashangaa nyie mnaodai kuwa mnamafanikio. Sijui ni mafanikio gani ya maana ambayo mnayo versus uhalisia wa mambo. Jaribuni kuwa watu wawazi na kweli kuhusu mafanikio yenu na namna mulivyo yapata. Tusiishie kudanganyana. Hizi ni zama za uwazi na ukweli. Wewe ni mtu unayeshindwa hata ku comprehend lugha yako ya asili. Sasa sijui kwa kuanzia hapo tueleze ni kitu gani ulichofanikiwa.
DeleteBongo ni tambalale.Uvivu,kuendekeza mission(short cut),ulimbukeni wa kujikweza,,kijicho na kurogana ndiyo matatizo yetu.Rudini home wabeba maboksi!
ReplyDeleteAaaaaaahhhhh sasa wabeba maboksi tena?????? Hahaha!
DeleteUnaweka uongozi kwenye miradi yako..sio kila kitu uwepo,kwa hiyo ukiwana mabasi ya kwenda mikoani mwenye basi ni lazima uwepo au unaweka schedule,hapo ndio tunapochemsha wabongo,wahindi wana maduka india na bongo,mbona kazi inaendelea?mlipe vizuri mfanya kazi na uwezo wa kujitawala
ReplyDeleteMaisha ni popote, na uliyoyaongelea wewe sijui lemutuz ni mawazo yako, kuna watu kibao wapo huku na kazi hizo unazozidharau wamewekeza bongo na wanawasaidia ndugu zao na kutoa ajira,ni juhudi zako na malengo, mimi kama naweza fanya kazi mbili mwisho wa mwezi nikasevu $2000 ni za kwangu na ni halali sijamdhulumu mtu wala sijafanya biashara haramu kama zinazoendelea bongo za sembe, na kingine katika nchi kama bongo ni ufisadi uliopitiliza ndo unaowafanya watu kama wewe lemutuz sijui uwe arrogant, asilimia kubwa ya wabongo wana hali mbaya kutokana na kutokuwa na ajira au mitaji ya kuanzisha biashara, by the way lemutuz uliwezaje kuishi miaka 30 states na hukujua yote hayo, your such hypocrite na kingine njoo uchukue wanao uliwatekeleza saa nyingine ni laana inayokufanya uanze kuongea mambo yasiyoleta maana, please come get your children here in america.
ReplyDeleteWewe kweli kama unaweza kusevu $2000 kwa mwezi. Tena bila deductions dah kweli wewe ni zinga la Robot hahaha duh
DeleteNakuonaga boya le mutuz ila leo umeongea kitu cha maana hakuna mfano.. napigia mstari maelezo yako kwa kile kilichotokea miezi minne iliyopita.. mtanzania mwenzetu mwenyeji wa tanga aliishi huko miaka mingi mungu akamchukua.. gharama za kusafilisha mwili wake kuja kuzikiwa huku bongo kumuepusha na kuchomwa moto na wazungu ilikua dola 16.. kama tsh mil25 hivi.. wabongo wanaoishi marekani walishindwa kuchanga.. alichomwa moto.. hii inareflect kipi kinaendelea kule kwa watanzania wanaoishi huko.. japo si wote ila harusi ngapi zenye gharama zaid ya hiyo znafanyika karibu kila weekend bongo hii?? Vijana wangapi wanapush magari ya zaid ya hela hiyo??? Lakini mlishindwa kumsafirisha.. le mutuz umenena.. wabongo rudini tubanane.. home sweat home!!
ReplyDeletemnataka tuje,,kuuza sembe,hatuweze tuacheni na taaluma zetu,wewr susa wengine twala,mfungu unaendelea,lemutuzz, usiuze unga,au usiwe km yule waziri aliye dai Tanzania ni muungano wa visiwa vya unguja na zimbabwe,ndiko unako elekea,makaburi hayajaisha ulaya tutazigwa huku,hata kama hamtakubali uraia wa nchj mbili,wakenya wanatuzidi,alafu mnataka tuje kubanana,tumefanya mengi katika nchi yetu hamuoni,mnajilaani wenyewe,
ReplyDeleteOh Celina piga konde moyo Oh Celina. Oh Celina utafanikiwa Oh Celina............
