Katika gazeti la Tanzania Daima toleo na.3536 la tarehe 30 Julai, kuna habari inayosema Lowassa aibukia ACT na kumuhusisha na Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA) Zitto Kabwe katika kile gazeti hilo kilichodai mikakati ya siri dhidi ya Chadema.
Habari hizo ni uzushi, na ni muendelezo wa mikakati ya kumchafua na kumgonganisha Mh Lowassa na wanasiasa wenzake wa kada na maeneo mbalimbali.Mh Lowassa kama walivyo wabunge wengine wa CCM amekuwa na uhusiano na wabunge wenzake bila kujali tofauti ya vyama vyao.
Mh Lowassa ni kiongozi makini ambaye hawezi kupoteza muda wake kujiingiza katika masuala yasiyo na tija kwa nchi, wananchi na ustawi wa demokrasia makini na endelevu nchini.Muda wake anautumia kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM jimboni kwake Monduli. "Mimi na chama chetu, tuko busy kutekeleza ilani yetu,kuwaletea maendeleo wananchi ili wazidi kutupa ridhaa ya kuwaongoza katika chaguzi zijazo" alisema Mh Lowassa.
Hata hivyo,Mh Lowassa anathamini mchango wa vyama vyote vya siasa nchini pamoja na Chadema katika kujenga demokrasia yenye tija kwa taifa.
Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa(mb
Rais,mtarajiwa umeshapata,, ila tunakuomba waziri mkuu wako awe magufuli
ReplyDeleteAdmn unazidi kuchanganyikiwa kuandika comment hii ya kumsifia Lowasa.Kwa taarifa yako lowassa hasafishiki.
ReplyDeleteLowassa mnamuogopa nini?????? Mkiona anakuja vizuri kisiasa mnasema hasafishiki', huku ni kumjengea zengwe, safari hii tayari amekwisha takaswa muacheni aikomboe Tanzania, TUMECHOKA NA MANENO BILA UTEKELEZAJI, KARIBU LOWASSA MTEKELEZAJI UTUKOMBOE.
DeleteAt this juncture we need a person of his character. Non other than him.
ReplyDeleteMwizi tuu huyo! Utajiri.wote kapata wapi????
ReplyDeleteMwizi tumpeleke ikulu kufanya nini? Si abaki kwenye biashara awwachie wazalendo kuongoza nchi
Bora magufuli awe rais, kuliko huyo bingwa WA ufisadi.
ReplyDelete