Maamuzi Gani Nichukue Dhidi ya Ndoa Yangu?

Mimi ni mama wa watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita, mwanzo kabisa maisha yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo, first of all niliwahi kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya hapo niliishi maisha ya tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza kujitambua.

Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na mwanaume niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndio atakayenifuta machozi na huzuni zangu.

Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya mahusiano yetu alienda oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata mawasiliano kabisa. Nilibaki na kovu na maumivu niliyokosa tiba. Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua kumove on na maisha yangu,ingawa ilikuwa ni ngumu sana.

Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye sikujua kama ni kweli nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa namuwaza X wangu aliyeniacha bila kusema neno lolote.

Mwanaume huyu mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na mkorofi kwa watu dakika mbili alishabadirika haeleweki kama kinyonga ,police kwake ilikuwa ni kama nyumbani.

Nyimbo zake mara nyingi zilikuwa ni za kina Tupac ,Snopy D na wale aina ya magang star Ingawa alikuwa msomi na kazi nzuri,na maisha yake mpaka sasa bado miziki yake ndio hiyo ,starehe kwake hataki kuacha wala kupunguza.

Niliamini atabadilika ingawa nilikuwa nakwazika sana kuwa nae alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa mnywaji mzuri na ili niwe nae Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio nakuwa huru na hayo ndio yakawa maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano ya muda mrefu hatimaye nilianza kumzoealakini si kumpenda ,

Tukiwa tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana kuanza kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi lakini kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwa akiniacha na kurudi usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku hadi siku.

Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baada ya kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua kabisa mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa najiuliza kwanini nafunga ndoa? 

Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama najifosi kufanya. Tulifunga ndoa takatifu nakuanza kuishi kama mke na mme ,na mungu akatujaalia kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini system yangu ni mpaka ninywe ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme wangu.

Ndani ya ndoa yangu nimekuwa nikiishi kwa kujifanya nampenda mme wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa nikilia na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake of my kids ndio napata faraja kidogo.

Kila siku zinavyoenda nazidi kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi mpaka lini nifanye nini ili nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa usingizi usiku kucha.
Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu unazidi kuwa mnyonge 

Nisaidieni juu ya hili 
By Ndoa Yangu JF

Quote of The Day:

I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Post a Comment

34 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naitwa Dr.Mathias,ningependa kukusaidia kwa ushauri wa kina.Mwanzo ulikuwa na uoga wa kuwa mpweke baada ya kubakwa,hiyo ilikuathiri kwa kiasi kikubwa kisaikolojia,ulipopata mwanaume wa kwanza huyo alikutoa kwenye wimbi zito la upweke na ndio sababu kuu ya wewe kumpenda.Alipoenda,ukawa mpweke kwa mara nyingine kwa matumaini ya kwamba atarudi hivyo ukaendelea kumpenda kama wakristu tunavyompenda Yesu.Umeolewa sasa ni mwaka wa saba,ni vyema ukifuta ndoto za huyo unaemwamini kuwa atarudi na ujifunze kumpenda na kumthamini huyo gangster,Sababu kuu ya kusema hivi ni kuwa kwa tabia uliyoielezea asingekujali na kukupenda hata miezi 2 usingemaliza.Mapenzi ni kuamua,kuna wenzio waliopenda kwa dhati zaidi ya wanaume hata 5 na kuolewa na wa 6 na wanawapenda na kusahau wale wote wa5!na hata wakipigiwa simu hawataki mawasiliano nao,hivyo kupenda ni kuamua.Amua sasa,mpende mumeo kwa dhati,acha asikilize miziki yote hata ya kina 50cent na eminem but deep inside he loves u,he kept u wt him this long u must respect &appreciate that kuna wanawake wenzio wakikuona wanawish wangekuwa wewe,hivyo usicheze na kilicho mkononi kwako sababu hujajua utajisikiaje kikipotea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafadhali Dr tunaomba mawasiliano yako tuko wengi hatuwezi post matatizo yetu in public

      Delete
    2. Dr.mawasiliano tafadhali

      Delete
    3. +255658-511156 Dr.Mathias

      Delete
    4. well said, DOKTA, ni maamuzi tuu, amua

      Delete
  2. Dr niko na wewe kabisa,asnte kwa kumsaidia mdau,Mungu ahidimiwe!