DeleteWoow! Mimi naishi majuu ila sina hiyo mitihani alhamdulillah. Nafikiri Le Mutu kajiongelea maisha yake yeye binafsi, ila sio watu wote wa majuu wana hali hiyo aise. Mimi kweli nashukuru majuu nafanya kazi masaa kumi kwa siku tano, napumzika vya kutosha, silipwi $400 kwa week!! $400 kwa week unafanya kazi KFC!!!? Tatizo la wabongo majuu wanapenda kufatana fatana kama kumbi kumbi ndio maana maindeleo yako yanakuwa 0. Aise majuu ukiwa na plan zako patamu sana, ila ukiwa mzembe, mvivu, mswahili mwenye kupenda umbea umbea...majuu huiwezi utanalala mika every freaking day! WaAfrika wenzangu kama unataka kuja majuu njoo tu ,usimsikilize mtu ambae maisha yamemshinda majuu. Mimi niko majuu mwaka wa 11 naenda home kutembea kila baada ya miaka 2, nimemjengea mama nyumba na nimejenga nyumba yangu mwenyewe. Majuu sina credit card wala mkopo, nina debit card basi. Naenda vacation kila mwisho wa mwaka nchi hapa hapa jirani. Majuu sio kubaya ila wavivu, kumpenda mteremko and wazembe hawapawezi! Wewe mtugani bongo anaelimu ya sekondari analipwa $400 kwa week!? Majuu kingereza hujuwi , shule zero na unapata kazi na inakulipa poa na unasomesha ndugu zako na unalisha familia. Ivi mtu utoke bongo moja kwa moja New York!! Unawazimu? Asikwambie mtu New York maisha ni ghetto alafu magumu, panya unatembea nao mtaani, ila wabongo wapenda sifa wanalazimisha ila waonekane wanaishi New York. Lol
ReplyDeleteKaribuni majuu mwaego...mtu kama maisha ya majuu yamemshinda ni uzembe wake mwenyewe. Hayo ndio maoni yangu :)
Kaka tuko pamoja . Maneno msumari ayo. Maisha yamekushinda bas ni uzembe na uvivu wako. Kama ukichakarika ndo pale tunapozilisha familia zetu na kuwasomesha na wao wakajiskia raha. ... duh maisha raha sana bana:))))
DeleteMafanikio yapo na mliobaki nyumbani ndio mnayoyaona tuseme ukweli nyumba mnakaa nyie magari mnaendesha na matatizo madogomadogo yanatatuliwa na hao walio nje nasio sababu kusema ulaya hamna mpango sio kweli ila nikutumia akili na kujielewa kwanini upo huku na hutumii akili basi hata nyumbani wapo waliokua na hela sasa hawana kwa stareh....
ReplyDeleteWata starehe wapi wakati majambazi everywhere........mabomu mpaka kwenye Restaurant Kha! Bongo mwishooo
DeleteDu LEMUTUZ umetoa mpya,hayo labda yalikuwa maisha yako binafsi,mi naishi Uingereza na nyumba bongo nishajenga ya maana kwa kulea wazee,bongo nitarudishwa kwa winji Hivi Hivi sirudi ngoooooooooooooo
ReplyDeleteAnampiga dongo Mbuta nanga.
ReplyDeleteJamani Mbuta Nanga kalazwa hospitali. Alidondoka ghafla ana kifafa.
DeleteLe Mutuz sio mchezo. Kampiga kipapai Mbuta Nanga mpaka amedondoka ghafla hajielewi kalazwa hospitali. Anaomba ma mburulazzz wote mumuombeee dua apone haraka. Dah Le Mutuz mwishoooo
ReplyDeleteMmh asante le mutu, kwa jinsi tulivyo sisi wabongo! Kuna watu hawaamini kabisa hadi yawakute, licha ya kuwa baadhi ya wabongo waliojifanya kuzamia meli wanatamni serikali iwasaidie kurudi, na ndio maana wanaenda kushikana ugoni ugenini huko, wewe waache mpaka watoe ta**o ndio watatulia
ReplyDeleteMfano mzuri mange kimambi,kapost pucha za mawigi anauza dola 800 kumbe kaiba picha kutoka kwa @trebellawigs afu huyo trebellawigs ye anauza dola 175,almost mara 4 ya bei? Trebella amemuumbua na amekasirika sana yani.mtu akuibie kazi yako afu auze mara nne yake? Mange kimambi umepatikana mwaka huu,kumbe unavokujaga na nguo zako hua unatuibia sana,sasa umepata komesha yako
ReplyDeleteKil mtu na bahat yake bratha athen unawaenjoy watu ww umetoka kwenye familia bora
ReplyDeleteNipo New hamshire naombeni address nitembelee mitaa aliyo ishi lemutuzz jinga new york ili nioni alivyo adhirika akili.
