Mabingwa wa soka nchini Uingereza Man City, wameingia kati mazungumzo ya mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast, Didier Drogba ambaye kutwa nzima ya jana alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kurejea kwenye klabu ya Chelsea ya jijini London.
Man City, wameingilia kati mazungumzo kati ya pande hizo mbili kutokana na hitaji lao kwa sasa la kuziba nafasi ya mshambuliaji wao kutoka nchini Hispania Alvaro Negredo, ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu kutokana na jeraha la mguu linalomkabili.
Mabingwa hao wa soka nchini Uingereza, wanaamini Didier Drogba ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, atafaa kuziba pengo lililopo kwenye kikosi chao.
Hata hivyo bado jibu kamili la nani atafanikiwa kumsajili Didier Drogba lipo moyoni mwa mshambuliaji huyo mwemnye umri wa miaka 36.
welcome back to chelsea club hommie we daimn need you.. ... ..
ReplyDelete