    ReplyDelete
  3. mi nafikir achana na huyo bwana ili ukaish maisha yako na wanao mana raha ya roho ni kuiridhisha other wise hautakua na raha ya dunia pole kwa hilo

    ReplyDelete
  4. Dr I'm so impressed wic yo advice.coz angekua mwingne angemwambia amuache tu.

    ReplyDelete
  5. Iyo ni kweli alivyo sema Dr apo juu,pia Nani Dr,nafikilri kwatatizo kama hilo siwezi pinzana naye,kwa ushauri zaidi tafadhali,piga sim kupitia Namba zi fuatazo out of U S A +1717-330-2349. Kama upo U S A use the same #

    ReplyDelete
  6. Dr. is right. mdau naomba ufikirie maisha ya upweke yanavyokuwa, fikiri mangapi bila yeye huwezi Fanya. Ndoa ni kuacha yako na yeye kuacha yake mkachukuliana. wapo wanawake wengi wenye majanga tena makubwa kuliko we we lkn wamejifunza kuchukulia mizigo na wanna amani.. pia wanaime nao wana matatizo mengi tu. wanapata wanawake vimeo lkn wanavumilia. Kubwa ni kuchukuliana. Tatizo bado unamlinganisha name yule uliyempenda. Mkubali na mpende utaona matokeo mazuri. Mweleze hat a Yale unayotamani kufanyiwa atafanya tu. Huenda hajui unataka nin., uguswe wapi, Hakka naamini ukiwa wazi mambo yatabadilika.

    ReplyDelete
  7. Dokta umemshauri vema! Mungu akubariki kwa ushauri wako wa busara, jifunze kumpenda mumeo utaona raha ya maisha. Mapenzi si ya kuzaliwa bali yanatengenezwa....tengeneza mazingira ya kumpenda mumeo...utampenda na ndoa yenu itadumu. Mungu aibariki ndoa yako

    ReplyDelete
  8. Dokta umemshauri vema! Mungu akubariki kwa ushauri wako wa busara, jifunze kumpenda mumeo utaona raha ya maisha. Mapenzi si ya kuzaliwa bali yanatengenezwa....tengeneza mazingira ya kumpenda mumeo...utampenda na ndoa yenu itadumu. Mungu aibariki ndoa yako

    ReplyDelete
  9. Sikubaliani na huyo Doctor kwa asilimia 2000. Huwezi kuwa mtumwa wa mapenzi ukitarajia maisha yatakwenda. Hakuna kitu kama hicho. Mapenzi ni two way traffic. Ni lazima watu wote wawili wapendanao wa compromise on each other terms. Huyu mwanamke anaonyesha ku compromise na huyo mjamaa wake lakini kwa upande mwingine huyo mjamaa inaonekana hayuko tayari ku compromise na huyo mke wake. Huo ni utumwa ndani ya mapenzi. Kitu ambacho ni hatari kwa afya ya wote wawili. Ushauri wa ya kuwa huyo mwanamke ni lazima ajifunze kumpenda huyo mwanaume kisa eti sio rahisi kumpata aina ya mwanaume anayemtaka. Huo ni ushauri hafifu na hauna mashiko. Kwa maana nyingine huo ni unyanyasaji mkubwa wa Kijinsia. Kwa nini huyu mwanamke aendelee kukaa kwenye Ndoa anayoithamini lakini mwenzake haoni na wala hakubaliani na mwenzake. Hiki kitu hakiingii akilini kwa mtu yeyote anayetumia busara katika hilo jambo. Na actually hii haijalisha ni upande gani. Kwani awe Mwanaume au Mwanamke yote ni sawa. Huu ni unyanyasaji. Kwa ushauri wa haraka ni as long huyu jamaa amekataa kukubaliana na hisia zako juu yake ni obvious hakujali na wala hana upendo wa dhati na wewe. Kwa hiyo Dada yangu achana na hizo dhana ambazo hazina mashiko. Jiamini na uanze kuchukua hatua za haraka sana za kujiondoa katika huo aina ya uhusiano ambao hauna uhai. Na hizi hatua ni muhimu kuzichukua haraka sana iwezekanavyo kwa sababu za kiusalama na afya yako na hasa hao watoto wenu. Kwani watoto ndio viumbe muhimu vya kuzingatiwa kuliko kitu kingine chochote. Jenga imani, jiamini na move on. Huyo jamaa ni hatari kwako na watoto wako.