ReplyDeleteNew Hampshire gani weweee.....pambaffffff
DeleteKilichomdondosha chini Flora Lyimo Mbuta Nanga ni ile severe depression ukichanganya na vya Le Mutuz ndio kabisaaaaa karibia afe hahaha
ReplyDeleteWe unaye taka kilaa MTU aliye uku akwambie anamafanikio gan akil yako mbovu sasa akikuongopea utahakiki VIP we kaa apoapoooo!
ReplyDeleteDuh hii mada ni tamu sana na mimi nna langu la kuchangia. .. ulaya bwana kila mtu anabahati yake na akili yake na kujichakarisha kwako kuyatafuta ayo maisha, ukija ukaruhusiwa kuishi kihalalli na ukahangaika kutafuta kazi bas ata ikiwa ya kusafisha choo, ila Ukiwa utajipanga kuyatengeza maisha ukawa hauna matumizi ya kijinga bas trust me mafanikio u tayari na. . Na ukija ukakaa mda mrefu bila kupata sheria bas na moto utauona ni kugumu kuliko Africa. But at the end of the day ni muhim kujaribu. Njooni tubanane.
ReplyDeletePeter Ligate na wenzake akina Mukama na Dj Luke wa vijimambo wanawadanganya wale watoto pale Marekani eti wao ni mapromota kwa kumleta Diamond. Halafu ukiona concert yenyewe iko feki waswahili kibaoooo weusiiiiii humuoni hata mzungu mmoja. Watoto wa watu wametoka kuwakamua mavi wazungu halafu wao wanaenda kuwatapeli vijisenti vyao walivyovihangaikia yaani mpaka huruma. Na hawa akina Peter Ligate na wenzake ni mapromota feki na uchwara tu. Sio kwamba ni mapromota wa nguvu kiviiileee na tuseme ni ma con artists fulani. Waache huo utapeli wao mara moja.
ReplyDeleteTena huyo Peter Ligate ni tapeli mpaka kwa mavuzi ya mke wake. Na akome na huo upromota wake uchwara. Atafute kazi ya maana ili apate hela zake kihalali. Au akakamue mavi ya wale Wazungu kwani hajakatazwa pambaffffff zake.
ReplyDeleteAfadhali kumskiza Mzazi kabla hujajuta. Majuto ni Mjukuu.
ReplyDeleteJamani Mie mwnyw maunhana na Lemuutz kwa silimia kubwa Sana. Kuna ndugu yangu pia alikaa huko miaka kenda Rudi. Hakuea na msiba nyumbani wala mini, siku ya kurudi amekonda km mbuzu WA jangwani na mbaya zaidi miguu imepasuka sagamba shilingi Mia inazama yote. Alivyokuta chakula vya kumwaga bongo mmhhh....... Tuacheni na Africa yeti bana kwani hatueaoni wazungu wanayoing'ang'ania bongo.....
ReplyDeleteSijawahi ona mwanamke mmbaya kama Flora Lyimo Mbuta Nanga, na alivyo na matatizo kuanzia ya akili mpk ya mwili.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba majority ya watu aliopo ulaya na marekani wana hali mbaya ila uwezo na nia ya kurudi haipo kwa sababu ya aibu!marekani kama alivyosema le mutuz kuuza madawa kwa mwafrika ni ngumu maana hiyo biashara ina wenyewe!ila ulaya wafrica hasa wanaijeria na wabongo ndo waendeshaji..tuseme watu wa kati.sasa kama huna channel hiyo ulaya hufanikiwi!kazi kwanza kwa sasa hakuna;hata zile za maboksi ni dhida hv sasa maana zinafanywa na eastern european!kwa hiyo jamani msimpinge le mutuz hayo ndo msisha ya watanzania waliowengi huku majuu!