    ReplyDelete
  10. Halafu wewe Doctor uchwara una hoja dhaifu ambazo sijawahi pata kusikia.Eti kwa tabia aliyoieleza huyo mhusika ni kuwa huyo jamaa asingemjali wala kumpenda katika kipindi kisichozidi miezi 2. I mean huo ni upuuzi. Na pia ni hoja dhaifu. Kwa mtu yeyote anayempenda na kumjali mwenzake ni pamoja na kuzingatia na kukubaliana na hisia za mwenzake. Kitu ambacho huyu jamaa ameshindwa kukionyesha. Na pia unajuaje kama huyo mjamaa ana take advantage ya unyonge wake huyo Dada. Ushauri Dada kaza buti na uchomoke haraka sana wewe na watoto wako. Kuendelea kung'ang'ania kwenye huo uhusiano hutakuwa umewatendea haki watoto wako. Watu wanaozingatia mahusiano ya maana katika mapenzi wako wengi. Na Mungu atakubariki siku moja utakutana naye tu. Achana na hao matapeli wa mahusiano ya mapenzi. Unless uko so desperate na mwanaume.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hakuna kilichokamilika chini ya jua wewe mwenyewe haukuwahi kumpata unayemtaka kwa asilimia mia.

      Delete
    2. Ni kweli mdau. Lakini haina maana ya kunyanyasana eti kwa kisingizio cha mapungufu ya Binadamu. Hakuna kitu kama hicho mdau. Ni lazima uijali ile Welfare yako. Na hasa kwa wale watoto.

      Delete
  11. Ni mtu ambaye yuko desperate ndio ataendelea kukaa kwenye hiyo aina ya relationship. Kwa mtu yeyote anayejiamini hawezi kukubaliana na huo ushauri wa kipuuzi na kipumbavu wa anayejiita Dr.Mathias

    ReplyDelete
  12. Halafu ukitaka kujua huyu ni Doctor uchwara angalia jinsi ambavyo ameshindwa kutueleza yeye ni Doctor anayetibu magonjwa gani. Kama anatibu pumbu ama kuma ameshindwa kutueleza. Pia ameshindwa kutueleza ni Hospital gani anafanya kazi. Ameshindwa hata kutuwekea email address yake. Kitu kingine cha kushtua ni kuwa ameanza na anonymous hala pale chini anajitambulisha kama Dr.Mathias.
    Jamani huu ni utapeli. Huyu jamaa siwezi kumtofautisha sana na Mbasha. Pamoja na kujua matatizo yote ya Mke wake yeye bado akaendelea kung'ang'ania na hiyo Ndoa. Matokeo yake nadhani kila mtu aliyaona. Ni kutombewa mke wake na gwajima na hatimaye akaishia kulialia kwenye vyombo vya Habari.

    ReplyDelete
  13. Dada na Kaka zangu. Unapokuja mgundua mtu ni mnyanyasaji katika mahusiano usisubiri kitu. Fungasha kilicho chako na uondoke haraka sana. Kwani tabia ya mnyanyasaji huwa haibadiliki. Mtu ambaye ni mnyanyasaji ataendelea kukunyanyasa tu. Hata umlambe matako mara 1000 bado atakunyanyasa tu. Hiyo ndio tabia ya watu ambao ni wanyanyasaji katika mahusiano ya mapenzi. Kwa usalama na afya yako ondoka. Usisubiri majanga.

    ReplyDelete
  14. nimependa ushauri Wa Dr. matias ni kuamua kumpenda na kila kitu kitawezekana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kupenda ni muhimu mdau. Lakini mpende akupendae. Usilazimishe. Kwani ukilazimisha utaishia kwenye majanga.

      Delete
  15. nimependa ushauri Wa Dr. matias ni kuamya kumpenda na kila kitu kitawezekana

    ReplyDelete
  16. Dk kachemka...hata kama mapenzi ni kujifunza/kubadilika kutokana na jinsi mwenzio alivyo hiii ni too much...tangia cku ya kwanza kuanzisha mahusiano yao alishasema hampendi mbaya zaidi mpaka wamezaa then wameoana stil hampendi....sa czani kama kuna dawa zaidi ya kumkimbia tena hara sana...otherwise dada utakufa kifo cha ajabu sana.....