ReplyDeleteHuyu jamaa anasema kweli kabisa,nimebahatika kutembea nchi kadhaa Ulaya,Afrika na Amerika.Kwa kweli nikagundua Watanzania unaowakuta huko wengi wao huwa hawana msaada wowote ikiwa ni pamoja na kukupa taarifa/maelezo ya uongo ili tu mambo yako yaharibike wapate cha kusimulia.Nilikaa nchi Fulani zaidi ya miaka miwili kuna binamu yangu hakutaka kabisa tuonane hadi nikaondoka.Watu kutoka mataifa mengine Ghana,Kenya,Gambia hata Bangladesh ndiyo wakawa msaada wangu mkubwa.TATIZO WATANZANIA HATUPENDANI NA JAMAA HAPO JUU KASEMA UKWELI WATU INAWAUMA UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI TU HATA MKIMTUKANA.Kwanza weni wenu huko hamna uwezo wa kumiliki nyumba mnategemea kupanga...!
ReplyDeleteKwa hiyo bora kuhangaika ulaya au bora kuhangaika bongo ? Ma deportee wengi wanaunga mkono what le mutu said sababu wana wivu na waliondoka sio kwa hiyari yao
ReplyDeleteBORA ULAYA $500 KWA WIKI = 800.000 KWA KUKADIRIA TU sasa bongo nani atakulipa hizo pesa ? ni wachache sana wenye bahati hiyo ..
hata wakikata tax am better of living in USA than TZ ..at least naweza kutuma hela ya mboga ngudu zangu wakati milo 3 kwa siku...
Hii inaonyesha kuwa mawazo yako ni short sighted,kama hujui tofauti ya nchi zilizoendelea na za ulimwengu wa tatu ndio hizi,umabidi ufanye kazi kwa bidii,ulipe kodi na kwani hali ya maisha ni ya juu.Umeme upo,matibau hata rais wetu anaenda huko nk.Ulifikiri ukiwa marekani watakujua kuwa wewe ni mtoto wa Malecela?Kule utaonekana mtu wa kawaida huwezi kupewa mikopo kijinga,au kupata privilege yeyote.
ReplyDeleteWewe mwanaume huna issue sana na wa tanzania tulio huku. Wewe kama maisha yamekushinda that's your problem. Baada ya kufanya kazi uka support Familia yako huko kutwa hunatukana watu ambao hujui life zao. Umekalia kuonyesha nyumbani yako ukonga.......nyumba ni yako hiyo?????umeshindwa kuimalizia kwa sababu siyo yako mjinga wewe. Tunajua yako mengi usione tumenyamaza hatutaki kukuhaibisha mbulula wewe. Uki miss united state ndio una Anza mdogo wake huko mkubwa.
ReplyDeleteKweli sio rahisi kama huku kwamba ukivaa tu shati la kijani umeshaingiza pesa,kumbe umegundua lazima ufanye kazi ndio uishi.Ndio maisha ya kisasa unafanya kazi ndio uishi.Baki hapa hapa ule pesa za wananchi,si umeshashona mashati ya kijani?
ReplyDeletewaishio ulaya wamepaniki
ReplyDeleteHatujambo panic huyu mshenzi anatutafuta......maisha yalimshinda akaona akimbo lie huko a likuwa hana mpango wa kurudi aliogopa child support kwa hiyo akaona akimbie....ndio maana ana hasira na sisi shenzi type.
DeleteHatujapanic.....huyu Jamaal anahuzi......Anadanganya sana. Hiyo life yeye ndio Kai pitiable sio kila mtu, yeye hakurudi nyumbani kwa hiyari, I libido harudI kwa sababu mwanamke alim divorce Wakaanza kumfatilia child support kwa hiyo hasira zote anatuchukulia sisi tulio majuu. He was not ready to go home period. Tunajua mengi yake mwambie any amaze kaka hatujamuanika humu. Mbulula na Bichwa kubwa, Babu wewe.
Delete