    ReplyDelete
  17. Jamani msimdanganye mwenzenu...Dkt amemshauri vzr sana kwa sababu angekuwa ni mtu asiyemuhitaji katika maisha yake wasingefunga ndoa na kuishi pamoja muda wote huo wa miaka 7. Ushauri wangu kwako mdada akili iwe kichwani mwako...wengine ni mashetani ndio maana wanakuashauri muachane. Fuata ushauri wa dr ujifunze kumpenda mumeo kuanzia sasa na kumsahau yule X wako utafurahia maisha yako na mumeo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Soma ile article vizuri na ujaribu kuielewa. Huyu Mdada sio kwamba hampendi yule mjamaa. Anampenda sana. Na ndio kwa maana unaona ameweza kumvumilia kwa muda wote huo pamoja na mapungufu makubwa aliyokuwa nayo huyo jamaa. Kimsingi huyu Mdada maji yamefika shingoni hawezi tena kuendelea na uvumilivu wa mtu ambae ameshindwa kujali hisia zake. Huyu Mdada ni muathirika wa tabia mbaya na mbovu za huyo mumewe. Kibaya zaidi ni kwamba anaathirika akiwa na wale watoto wa kulea.

      Delete
  18. Sijui akina dada wameumbwaje. Lakini ni jambo la kusikitisha hasa kwa wengi wao ambao licha ya mateso na manyanyaso wanayopata ndani ya mahusiano ya mapenzi lakini ndio kwaaanza unawaona wameshikilia uzi. Kwa kweli wanawake ni watu wa kuwahurumia tu.

    ReplyDelete
  19. Kwa wale akina Kaka na akina Dada ambao mko kwenye mazingira kama hayo. Amkeni, fungueni macho ili muone. Acheni tabia za kuwa ving'ang'anizi. Mazingira ya namna hiyo hayana Maendeleo. Muda mrefu mtakuwa mnajadiliana vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu badala ya Maendeleo. Mazingira ya namna hiyo ni full of Drama asikudanganye mtu.

    ReplyDelete
  20. Mummy so what your heart says Marriage is being happy nani kasema ndoa ni kuvumiliana kama mtu habadiliki na hataki kubadilika just start afresh bwana tusidanganyane kuna watu ambao huwezi kuwavumilia jamani lol walioko kweny ndoa wanaelewa

    ReplyDelete
  21. Jamani Wema Sepetu majanga. Kakataa kwenda kula kuku waliotayarishwa na Steve Nyerere. Akaamua kuwafuturisha waislam na champagne hahaha yule mtoto balaaa. Yeye na aunt Ezekiel wamemuogopa Kajala.......Cheza na Kajala wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha kuleta umbea..changia mada...pumbaaffffffffffffff

      Delete
    2. Umbea babako kwani uongo...cheza na Kajala wewe.

      Delete
    3. napita yawezekana nashindana na chizi.......

      Delete
  22. Fikiria unaishi na Mwanaume au Mwanamke halafu hakuna hata jambo la maana mnaloshauriana. Kunakucha Kunakuchwa maisha ni yale yale. Hayasongi. Mnabakia hapo kutizamana kama vile robot. Wote baba na mama akili zenu mgando. Kwa kweli maisha ya aina hii yanata moyo. Mtapata vipi Maendeleo kwa mtaji huoooo???????

    ReplyDelete
  23. Guys huyu dada hakusema kama anampenda mumewe alisema alianza kumzoea na sio kumpenda and this guy pia he seems to be careless katika mapenzi kiasi kwamba haoni kama mkewe hampendi ila amemzoea....nadhan yawezekana way back mwanaume pia labda alishakuwa hearted kwa hiyo anaogopa kupenda kwa ushauri we dada mumeo pia atakuwa anatatizo sycologically u two guys both u need to seat down and talk and futher more u need to see a relationship specialist ili kila mtu afunguke anavojiskia maana naona wote wawili mnasecret ambazo zinawafanya muwe na hizo tabia...Ni hayo tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad